Kusema Israel ni taifa teule ni kumtukana Mungu wa kweli

Kusema Israel ni taifa teule ni kumtukana Mungu wa kweli

Hii dhana inaitesa sana dunia, mpaka karne hii kuna wapumbavu wanamini Israel ni taifa Mungu!! 🤔 ni uongo mkubwa sana.

Mungu gani mbaguzi? Je, Mungu anapenda wanavyoua raia wasio na hatia? Mungu anawachukia wapalestina?

Kama sio wazungu Israel isingekuepo leo hii. Hata Misri tu inatosha kuipiga, ila kwa msaada wa Marekani Uingereza na nchi nyingine ndio mana wanaoea majirani zao. Huyo Mungu wa Israel labda atakuwa mzungu.

Dhana hii inatilia shaka kama kuna Mungu ndio maana watu wengi wanaona haiwezekani kuwe na Mungu anaegemea upande mmoja.

Kwa hakika Mungu hana ubaguzi.

Matendo 10:34

Kut 4:22​

Nawe umwambie Farao, BWANA asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu
 
Wote magaidi Si Israël si Hamas. Ndo maana mimi ninawalaani wote wawili.Wanaua watu wasio na Hatia. Ninalaani kitendo cha Hamas kufanya mauaji ya watu wasio na hatia,nilalaani Israël kwa kufanya mauaji kwa watu wasio na hatia.
Hujitambui wewe, uanze uchokozi wa kuua na kubaka wanawake wakikurudishia useme ni magaidi wote.
 
Soma hapa
20231018_191557.jpg
 
Kwa kukusaidia soma Kutoka 4:
22, Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu;

23, nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako.​
Maneno ya nani hayo
 
Soma hapo wewe;

SOMA: Namna BIBLIA ilivyotabiri kipigo cha GAZA na Majirani zake, na namna GAZA ilivyokuwa ikisurubiwa toka enzi za manabii


Nabii Amos alitabiri kuwa Gazi na nchi jirani watakuwa wanapokea kichapo tu... Na haijawahi kutokea Israel ikapigwa toka Amos alivyotabiri. Unazungumzia misri anatosha kumpiga Israel lakini unasahau Israel alipigana na waarabu wote ukanda huo, yani kina Misri, Syria, Uturuki, Lebanon, Palestina na wajinga wengine wengine wote wakapigwa vibaya sana, na Misri ikanyanganywa eneo la sinai, ila badae wakarudishiwa... Huu ni unabii wa Amos

AMOS 1:6-8 alitabiri juu ya kichapo
😂Yesu alitabiri atarudi kabla ya wafuasi wake kufa Kama tunamwona vile.
 
Ukimkataa tu YESU, vita ipo mlangoni...

Vita sio tu hiyo ya Israel na Hamas tu...

Vita yaweza kuwa ya uchumi, ndoa, kazi, wachawi, washirikina, shule kila mtu anavita yake...

Yani ukimkataa tu YESU unapigwa...
😂Na ukimkataa Muhammad Kuna moto wa milele...😂hizi dini tukiziacha tutakuwa mbali sana
 
Ndo huyo huyo anayekuja kuuhukumu Ulimwengu juu ya dhambi.

Usipomwamini jiandae kutupwa Jehanum.

Nakuombea umpokee, akuokoe uwe kiumbe kipya.

Amen
😂😂So tuamini dini yako Ina evidence gani...huyo Yesu tokea enzi za Paulo hajarudi tu...
 
Wewe endelea kubisha lakini huo ndio ukweli, kama Israel sio taifa teule mngekuwa mmeshalifuta kwenye ramani ya dunia muda mrefu sana,ila kwakuwa Mungu yupo na Israel hamuwezi kumfanya chochote kama umesahau nakukumbusha kidogo tu,rejea six days war,mliungana waarabu wote lakini mlipigwa na kataifa kachanga kabisa,utasema alisaidiwa na marekani mbona marekani mwenyewe kashindwa vita nyingi tu,na sio kila taifa linalosaidiwa na marekani linashinda kama unaakili timamu utaanza kujiuliza hii nchi inapataje ushindi, na kwanini mataifa yote duniani yanaitetemekea Israel na habari za Israel zinagusa dunia nzima, jibu Mungu yupo kazini na Israel vyovyote vile ya yanayoendelea ipo sababu ambayo yeye Mungu anajua kwanini ipo hivyo.
Nchi gani imeshawahi kufutwa kwenye ramani?
 
Kwa kukusaidia soma Kutoka 4:
22, Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu;

23, nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako.​
Kwa hiyo Mungu aliua mzaliwa wa kwanza ambaye hakuwa na kosa? Kwahiyo wauaji wanaendeleza alichofanya yeye?
 
