Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

Kutoka Jangwani: Uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) - Agosti 29, 2015

TAARIFA MUHIMU;

Lowassa kuhutubia live usiku huu; Mgombea Urais wa CHADEMA ambaye pia anawakilisha UKAWA, Edward Lowassa atahutubia taifa usiku huu moja kwa moja kupitia Kituo cha Televisheni cha ITV mara baada ya taarifa ya habari. Hii itakuwa Kwa ajili ya Watanzania ambao kutokana muda kuwa mfupi hawakupata fursa ya kusikia hotuba yote aliyopanga kuitoa leo Kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni za kitaifa za CHADEMA na UKAWA.

Ni habari niliyodokezwa hivi punde...!
 
Nilikuwa nafuatilia neno hadi neno linalotoka kwa EL ili nisikie atafanya nini katika vita ya rushwa. Sikusikia neno 'rushwa' likitajwa kutoka mdomoni mwake, kama nimepotoka naomba nisahihishwe na kukumbushwa. Agenda kuu ya upinzani ilikuwa vita dhidi ya rushwa leo wamekuja na elimu bure, kufufua reli na ATC na kuwatoa gerezani Babu Seya na wengineo.

Wajinga ndio waliwao!

Nisahihishe kama nimekosea, lakini inaonesha ulikuwa pocho sana wewe wa hesabu shuleni. Na ndio maana unashindwa kuunganisha dots.

Priority ya ukawa ni katiba ya wananchi. Na ndani ya katiba ya wananchi ndimo rushwa inapigwa full stop. Mpaka rais hana kinga aendapo kinyume. Nini zaidi ya hapo tena
 
Haya ni mahaba, sio mapenz tena, Asanteni Dar es salaam, mikoa mingine tutawaunga mkono msiwe na mashaka. Kura tutapiga hata kwa mabomu na risasi msiwe na shaka, ASANTENI WANA DAR ES SALAAM, TUMEFARIJIKA NANYI,
URAIS UKAWA
UBUNGE UKAWA
UDIWANI UKAWA
 
Kingine tukumbuke campaign ndio zimefunguliwa Leo mpaka tarehe 24 October hivyo hakuna sababu ya kutaja yote yaliyopo kwenye ilani Leo...Leo ni kuzindua ilani na kutaja vipaumbele vichache mengine yatazungumzwa mikoani huko
 
Mi hata sijui.......hivi ni lini wanamshtaki......?......nilisikia kuna kesi inakuja........nataka nikasikilize labda nitapata kitu.........

Leo watakuwana maumivu ya viboko vichache walivyochapwa na Sumaye.Imagine unakatiwa umeme baada tu ya Sumaye kumaliza,hasira kweli kweli.
 
Mkuu hautakiwi kuwa hapa ni muda wa kwenda net rais kashatoa home work
 
Ila huyu Tambwe Hizza lazima awe kwenye probation period, huwa simuamini kabisa huyu!
 
Mgombea anaongea dk zisizozidi tano anaahidi kumtoa babu seya... Hivi babu Seya ni kipaumbele nchi hii?nchi hii Ina tatizo la ufisadi hasemi namna gani atadeal na ufisadi na anatwambia habari za babu Seya, who the hell is Babu seya???

Namkumbuka Dr Slaa Kwa kweli
babu seya aliyesema ni yeye au ni wananchi.. yani mnapenda kuegeuza maneno mnaumbuka...uongo utawaua hatuogopi libya ...kazi moja kuondoa ccm
 
Kwa huu upuuzi wa huyu jamaa hapa jangwani, naamua kurudi CCM. wala cjui kusoma na wala hiyo www.wwwww.wwwww cjui ni kitu gani. Alafu ahadi gani hizo za kuwaleta kina balali!?Kama ni elimu magufuli keshaahidi. Au kwa kuwa huku ni elimu *3!?
Hizi ndio hotuba wanazoshangilia malofa na wapumbavu na anajuwa akisema watalipuka kwa shangwe.
 
mimi ninawashangaa sana wanaccm. Mnatia haibu kabisa.

