Binafsi ninaamini Mungu yupo [Ingawa siwezi thibitisha], ila sina hakika kama Mungu huwa anatoa laana kwa matukio makubwa kama haya ya Uonevu wa serikali na majeshi au yeye hutoa laana kwetu sisi katika individual level kwa vimakosa vyetu kama kuibiana, kudhulumiana n.k (yaani god of small things). Kwanini nasema hivi.
Ukitazama historia ya mwanadamu, toka dunia ya kale, mwanadamu amekuwa na hulka ya kumvamia mwenzake, kwa vigezo vya udhaifu, na kisha kumtawala. Hii si kati ya mzungu na mwafrika tu, bali hata jamii zingine. Mfano, huku kwetu africa dola kama Baganda ilikuwa kubwa kutokana na kuzivamia dola zingine ndogo ndogo kisha kuwa maeneo yake na kutanuka kwa ufalme (unyanganyaji ardhi), kina Milambo, Mkwawa, n.k wote wamefanya hivi. Warumi walitawala wazungu, waarabu wa Ottoman waliwatawala wazungu pia kwa miaka mingi, waarabu waliwachukua watumwa waafrika na kujenga miji yao huko, miaka ya 1500 wareno, waholanzi wote waliitawala dunia, kimabavu. Uingereza miaka ya 1800 to 1940s.
Leo Mmarekani amepindua/kujaribu kupindua serikali Zaidi ya 30 toka 1940. Mamilioni ya watu wameua kwenye mission hizo. Ugaidi ambao unatengenezwa na mataifa makubwa umeua takribani watu 2,000 duniani. Watawala madikteta kama kina mobutu, Noriega wamewekwa na Marekani wakiua watu wake, wakiuza unga huku yeye US akivuna rasilimali na kuzidi kuwa taifa tajiri zaidi. Libya wamemuua Ghadafi na maelfu ya raia wamekufa kutokana na ukosefu mapinduzi hayo, kisa tu Ghadafi alitaka kuanzisha sarafu itayotumiwa na Arab Countries kuuza mafuta. Hao Israel, wamewekwa pale Kibabe, na hadi leo wanazidi kuchukua maeneo ya wapalestine na kuua raia wasio na hatia. Karibu miaka 70 sasa, Mungu haoni tu? Dua ngapi zimeombwa na wapalestine, vilio vingapi vimetoka kwa kina mama na watoto wadogo wasio na hatia(ambao imani zinasema hakuna dua na laana mbaya kama ya mtoto!?).
Kwa hulka ya mwanadamu, kumtawala mwenzake akipata upenyo, ndio maana tulijiwekea sheria. Sheria hizi ndio zinaweza mdhibiti mwanadamu. So, hizi dua na laana sidhani kama zina majibu yoyote katika mambo haya ya kiserikali. Suluhu ya wapalestine ni wenzao wa M.E kuungana nao, kitu ambacho sikioni kikitokea. Jambo ambalo nina uhakika nalo ni kuwa, Palestine inaenda kupotea.