Kwako Rais Samia, sisi Askari tunaomba utuongezee maslahi

Kwako Rais Samia, sisi Askari tunaomba utuongezee maslahi

Polisi hamjawahi kuwa WATII kwa Katiba na Sheria. Mmeua sana raia, mmebambika sana kesi wasio na hatia, mmetimbatimba demokrasia na haki za binadamu, mmeshiriki sana kuiba kura...

Sioni umuhimu wa nyie kupewa kipaumbele kwa sababu mnashiriki uhalifu wa kisiasa dhidi ya nchi
 
Nadhani magereza wako ICU kabisa,ukikutana nao na uniforms zao na wao utadhani wafungwa kabisa,wako Hoi bora traffic na hawa wengine wanapata vijisent, angalau ni nadhifu kidogo
 
Rais Samia pokea andiko hili linaloletwa kwako nasi askari wako wa Wizara ya Mambo ya ndani kutoka Magereza, Polisi nk .

Rais tunayo madai yetu ya muda mrefu ambayo kisheria tunastahili kulipwa.

1. Posho za maji na umeme zilipwe moja kwa moja kwenye mishahara yetu moja kwa moja tofauti na sasa ambapo posho hizo zinaliwa na wajanja wachache wizarani na ndani ya majeshi yetu, ifanyike kama inavyonyika JWTZ

2. Posho ya chakula ipandishwe kutoka 10,000 per day Hadi 15,000 per day kwa sababu gharama za maisha zimepanda hasa vyakula kutokana na wakulima kupandisha bei baada ya serikali yako tukufu kuwaruhusu nje ya nchi ili nao wafaidi matunda ya jasho lao, tunaomba posho hiyo iwe 450,000 kwa mwezi.

3. Posho ya pango (ngome) alipwe kila Askari kama ilivyo JWTZ ili Askari warekebishe nyumba chakavu wanazoishi kambini.

Rais madai yetu ni ya muda mrefu sana lakini yamekuwa yanadhibitiwa na viongozi wetu ndani ya majeshi yetu au wizarani kwa manufaa yao wenyewe.

Aidha tunakuomba utuondoe utumishi na utupeleke mfuko maalumu (consolidated fund) maana sheria zetu haziendani na utumishi.

Rais tunajua unayo mambo mengi ya kufanya lakini tunaomba uyaangalie mambo hayo kwa huruma na upendo ili kuboresha maslahi ya Askari wako. Kama unavyoelewa askari hana chama cha kumtetea bali chama chake ni wewe Rais hivyo ndivyo tunavyofundishwaga mafunzoni.

Tunakutakia afya njema mama, bajeti hii tunaomba utufikirie kwa mambo hayo kadhaa tuliyoyaainisha hapo juu.

Tunakusalimu kwa jina la jamhuri tukufu ya muungano wa Tanzania.
Askari yupo tayar kufanya kazi kwenye mazingira magumu...wewe ni askari maslah... askari Lia Lia.....
At least wew una posho ya 10,000 chakula per day...

Tanzania ni nchi maskini wew UNATAKA maslahi Gani? Acha kazi kafanye Biashara....

Maana mwenye nchi hii PHD holder anaweza akawa amiliki hata bajaji...... standard seven ana ghorofa na good life kuliko profesa wa chuo kikuu ....

R.I.P PROF Y.BWATWA
Wewe ulitufundisha vyema

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
Wasalaam
Kwa Sasa
+267
 
Rejea yanini kwani Hao aliowataja wako wanafanya majukumu yanayofanana???kanuni na taratibu zao zinafanana???

Wao ushawahi Kuja kuona wanaandika kama alivyoandika huyu wa wizara ya mambo ya ndani bado huoni tofauti baina yao???

Kama Fulani kama Fulani hakuna kitu kama Fulani jeshini Raia ndiye anaweza kusema nipe kama fulani sio kauli ya mwanajeshi hii
Hujui ukisemacho binti mrembo,,,mipaka yetu tunaijua wewe unataka wao walalamike wakati wanaona wanachopewa kinakidhi angalau,,,tulia binti wenye akili wajadili na wenye mamlaka wafanyie kazi,,hakuna nidhamu mbele ya njaa
 
PORISI HAMFAI KBSA MLINILIA 70k KISA KUTRAKI SIMU

NA MLISHIRIKI KWENYE UCHAFUZI 2020

HAMSTAHILI
 
Kwahiyo mnataka itoke Posho ya laki 300,000 Kwa mwezi iende 450,000 Kwa mwezi!?? Halafu ulipiwe maji na umeme!??aiseee!!! Hatari!! Hivi Ina maana huwezi kujilipia umeme Kwa mwezi shiling 20000!? Aisee !! Hatari!!
Hujui mambo ya dola mzee tulia,,,posibility ya kufa kazini ukaacha familia ni 75% ndo unataka ulinganishe hicho kimshahara na viposho na risk tunayoikabili kila siku!?
 