Nani alikudanganya kuwa israel inalindwa na marekani? Nani alikudanganya Mungu wa Biblia anawachukia wapalestina? Kupitia Yesu Kristo Mungu wa Biblia anapenda watu wote kwa upendo wa kufa msalabani kuonyesha kwa jinsi gani anawapenda watu wote! Swali la kukuuliza! Hao wapalestina wanampenda Mungu wa kwenye Biblia? Waislamu wanampenda Mungu wa kwenye Biblia? Jibu hapana! Kwahiyo pambana na hali zenu! Mtapigwa tu! Hata hivyo wakati utafika ambapo dunia nzima pamoja na huyo mmarekani watamchukia Israel na kujipanga kumuangamiza! Vita hiyo inaitwa vita ya 'Amaegadon' ambapo Yesu mwenyewe ndo atashuka kuwatetea Israel! Mleta mada tambua kuwa hata Israel ya sasa hawamtabui Yesu Mesiah kuwa alishakuja! Bado wanasubiri wakati alikuja wakamuua kwa kumsurubisha msalabani! Hizi nyakati za mwisho okoka!
Mungu wa kwenye biblia ndio ameruhusu waisrael waue watoto?
 
Nchi gani imeshawahi kufutwa kwenye ramani?
Ungekuwa unafuatilia historia usingeniuliza hili swali tangu enzi za ayatollah hameniu wa iran walisema wataifuta Israel kwenye ramani ya dunia,labda waulize wao walimaanisha nini.
 
Mimi ni mkristo makini ninayesoma sana biblia lakini huwa hainiingii akilini ninaposoma stori za kwenye biblia. Kama Israel ni taifa teule mbona Mungu mwenyewe amekuwa akiwasotesha sana? Kwa mfano kulikuwa na sababu gani za kusafiri miaka 40 jangwani kutoka Misri hadi Caanan? Na ilikuwaje taifa teule liwe watumwa kwa wamisri? Kwenye biblia kuna stori za mtu anaitwa Hamani aliyetaka waisrael wote wauwawe, inakuwaje wateule wasiwe na ulinzi? Hata miaka ya Yesu bado Israel ilikuwa koloni la warumi. Hata kwenye hii miaka yetu kuna Hitler ambaye aliwaangamiza vibaya. Ninadhani huu uteule wao una walakini. Watafakari upya. Ni wateule wanaoishi kwa mashaka miaka yote tangu enzi za Musa.
 
Okoka na Mpokee Yesu Kristo aliye Mwisrael OG, Ili uwe Raia wa Mbinguni.

Yeye ndiye AMANI, mfalme wa HAKI, BWANA wa mabwana, Ufalme wake Hauna mwisho,

Ni wa Milele na milele.

Ukimkataa Yesu, vita IPO malangoni.

Amen
Hawa Israeli kwani si ndio waliomtandika Yesu mijeledi, Kalitaje hilo jina la Yesu huko Israeli uone kitakachokufika. Ndani ya Israeli wakristo wanaishi kama digidigi. Huku nyie kipovu kinawatoka kwa kuwaabudu.
 
Hawa Israeli kwani si ndio waliomtandika Yesu mijeledi, Kataje hilo jina la Yesu huko Israeli uone kitakachokufika. Ndani ya Israeli wakristo wanaishi kama digidigi. Huku nyie kipovu kinawatoka kwa kuwaabudu.
Lakini pamoja na ukorofi wao,

Haibadili UKWELI kuwa Israel ni firstborn wa Aliye juu.
 
😂😂So tuamini dini yako Ina evidence gani...huyo Yesu tokea enzi za Paulo hajarudi tu...
Kristo Yesu hakuja kuleta dini duniani.

Ukristo Si dini, ni maisha matakatifu yampendezayo Mungu.

Yesu amekaribia kurudi, ingia ndani ya safina usijeangamia.
 
Mungu anawachukia wapalestina?
Amosi 1:7-8
7 lakini nitapeleka moto juu ya ukuta wa Gaza, nao utayateketeza majumba yake.

8 Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.
 
Ndugu yangu akili iliosalama haukubali uongo na ujing huo. Hawa watu hawajawahi kuishi kwa amani toka dunia ilipoumbwa, kama kweli wateule wa Mungu mbona amekua akiwatesa maisha yote. Rudi ukasome tena bibilia utagundua hawa watu wamelaaniwa.
Nawe Rudi katika maandiko, ukasome utawala wa Mfalme Suleiman,

Hapakuwa na vita katika utawala wake.

Ilikuwa Amani tupu,

Alipomwacha Mungu na kugeukia miungu, mtoto wake akakumbana na LAANA ya vita kama ADHABU.

Mungu akipewa nafasi kuongoza Watawala Amani hutamalaki, la vita IPO malangoni.
 
Back
Top Bottom