Kwanini siku hizi vijana wengi mnamchukia Mungu, mmegombana nae?

kuporomoka kwa maadili Afrika? Tujadili.
Kwa Imani uliyonayo wewe leo Babu yako mzaa Babu yako ndio ataona wewe na Babu yako ndio mmekosa Maadili kwa kuacha Mbachao...

Anyway to each his own...;

Binafsi nasema napenda watu wanao-question ili kupata ufahamu zaidi; hilo la kuhusu chuki nadhani ni la kwako - Logically kama huamini kitu kama kipo utakichukia vipi ?!!! Wanaochukia wanaamini lakini wanaona wamekuwa short-changed...
 
Naona hawamchukii Mungu ila hawaamini katika hizi dini za mchongo. Wapo katika imani yao ya jadi ambayo ndiyo Mungu wa kweli anakopatikana.
 
Vyuma vimekaza...

Wao walidhani kuwa kuwa na dini tu inatosha unaweza toboa...

Kmbe kuna kumtafuta Mungu kwa bidii na haki yake ndo utafanikiwa...
 
Kwanza elewa hiki ni kizazi Cha siku za mwisho kinaitwa Generation Z kimeanzia miaka ya elf 2.
Na yote yalitabiriwa yasingetokea Biblia ingekuwa ni kitabu Cha uongo
 
Roho ndo kitu gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Coz watu wanaamka na kuona ukweli ambao Upo wazi kwa kila mtu. Tupo peke yetu; Hakuna divine justice au divine punishment na tunaona jinsi maovu daily ya watoto kubakwa, maskini kunyanyswa etc while iyo mijambazi wanapiga raha tu na ukweli ni kwamba Hamna anayejua ukifa kuna nn; so ni watu kuwa rational tu.
 
Jina halina uhusiano na matendo ya mtu mwingine.

Ina ushahidi Mwafrika ndio mtu wa kwanza?
Ushawahi kusikia binadamu wa kwanza kugundulika kutoka Uarabuni, Ulaya, India, China, au sehemu yeyote ile zaidi ya Afrika tena hapa Afrika Mashariki? Dini ni ujinga tu, tumeaminishwa upuuzi mpaka hatujitambui akili na bado tunazidi kuchezewa tu na kina Masanja Mkandamizaji na wasanii wenziwe kina MC Pilipili na Mze wa Upako pamoja na masheikh wa michongo waliojaa hapa mjini kukimbia njaa huko mikoani.
 
Hahaha vijana tumevurugwa
Mmevurugwa kuamini dini ambazo hazina umuhimu kwetu Waafrika. We umeona wapi mtu anamuomba Mungu anaongea lugha asiyoielewa, hivi mtu ukisali kwa lugha yako ya Kiswahili huyo Mungu hakusikii kweli? Serikali ipige marufuku hizi dini hatuzitaki hapa Tanzania, tunataka maendeleo tu dini peleka Uarabuni na Israel.
 
IPO SIKU TU WATAMRUDIA WAKIPATA NEEMA. SHETANI HAJAWAHI KUWA RAFIKI WA MWANADAMU.
 
Huenda ukimuomba Mungu, hakupi haraka ila shetani ni chapchap. Na vijana mambo yao ni chapchap.
Mungu hawezi kukupa kitu unachokiomba kwa lugha ambayo hata wewe mwenyewe huielewi, unamuomba Mungu kwa Kiarab wakati wewe ni Mtanzania, kwani nani aliyesema Mungu ni mwarab? Waafrka tunajichanganya akili wenyewe tu kwa kujipa laana kuamini vitu visivyoaminika na kuingia kichwani.
 
Kwani roho ni nini Kwa mujibu wa vitabu vya dini?
 
Waliotuletea dini za Mudi na Yesu ..wao wenyewe wamekengeuka..... Sasa nigombane na nisiyemuona !!? Huo ni ulozi....
 
Hata masheikh na walimu wa madrasa wanaoa mpaka wake wanne Bado wanalawiti vitoto.... Usiingize uzani mmoja tabia ya mtu na dini/imani.
 
Tuchukulie mfano hujawahi sikia habari za mungu wala kusoma chochote kimhusuyo yeye.

Mungu ni nani na yuko wapi?
Well said, kwa hapa kwetu Afrika kabla wababaishaji waarab na wazungu kuja kutuletea dini zao za mchongo.....kila kabila hapa Tanzania lilikuwa linaamini Mungu kivyao, yaani kulikuwa na viongozi wa kikabila waliochaguliwa kuomba kwa a superior being kwa imani yao ili kuwaletea au kuwafanyia jambo fulani na walikuwa wanafanikiwa. Baada ya Usilam na Ukristu kuja, tukaacha kuabudu imani zetu na kufuata vitu vya hajabu (Uislam na Ukristu) mpaka kufikia kujilaani wenyewe. Kumbuka, kwenye imani zetu tulikuwa hatuui watu wala kubaka na ukifanya hivyo ulikuwa unachukuliwa hatua za kimila ila Uislam na Ukristu kuuana ni jambo la kawaida tena na wakati mwingine Mungu wao alikuwa anawasaidia kuua wakati Mungu huyo huyo anakataza kuua kwenye moja ya amri zake kumi au saba kwenye vitabu vya dini zao. Unapofuata dini za watu unaiga pia mila na tamaduni zao, tuamke Waafrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…