Kwanini Rais Samia mpaka sasa hajaongea na waandishi wa habari kuhusiana na sakata la Bandari?

Kwanini Rais Samia mpaka sasa hajaongea na waandishi wa habari kuhusiana na sakata la Bandari?

Ni zaidi ya mwezi sasa hili suala la bandari limeendelea kuwa gumzo, kinyume na matarajio yangu!

Mwanzoni nilidhani lilikuwa ni upepo tu upitao kama yalivyo masuala mengine.

La hasha. Haijawa hivyo.

Kila kunapokucha, gumzo la bandari zetu ndo linatawala vinywa vya wananchi.

Hali hii imenifanya nijiulize maswali kadha wa kadha;

Kwa vile ni gumzo ambalo limeendelea kutawala mazungumzo ya watu kwa muda mrefu [kwa zama hizi za utandawazi, umma kuongelea jambo moja kwa zaidi ya mwezi, ni muda mrefu!], basi ni wazi kuwa wananchi wengi wanaliona kuwa ni suala la muhimu sana.

Sasa kwa nini mpaka sasa Rais Samia hajaitisha mkutano wa habari na waandishi wa habari ili kulizungumzia na kulitolea ufafanuzi na kujibu maswali ya wananchi?

Badala yake, ni kama vile kajificha nyuma ya makada wa chama chake pamoja na baadhi ya wateule wake serikalini ambao wao ndo wamejaribu kulizungumzia, lakini kila wafanyapo hivyo, wanaishia kuzua maswali mengi zaidi.

Ni kwamba hana taarifa za kutosha za kumwezesha kulizungumzia hilo suala mbele ya waandishi wa habari?

Au hajiamini kuongea na waandishi wa habari?

Come on Samia….talk to the press [and the nation].

If everything is above board….is on the up and up, it shouldn’t be that difficult for you to talk to the press and take their questions.

Ona huyu alivyokuwa anakabiliana na waandishi wa habari wa kimataifa…

Waandishi wenyewe ni hawa kina Deodatus Balile au unaongelea waandishi wa BBC na CNN?
 
Huyu faiza ni nani nchi hii anajihusisha na shughuli gani kwanini anapambana sana wakati huu hasa sakata hili la bandari si usiku si mchana yupo active tofauti kabisa na kipindi cha magufuli
Huyo hana maslahi yoyote zaidi ya dini tu.

Anaamini Waarabu ni ndugu zake katika imaani na Samia ni muislamu.

Huyo Faiza haamini hasilani kama kuna Waarabu Wakristo, yeye kwake Uarabu siyo race ni uislamu.

Katika wajinga wa JF ukiweka shindano la Top ten lazima ashike namba one.
 
Haihusu.

Wapo wenye kazi zao juzi waliitisha kongamano wakajibu maswali yote, na wamekubaliana kikao kijacho itakuwa ni mdahalo na wale wamaopinga.

Mama ana mengi sana ya kufanya, hana sababu za kubishana na wajinga.
Nchi ina watu milioni sitini. Ni kujidanganya kusema wenye kazi zao washaamua kwenye kitu ambacho kinataka unyenyekevu na hekima ili kukipeleka mbele.
Muda unabadilika. Mwenye macho haambiwi ona. Na mdharau mwiba..... Baadae tusije kusingizia dini au sijui nani anafanya nini...maana tunawajua wazee wa kuhamisha magoli.
Kipindi hiki watanzania wamesema na wamesikika
 
Wakina wakili Mwabukusi na wenzie pamoja na watanzania wengine wanao Pinga sio kwamba hawataki uwekezaji, lakini wanataka ufafanuzi na kuwekwa sawa katika vile vipengele wanavyo vipigia kelele,

lakini serikali badala ya kujibu hoja zao inakuja kuwaambia kwamba wao ni wapotoshaji, na wengine wakasema wana hongwa lakini hawasemi wana hongwa na nani, hapo ndipo ukakasi unapo zidi, kama wao ni wapotoshaji ukweli ni upi mbona hawa usemi kwa kunukuu mkataba wao?