Mlitaka lowassa aongee nini?
wacheni wivu wakijinga, kama ninyi chaguo lenu ni magufuli, basi kuweni wa staarabu,

cctumesha hamua kumchagua lowassa, mtasema sana lakini mwisho wa siku nchi lazima ipate kiongozi bora na sio mtawala,

haibu-Aibu
cctumesha hamua-sisi tumeshaamua
 
Naona mnajitahidi kujitoa ufahamu. Lowasa ameshasema katika suala la Richmond mikono yake iko safi. Akaendelea kusema kuwa 'mamlaka ya juu' ndiyo yenye Richmond. Sasa mnataka aseme nini zaidi? Na amesema kama mtu ana ushahidi aende mahakamani, Mwakyembe aache kubwabwaja, apeleke ushahidi mahakamani kama yeye kweli ni mzalendo. Halafu mnataka Lowasa ajibu, mbona 'mamlaka ya juu' hajibu mapigo ya Lowasa. Ajaribu basi aone!!!!
 
mkuu tabia za watendaji. Sio waongeaji kama kasuku, hilo ulifahamu mkuu,

hata YESU alisema maneno yenu yasiwe mengi.

Watanzania kwa sasa hawahitaji ngonjera wanahitaji matendo.

Hebu onesha rekodi ya Utendaji wa Lowassa. Pia nyie msiofikiri mnapaswa kujua kuwa hotuba ni sehemu ya majukumu muhimu ya rais. Kuna mialiko nje ya nchi, kuhutubia jumuiya za kimataifa nk. Acheni kupeana faraja za vijiweni. Lowassa anakosa sifa muhimu kabisa ya uongozi. Kama ni Utendaji tu, akawe mkurugenzi, au meneja kama alivyomwita Sumaye leo.
 
Watu tunalia kila siku wahalifu wafungwe jela....lakini sera ya chadema ni kufungulia wahalifu na wabakaji!! maajabu haya sijui yataisha lini

Nendeni mkamjibu SUmaye maswali yake,ya Twiga kupanda ndege,Madawa ya kulevya,Escrow account,duh sijasahau zile pesa za EPA na kusamehewa kwa watuhumiwa.

Ohh nimesahahu yale MABEHEWA ya kichina na MELI ya mwaka 1978....
 
Bibi yangu kijijini anaomba nimtumie Website aangalie ilani ya CDM ila hajui kusoma wala kuandika. Nipeni ushauri.

Queen Esther

Hebu tujikumbushe yalio tokea leo Jangwani na yaliyo semwa na Loassa mgombea wa Ukawa aka Chadema.

1: Lowassa amesema atamtoa Babu Seya akiwa Rais. Je huko sio kuingilia utawala wa sheria? Je ana uhakika gani alisingiziwa? Hivi ndio vipaumbele vya serikali kwenye nchi yenye matatizo kiasi hichi? Tokea lini Lowassa amekua hakimu? Je, na wafungwa wengine atawaachia huru?
2: Lowasa kasema atatuletea/kumfufua Balali, sasa najiuliza si watuambie leo hii yuko mji gani ama nchi gani na kwanini asubiri awe raisi ndio watuletee Balali? Hichi nacho ni kiapumbele? Au hii ndio ilani ya UKAWA?
3: Lowasa kasema eti, elimu itakuwa bure! Kuanzia primary-University lakini ameshindwa vibaya sana kusema fedha zitatoka wapi? Hivi, wakati wa Nyerere nani alilipia elimu?
4. UKAWA wamekiri wao ni ma lofa kutokana na t-shirt walizotengeneza na kuuza uwanjani lakini hapo hapo wameambiwa wakasome hotuba ya mgombea Urais mtandaoni je kama ni kweli ni ma lofa wana access ya internet? Kulikuwa kuna aja gani ya mkutano kama mngeweka vitu vyote online? Vipi kuhusu wazee wa Mashambani, nao waingine dot com kusoma ilani?
5. Ukawa wametuhakikishia kuwa hawana sera wala ilani zaidi ya kufukuza upepo.
6. Ukawa wamebakia kumjibu Mtaafu Rais Mkapa ambaye aliwateka Kisaikologia na kuwa gumza la Ukwa leo Jangwani.


11951204_1068783333154019_992321555451370143_n.jpg


 
Back
Top Bottom