Habari!
Hii ni mahususi kwa wale wanaohitaji kufanya biashara, sio wanaofanya biashara.
Njia panda,mahala salama pa kutafakari upande upi uelekee ama uufate. Nimechagua leo kushare nanyi ndugu zangu kwa kile kidogo, na kesho siku yakuanza mfungo ianze vema.
Haihitaji shule kufanya hili, inahitaji dhamira, kuamka na kufanya. Waweza kuwa na mapesa mengi ama kidogo sana..
(1) Tafuta laki 3 TU ama ukiwa na pesa zaidi sio mbaya, ni nzuri zaidi.
(2) Tafuta simu ya android, hata window phones poa
(3) Tenga muda wa kutembelea mitandao hii:
a.AliExpress.com - Online Shopping for Electronics, Fashion, Home & Garden, Toys & Sports, Automobiles from China.
b.Manufacturers, Suppliers, Exporters & Importers from the world's largest online B2B marketplace-Alibaba.com
c.ebay.com
NB: Hapa masoko ya kwenye mitandao ni miiingi sana lakini for beginners anzia hapa, 1 step at a time, pia apa hakikisha unaspend almost siku 14 kuipitia hii mitandao kwa kina, usijipe moyo kwa siku moja tu kwamba aah niisha umaliza kuupitia, mind u; The more u get involved to them the more new things about them you will learn.
(4)Tenga muda wa kushare urafiki na watu wako wa karibu ata kama ulikuwa huna tabia io,sasa unahitaji watu katika biashara yako,maana wao ndio wateja wa kile utakacho anza uza,pokea watu wote... Hudhuria vikao vya harusi ata kama huna mchango wa kuchangia,uwepo wapo ni muhimu zaidi kuliko ile pesa,nenda kuswali kwa jumuia sio ndani kwako pekee,kama msikitini,kanisani n.k
(5)Jiunge na magroup kupitia hiyo android phone yako either katika WhatsApp, viber, instagram n.k laweza kuwa group la ulio soma nao,group la kazini kwenu,group la washkaji wanywa pombe,group lolote ata wewe waeza kubuni waunge tu ata watu 7 kwa siku
(6)Jiunge na facebook na magroup yalioko umo,yatakusaidia...
Itaendelea...