Sawa lakini na nyie kuweni na utu kupiga watu Hadi wanashindwa kutembea ni Jambo Ambalo halifai Kabisa
 
Anaweza kujilipa ila kimsingi pesa hiyo ataichukua kwako raia,halafu utakuja ulie lie hapa polisi wana njaa mpaka buku 2 wanabeba.
Ndio maana wakitoka kazini baada kustaafu hufa mapema kupenda bure ni kwingi mno
 
Kila siku ombi langu kwa Mungu ni kuona vyombo vya dola vinasimamia haki, uonevu kwa raia umekuwa mkubwa sana.

Ninaamini sitahiki zenu mtakumbukwa hata kama sio leo au kesho, pia yale mnayopenda mtendewe basi na nyie watendeeni vivyo hivyo nanyi mtaishi vema na amani ya moyo itatawala ndani yenu.
 
Mlishindwa nini kumuomba MAGUFULI? Afu wewe askari gani fala wewe? MBONA MAMA SAMIA KAPANDISHA POSHO?
 
Kahh kumbe mshahara wenu mdogo hivi..ndo mana mna stress sana
 
Rais Samia pokea andiko hili linaloletwa kwako nasi askari wako wa Wizara ya Mambo ya ndani kutoka Magereza, Polisi nk .

Rais tunayo madai yetu ya muda mrefu ambayo kisheria tunastahili kulipwa.

1. Posho za maji na umeme zilipwe moja kwa moja kwenye mishahara yetu moja kwa moja tofauti na sasa ambapo posho hizo zinaliwa na wajanja wachache wizarani na ndani ya majeshi yetu, ifanyike kama inavyonyika JWTZ

2. Posho ya chakula ipandishwe kutoka 10,000 per day Hadi 15,000 per day kwa sababu gharama za maisha zimepanda hasa vyakula kutokana na wakulima kupandisha bei baada ya serikali yako tukufu kuwaruhusu nje ya nchi ili nao wafaidi matunda ya jasho lao, tunaomba posho hiyo iwe 450,000 kwa mwezi.

3. Posho ya pango (ngome) alipwe kila Askari kama ilivyo JWTZ ili Askari warekebishe nyumba chakavu wanazoishi kambini.

Rais madai yetu ni ya muda mrefu sana lakini yamekuwa yanadhibitiwa na viongozi wetu ndani ya majeshi yetu au wizarani kwa manufaa yao wenyewe.

Aidha tunakuomba utuondoe utumishi na utupeleke mfuko maalumu (consolidated fund) maana sheria zetu haziendani na utumishi.

Rais tunajua unayo mambo mengi ya kufanya lakini tunaomba uyaangalie mambo hayo kwa huruma na upendo ili kuboresha maslahi ya Askari wako. Kama unavyoelewa askari hana chama cha kumtetea bali chama chake ni wewe Rais hivyo ndivyo tunavyofundishwaga mafunzoni.

Tunakutakia afya njema mama, bajeti hii tunaomba utufikirie kwa mambo hayo kadhaa tuliyoyaainisha hapo juu.

Tunakusalimu kwa jina la jamhuri tukufu ya muungano wa Tanzania.
kama huna ndugu hupati kazi vyombo hvi vya ulinzi, laana hiyo iendelee kuwatafuna. yaani 10k per day kwa ajili ya msosi unaiona haitoshi??

na cc jobless tusemeje tunaolipwa elfutatu kwa wahindi??
 
Kwanza Ombi lenyewe limechelewa, maana Bajeti imeshachelewa. Lakini inaonesha ni jinsi gani woga ulivyojaa kwenye jamii yetu ya Kitanzania. Anapokuja IGP ni kwa nini huwa hamumwambia hayo mambo??
Thubutuuu ..

Kuna ntu inasemekana kapiga 4Billions ya kufa na kuzikana.

Nadhani hii kufa na kuzikana ni katika ule ukoo wa CWT ya walimu.

Polisi ikataeni KUFA NA KUZIKANA ili tujue kufa kuwa kweli mmeanza kudai haki.
 
Back
Top Bottom