Kuna njia nyingine ya kupunguza uzito?

Mkuu umesema vizuri ila hapo kwenye usingizi ikifika saa 5 usiku mimi hua kichwa kinakua kizito yaan hapo naweza nikalala na nisijijue km nimelala nitakoromaa hapo wee mpaka nishutushwe au nishutuke mwenyewe kwa hio hapo kwenye usingizi ni mtihani mwengine ila hivyo vengine nitajaribu nitakupa mrejesho
 
Mimi ni mnene ila sio fala mkuu nachukia sana mtu kuniona mimi fala

Neno fala umeanza kuliandika wewe kwenye uzi wako ndio maana swali likaulizwa unene na ufala vinahusiana aje
 
Mimi nakula kawaida sana mkuu ila siwezi kukaa bila kula hofu yangu ni hio yaan nikishikwa na njaa lazima nile na njaa inashika muda wowote

Ukipatwa na njaa lazima ule
Utapunguaje sasa
 
Neno fala umeanza kuliandika wewe kwenye uzi wako ndio maana swali likaulizwa unene na ufala vinahusiana aje
Ndio nimeuliza kwani kua bonge ni ufala?
 
AChana na Ubwabwa na Chai ya sukari asubhui!, unaweza ukaskip breakfast ukala mchana tu na usiku chakula kidogo, ukipiga na jogging kimtindo itakuwa safi.
Tizi napiga sana mkuu yaan kwenye kupiga tizi hapo naweza nikapewa medal 🏅
 
Hapa umenena jambo mkuu kwa hio ukitaka upungue haraka unabidi ufanyeje? Kwa experience yako wewe
Kwanza, punguza kula wanga sana, kula matunda na mbogamboga(siyo zile za kukarangiza zilizojaa mafuta kibao, mboga simple tu) iwe sehemu ya maisha yako, mboga na matunda ni muhimu Kwa afya na pia vitaweza kukufidia Kwa kiasi ile sehemu ya wanga uliopunguza kula.

Pili, acha kula au punguza Kwa kiasi kikubwa kula junk foods, hizi hazifai kabisaaa, dada zetu karibu wote wana vitambi sababu ya chips, kuku za kukaanga, chipsi yai and the likes.

Tatu, acha matumizi ya vinywaji baridi na vyenye sukari nyingi mfano kama hizi soda, beer nk. Kinywaji chako ni maji tu tena ya kutosha kabisa. Acha vilevi vyote kama unatumia

Nne, Acha kula nyama nyekundu Kwa wingi. Nyama ya kula ni nyeupe tena si za kukarangiza kwa kiasi kikubwa. Hapa ndipo gharama unaweza kuingia baadhi.

Tano, Fanya mazoezi ya kutoa jasho kweli kweli, kama push ups huwezi basi jifunze, kimbia sana nk.

Sita, Punguza stress Kwa kiasi kikubwa. Stress hazizuiliki lakini kwanini zizidi?, basi tafuta njia ya kupunguza stress zisiwe mzigo.

Saba, Pata usingizi wa kutosha Kila siku, huwezi kufika lengo kama unalala Kwa kubahatisha, kinachohitajika ni ubora wa usingizi wenye muda mwingi wa kujipumzisha, jiwekee ratiba.

Nane, kuwa na muendelezo, siyo baada ya miezi sita unaacha unakata tamaa na hii ndio huwafanya watu wasipungue kilo zao.

Tisa, Anza kufunga Kwa muda Fulani kama wafanyavyo waumini wa dini au punguza Milo mathalani unakula mara mbili tu Kwa siku, hii nayo husaidia sana.

Kinachotuua ni misosi tu, mazoezi watu wengi hufanya lakini Bado mfumo wao wa kula ni ule ule, huwezi pungua hata ufanyie mazoezi mbinguni.

Wanasema kuwa "Weight loss is a journey and not a race"
 
punguza misosi ya wanga,
sukari na matunda yenye sukari nyingi
Halafu jitahidi kula yako iwe mwisho saa kumi kamili jioni hakuna kula mpaka kesho yake
 
Nilifikiri umekosea kuandika ukitaka kumaanisha chai. Kwa kweli Chia sizifahamu ndio nimesikia hili neno leo, hata muuliza swali anaweza kuwa hazifahamu, tueleweshe mkuu, ikiwezekana kwa picha kabisa
Mkuu Google utaziona ni ndogo kama ulezi ila zinatofautiana rangi
 
Punguza kula vyakula vyenye sukari Kwa wingi, piga mazoezi hakikisha unakimbia 3km , piga push up si chini ya 200, kunywa maji mengi na mboga mboga Kwa wingi
 
Kumbe tatizo lipo hapa
Sasa bila misosi misosi tuashije mkuu mimi nikikaa masaa mawili tu wadudu wa njaa wanaanza kuimba tumboni kwa hio lazima nile, sasa nitafanyaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…