Swali lingine limeibuka na halija patiwa majibu, kama huu mkataba una neema kiasi wanacho sema kwa nini bandari za Zanzibar hazimo kwenye huo mkataba

Serikali itoe majibu kwa wananchi, watoe majibu ambayo yataondoa ukakasi wote uliopo kwa sababu wale wanao waita wapotoshaji ndio walio wafahamisha watanzania wengi uwepo wa huo mkataba na watu Waka waamini sasa wanavyo jichanganya kwenye majibu yao inafanya watu waamini kuna shida kwenye huo mkataba
 
Muhimu ni kwamba wataalam kama kina shivji washaongea sasa we shivji unaona hana akili?mtu ka publish mavitu yanasomwa chuo kikuu Leo hii aongee kitu kuhusu tasnia yake me nimpinge..sorry kwanza kwani rais mama samia kasomeaga nini??
Record keeping
 
Na yeye na usomi wake alitahadharisha ubinafsishaji wa mabenki hatari kwa nchi asimame mbele leo atuonyeshe hizo athari kwenye hili la masuala ya uchumi na mageuzi huwezi sikiliza mtu kama Shivji alishaharibu toka mwanzo huko ukishachanganya imani zako za mambo ya ujamaa na taaluma utatoa tahadhari zisizokuwa na maaana , akajifunze kwa wenzake kama dean wa school ya Lee Kuan Yew watu wametoa michango ya kufanya nchi zao zimekuwa mataifa tajiri ulimwenguni .
 
Haihusu.

Wapo wenye kazi zao juzi waliitisha kongamano wakajibu maswali yote, na wamekubaliana kikao kijacho itakuwa ni mdahalo na wale wamaopinga.

Mama ana mengi sana ya kufanya, hana sababu za kubishana na wajinga.
Kwi Kwi Kwi ! Hali mbaya ! Maji yamekorogeka
 
Ww ni kikarogosi ww uliona kuna mtu alijibu kitu pale zaidi ya bla blaa za hapa Na pale
 
Kuongea ongea sana wakati wa kula itapelekea upaliwe na kushondwa kuendelea kula
 
Haihusu.

Wapo wenye kazi zao juzi waliitisha kongamano wakajibu maswali yote, na wamekubaliana kikao kijacho itakuwa ni mdahalo na wale wamaopinga.

Mama ana mengi sana ya kufanya, hana sababu za kubishana na wajinga.
Mie nilidhania una akili!
 
Huna hoja ndo maana umemshambulia nafsi yake!
Tu
Kwi Kwi Kwi ! Hali mbaya ! Maji yamekorogeka
Waarabu wa DP World wana moto na Royal Tour saa hizi. Unafikiri hizo porojo zenu watu wana habari nazo? Jionee👇🏾
Ww ni kikarogosi ww uliona kuna mtu alijibu kitu pale zaidi ya bla blaa za hapa Na pale
Nyie hororojeni na kubwabwaja, mama Samia anajibu kwa vitendo:

Haihusu.

Wapo wenye kazi zao juzi waliitisha kongamano wakajibu maswali yote, na wamekubaliana kikao kijacho itakuwa ni mdahalo na wale wamaopinga.

Mama ana mengi sana ya kufanya, hana sababu za kubishana na wajinga.
kwani wale wakina Johari ndiyo wamepewa madaraka ya Kusimamia rasilimali za taifa kwa mujibu wa katiba,mpaka wawe final say?
 
Mazao ya Royal Tour 👇🏾

Sauti ya Professor J. Canadian diaspora.
 
Inahusu sana tu. Mjinga ni anayeogopa kukabiliana na waandishi wa habari.

Huyu alikuwa na mambo mengi sana na hakuwa anajificha katika kuongea na waandishi wa habari!!

Mkuu acha kufananisha icho kichwa na Kabeji!
 
Mzee waa porojo tu huyo.Katuwacha masikini wa mwisho duniani, simsahau umasikini wa ujinga wa mwisho duniani aliotuwacha nao.

mama ni wa vitendo zaidi.
Kwani sasa wewe ni tajiri?
 
Back
Top Bottom