Kuna ulazima hayo mashindano ya Quran yafanyike Mkapa Stadium? Siku ya mchezo Simba vs Orlando!?

Hakuna anayesema hayana muhimu, Ila kwa nini lazima yafanyike uwanja wa Taifa yasifanyike hata uhuru?
Ndio Mana vilabu vinatakiwa viwe naviwanja vyao.Unaambiwa waliotangulia kukodisha ni waislamu wameulipia na risti zote wanazo na walianza kutoa matanganzo.kisha mtu akuhamishe kirahisi rahisi .

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Mashindano ya Qur-an ni bora zaidi ya huo upuuzi wa mpira wa simba na orlando,Uwanja ni wa taifa na unatumika kwa watanzania wote wawe waislamu au wakristo...mleta mada una chuki na uislamu na bado uislamu utazidi kupaa juu zaidi na mtabaki mnashangaa kama kule Times Square,Hoja za hovyo eti watu watatokaje uwanjani baada ya mashindano kuisha,hakuna muislam anayeweza kujaribu kujificha eti aangalie mpira bure..ilhali kaenda kwa dhati kabisa ya moyo wake kusikiliza maneno matukufu ya Mola wa ulimwengu huyo atakuwa kafiri na sio muislam..naamini baada ya shughuli kuisha watatoka wote ili kupisha wapenda mpira kuingia...uislamu ni dini ya haki hivyo hatuwezi kudhulumu haki ya mtu siku hiyo.
 
Waislamu wana mambo ya ajabu sana kwenye kila jambo lao, hata mtaani wanafunga barabara ety kisa cjui visherehe vyao vya kupotezeana muda.
Cheki zenu dhidi ya uislam hazitoisha mpaka kiyama hilo tunalijua, na uzuri wake ni kuwa tumefundishwa jinsi ya kuishi na nyinyi bila shida.
 
Hakuna anayesema hayana muhimu, Ila kwa nini lazima yafanyike uwanja wa Taifa yasifanyike hata uhuru?
Ule uwanja ni kwa ajili ya shughuli za kijamii, ili upewe ruhusa ya kuutumia kuna taratibu za kufuata.
Wanatumia hapo kulingana na mahitaji yao, hususani wingi wa watu wanao hudhuria shughuli hiyo. Uhuru ni mdogo.
Kingine ni hivi kipindi wanapewa kibali cha kutumia eneo hilo ratiba ya mechi ya simba ilikuwa bado haija pangwa tarehe.
Kikubwa ni kwamba tujifunze kutatua mambo yetu kwa busara, wakae pamoja pande zote waone jinsi gani watalitatua jambo hilo, mihemko haitosaidia chochote zaidi ya kuleta chuki katika jamii.
 
Mimi nimefunga sipo hapa kwa ajili ya matusi na kejeli na wala siyo mpenzi na mfuatiliaji wa hayo mashindano ,ila naona wana Jf(baadhi ya wakirsto) inapokuja maada inayohusisha na Uislamu hata kwa asilimia 1 mna chukua advantage ya kutukana hovyo na kwenda pakubwa nje ya maada iliyoletwa kiasi ambacho kinapelekea kukosa pasi na UADILIFU

Hapo uwanja wa Taifa miaka ya nyuma matamasha ya injili ya 'Msama promotion' kuna kipindi yalikuwa yakifanyika kila mwaka na hayo mashindano ya Qur'an kwa miaka mingi yamekuwa yakifanyika hapo
 
Lakini ule ni uwanja wa michezo, Je hayo mashindano ni sehemu ya michezo?
 
Haina shida..quran itasomwa na simba itafuzu nusu fainali..
 
Kwan si kuna viwanja viwili?
Why wasipelekwe shamba la bibi wabaki kung'ang'ania wa taifa (lupaso) kama watt wadogo
 
Samia anachanganya dini na serikali.Anaharibu hii nchi,Jesuit mko wapi?okoeni hili taifa dhidi ya 'Nebukadreza'.
 
UWANJA NI WA SERIKALI NA IMETOA IDHINI YAFANYIKE MASHINDANO YA QUR'AN...Simba wangekuwa na uwanja yasingetokea haya
 

Sizan km unajua ulichoandika
 
Na ikumbukwe kuwa haya mashindano ya quran hayana kiingilio

Watu wataingia bure lakini uwanja umekodiwa Watu waeshalipiwa kila Kitu Wetu waingie bure ndiyomana Wenye Uwanja hawezi kuyahairisha au kuyahamisha.

Hebu jaribu kufuatilia matangazo yao utaona Masponsor kibao pale wametoa mamilioni kulipia uwanja na Matangazo ya Moja kwa moja ya Television hivyo wanaosimamia Uwanja hawawezi kuhairisha kwasababu ya mechi ya mpira hata siku moja wakati kuna hela Cash wameshazinyaka wakichanganya na za mechi ya Simba tayari wameshanasa double payment hapo.

Ndugu uwanja ni Biashara hule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…