Tatizo la kubwa la bukoba ni unafiki uliokithiri ndo chanzo cha kubak nyuma, pili muingiliano wawatu tofaut tofaut hakuna wamebaki kuwa na kabila moja2 vitega uchumi hakuna
Mkuu Mwombeki, mi nafikiri ingekuwa vema kama tunge base hoja zetu kwenye facts na figures - hapa tumepewa takwimu kwamba once upon a time i.e baada ya uhuru Mkoa wa Kagera ulikwa wa pili kiuchumi Tanzania nzima ukifuatiwa na Kilimanjaro, kumbuka enzi hizo muingiliano wa watu ulikuwa negligible, swali ni je, Mkoa ulifanikiwa vipi kuwa mbali kiuchumi na kimaendeleo? Najua kuna baadhi ya members watakuja hapa na hoja kwamba zao la kahawa ndilo lilichangia sana - hiyo si kweli mbona Mbinga na Musoma wanalima kahawa?
Tukirudi kwenye hoja ya Mkoa kujiletea maendeleo ya kiuchumi mbona tuna mifano ya kudhilisha hilo - chukulia chama cha wakulima cha BNCU/BCU/KCU kilicho anzishwa in 1920s au 1930s kama sikosei, chama hicho kilikuwa kina vitega uchumi chungu mzima kwa niaba ya wakulima, vile vile na Kalidinald Rugambwa enzi hizo alianzisha/fungua Credit Union, Wahaya walijenga Ukumbi mkubwa wa kisasa wa mikutano ya Buhaya Council pale Rwamishenye - hapo ndipo walikuwa wanajadili mbinu za kujiletea maendeleo na walifanikiwa sana katika nyanja za kuimarisha kilimo cha mazao yote specifically kahawa, kujenga mashule na vyuo vya carpentry na kilimo, kugharimia elimu ya shule za msingi mpaka vyuo vikuu vya nje kwa wazazi ambao hawakuwa na uwezo wa kugharimia karo - hapo nazungumzia kabla karo haizijafutwa - the list is endless.
Sasa mkuu Mwombeki hivi inaingia akilini kwamba wenyeji wa Mkoa wa Kagera ambao walikuwa so organised kujiletea maendeleo wanaweza kufanya a U turn in less than a decade tangu tupate uhuru wakajikuta wanarudi nyuma kwa kasi ya kutisha i.e uchumi/maendeleo ya Mkoa yana decay at exponential speed - the question is: Is it true kwamba wachawi wa Mkoa wetu ni sisi wenyewe - personally I don't think so.
Siyo siri kuna forces from without zilizo geuza Mkoa wa Kagera inside out and upside down sio bahati mbaya au sijui unafiki uliyokithili hiyo si kweli - mimi na amini it/is was a political decision ambayo ilikuwa inakuwa implemented quietly kudumaza Mkoa - I might be wrong lakini ukweli ndio huo, jaribu ku revisit majibu ya baadhi ya members ambao wanajulikana hulka zao kuhusu wazaliwa wa Mkoa wa Kagera what does that tell you kuwahusu? Je, unafikiri check watu kama hao wangepewa wadhifa wa kushugulikia Mkoa wa Kagera unafikiri wangejali au kuupa kipaumbele - thubutu, wangetoa visingizio tu ili Mkoa uendelee ku marktime, usidanganyije mkuu -ve atittude 2wards Wahaya hipo so deeply seated kwa baadhi ya members wapo radhi kusingizia au kusema lolote just 2 get even - sio utani they mean it, soma wanayo andika humu wana derail mada nzima na kutumbukiza vitu vya kushangaza ambavyo havina uhusiano wowote na mada.
Jamaa mmoja amesema mleta mada angezungumzia Mkoa mwingine basi members karibu wote wangechangia calmly, lakini kwa kuwa mada yenyewe inahusu Mkoa wa Kagera basi ajitayalishe kubamizwa kwa maneno ya kashfa na kejeri - na kweli ndicho kinacho endelea hapa - elimu zao za Vyuo kikuu kwa baadhi ya wachagiaji mada notwithstanding, wanakuwa overly consumed na blind hatred.
Mkuu Mwombeki, kioo cha kuonyesha mandeleo ya Mkoa ni Makao Makuu ya Mkoa, je mji wa Bukoba hupo hali gani miaka nenda rudi si unaonekana kama a ramshackle - uwezi kuamini kama Mkuu wa Mkoa na Wilaya wapo pale, ilikuwaje manispaa inafikia hatua ya kukwangua lami mji mzima barabara zote zinabaki vumbi tupu, nyumba zilizo taifishwa na Serikali azipakwi rangi, standi ya mabasi ndio kabisaa, soko limebaki hivyo hivyo tangu enzi ya ukoloni wa Kijerumani sehemu hizo zote ni wajibu wa Serikali kuzishugurikia kama wanavyo shugurikia Mikoa mingine, Makonda kapewa hela ngapi kusisambaza kwenye manispaa za jiji la Dar kwa ajili ya maendeleo mbona hawasemi eh wait a minute jiji la Dar wenyeji wake ni Wazaramo, Wakwere, Warufiji na Wagenderoko - wote hao wajitegemee Kuendeleza Mkoa wao bila ya kutegenea Serikali.
Back 2 the main point kuhusu mji na Bukoba na Mkoa wa Kagera Narudia kusema kwa nia njema tu, kwamba kidogo inashangaza kuona Mkuu wa Mkoa na wa Wilaya wanapita kwenye barabara za Mji wa Bukoba zilizo kwanguliwa lami na kubaki vumbi, mjini hauna taa barabarani usiku ni giza tupu lakini wakuu hao awachukui hatua za kuwajibisha watu walio chini yao wakati wakijua fika kwamba Mikoa yote nchini Serikali Kuu utoa fedha za kushugulikia/endesha/gharimia maendeleo ya miji na manispaa zake - yaani hali ya mji wa Bukoba ilivyo hauna hata hadhi ya kuitwa manispaa ni majanga matupu!!
Binafsi nakumbuka nikiwa shule ya msingi barabara zote za mjini Bukoba zilikuwa na lami na taa, maji na umeme wa kuaminika, matrekta ya town council yalikuwa yanapita kila siku kusomba uchafu - mjini nzima ulikuwa msafi masaa yote, yote hayo yamebaki kuwa historia.