Kwanini baadhi ya "wanajeshi" wetu wana vitambi?

Wanajeshi wa nchi zingine: Rwanda, China, Korea, n.k. hawajaridhika?
 
Kumbee ,nimejifunza kitu🤔
 
Mambo mengine ni nature hayazuiliki. Kuna watu hawapati vitambi hata wangekula vyakula vya dunia nzima. Na kuna wengine wanakula kawaida tu ila kitambi kinamjia.
 
Mike..
 
Wanajeshi wa nchi zingine: Rwanda, China, Korea, n.k. hawajaridhika?
Kwani, wanajeshi wote unawaona wamefuga vitambi mkuu?

Na hao wa nchi ulizozitaja, unaonana nao kwa karibu kila siku kama unavyokutana na wa kwetu ili kuweza kuwatathimini?

'Body index' katika jeshi huzingatiwa, wakiamini kabisa Urefu x Uzito usiorandana ni tatizo la ki afya na vikipishana lazima mtu hushauriwa akavipunguze.

Halafu lazima uelewe kuwa maumbile ya miili ya watu katika jamii mbali mbali hupishana kwa kimo na kwa ukubwa.

Sasa jamii ya kichina waweza linganisha na wabantu?

Katika uchambuzi wako kwa ulinganifu, wamarekani ama Canadians kwanini haukuwaweka ili kuboresha mjadala?
 
Mkuu hautaki na sisi tuwe tuvitambi twa kufutia simu..?ahahahha
 
Mkuu, inaelekea wewe ni msoja! Kwani nawe una kitambi?

Siyo wanajeshi wote wa Tanzania wana kitambi mkuu. Lakini hao wachache wenye navyo "wanalishuhshia" hadhi Jeshi.

Sisi raia tunaamini kuwa askari asiye na kitambi yupo fiti zaidi kimedani kuliko anayeonekana kama kazi yake ni kufuga tumbo.

Unamkuta mwingine tumbo ni kubwa mpaka linaninginia.
 
Fuatilia maisha yako wewe,furahia sana tunu hii ya amani tuliyo nayo japo gharama zake huzijui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…