Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Pole sana kwa kupigwa Mkuu.

Laini za Vodacom zinatolewa bure.

Cha msingi uwe na TIN NUMBER & BUSINESS LICENCE.
 
Nenda kariakoo chukua viatu Sandoz, ila sijajua unalenga soko lipi na mazingira uliyokusudia kufanya biashara. Ni jambo njema ukaeleza uko wapi na biashara unaenda kufanya wapi.
 
Ni kweli kabisa line zinatolewa bure ila kwa utaratibu. Uwe na leseni na tin namba pia na mtaji usiopungua mil 1 baada ya hapo ujiandae kusubiri kwa muda usiojulikana ili kupata hizo line,mtandao wa Voda kwa sasa wamesitisha kuzalisha line za Wakala mpaka watakapo tangaza tena.Ukihitaji kwa haraka unazipata kama nilivoeleza hapo juu,ni hiyari yako kuchagua
 
Nashukuru kwa MAWAZO yako mkuu...
Yameniongezea kitu..!
 
Ahsante kwa taarifa hii muhimu mkuu..!
Naamini itawanufaisha na wengine pia..!
 
Mkuu...
Hiyo biashara tunaweza fanya muda wangu wa ZIADA..?
Maana me ni mwanafunzi..!
 
Samahani naomba uliza ni leseni ya biashara yoyote, na ni kwa mitandao yote ama?
 
Kachukue tin number tra ni bureeeeeeeeee.... Kachukue lesen ya biadhara halmashaur za miji au manispaa, huwa kuna tathmin ya utoaji Wa lesen ya biashara,. Nakuomba ukifika ofisin hapo sema unataka lesen ya biashara ya KUUZA VOCHA NA LAINI ZA SIMU..... Gharama yake ni kati ya elfu 30-50


Bravo
 
Salamu kwenu wana jamii...
Kama heading inavyojieleza...
Ni biashara gani nayoweza kufanya kwa mtaji wa shilingi laki tano za kitanzania..?
Nahitaji mawazo yenu KAKA na DADA zangu wa jamii forums katika jambo hili..!​
Nguo za mtumba na viatu
 
Nguo za mtumba na viatu
Kaka Mshana, hawa jamaa wanaotuuziaga wengi huwa wanasema wanafuata Mombasa ndo kuna mitumba grade ya juu. Kuna ukweli hapo?

Kama sivyo mzigo unapatikana wapi kwa hapa Dar?
 
Mfano wa forever living.
 
Kaka Mshana, hawa jamaa wanaotuuziaga wengi huwa wanasema wanafuata Mombasa ndo kuna mitumba grade ya juu. Kuna ukweli hapo?

Kama sivyo mzigo unapatikana wapi kwa hapa Dar?
Saa nyingine ni kuaminishana tu hata hapa ipo shida ni kwamba wauzaji wetu hapa ni wachakachuaji
 
Mkuu George Betram Kuna wazo pale juu kakupa kaka mshana jr naomba ulifanyie kazi.

Sijajua upo mji gani na chuo gani, lkn nakushauri jiingize ktk biashara ya mitumba.

Anza na bidhaa za mitumba za wadada. Usinunue BARO, nenda kwa ile style ya KUPOINT zile unazoona zina ubora. Kwa upande wa nguo, kama ungekuwa DSM, ni kujihimu pale Karume alfajir ya kila Jumamosi, KUPOINT. Kwa hiyo laki5, inatosha kuchota laki 3 na kuanza biashara huku ukipima upepo ulivo.

Ukirudi chuo unaziongezea ubora kwa kuzipiga pasi. Uuzaji wako unakuwa ni wa kuwafuata wateja wako hostel kwao, chumba kwa chumba!

Ndani ya biashara hii utaanza kupata oda za wateja wako nini wanataka ukawaletee kutoka sokoni. Wadada wengi hawana muda wa KUZURURA ktk masoko ya mitumba.

Nimekushauri ujihusishe na bidhaa za wadada kwa vile ktk maisha ya Chuo, wadada wanaongoza KUSHINDANA KUVAA kuliko men. Pia wadada kama utakuwa makini hamtasumbuana sana ktk malipo.

Wanaume baadhi wawapo chuo huweka pembeni hobby ya mavazi na wengi huigiza HIP HOP ama UGUMU lkn nyuma ya pazia wanamaanisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…