Kwanini siku hizi vijana wengi mnamchukia Mungu, mmegombana nae?

Kwanini siku hizi vijana wengi mnamchukia Mungu, mmegombana nae?

Kwa ufupi Mungu yupo,.
Tatizo tu maisha namna yalivo inasababisha kutoaminika.
Mfano wenye Imani kubwa ndio wanaougua, wanakufa nja, hawana Hela, ila haya mikurumbembe mingine inatusua tu hapo ndipo itaona kijana mwenye akil chache anaona hakuna uwepo wa Mungu.
 
Kwangu mimi naamini uwepo wa Mungu, piga ua garagaza bado nitakwambia "God is Surely Alive"

Kwa vile nilivyovishuhudia hadi kufika hapa na experience yangu ya maisha ya kiroho na kijamii kwa ujumla siwezi kukataa uwepo wake. Mungu anaishi.

Though kwa dunia ya sasa tunakutana na mafundisho mengi ya kitapeli lakini vyote haviwezi ondoa dhana ya uwepo wa Mungu....

Ukitaka ujue uwepo wa Mungu basi fungua na hii dhana ya uwepo wa Majini, mapepo, mizimu, uchawi na ushirikina... Ukianza kuvielewa hivi basi hakika utajua kuwa kuna invisible spiritual power inayo monitor dunia hii...!!

Lengo la adui (Shetani) ni kuzifunga fahamu za kibinadan zisisadiki uwepo wa Mungu just kwa simple fact wanayoiita elimu na haohao vijana wanao jiita wameelimika wanashindwa kuchunguza kuyachunguza zaidi maandiko... Wanaanza kuelea na zile simple facts wanazokutana nazo mitandaoni na mitaani!!!

Msingi mkuu wa kumjua Mungu ni maandiko na si kuyasoma tu kama gazeti lakini pia omba uvuvio wa Mungu uwe na wewe unapoanza kuzifahamu siri zilizofichwa kwenye maandiko

Nawasilisha

Agapeboy nimemaliza
Wewe nan kakwambia malengo ya shetani?

Habari ya kufunga akili kwa fact ya elimu umeipata wapi?

Kuna kauli moja huwa ni ya Kijinga sana kwa upande wangu, kauli isemayo eti maandiko kuyasoma kama gazeti" kumne yasomwaje? Assume mtu hajui na anataka amjue Mungu wenu kwa mara ya kwanza unataka akubali kwanza Mungu yupo ndio asome si ndio? Ikimaanisha kuwa akubali kila anachokikuta kwenye hadithi tata za Nyoka kuongea na yule samaki mmeza watu.

Hii kauli ni mbovu sana, Nafkiri Mungu wenu aliishiwa mbinu. Kama ni siri amezificha kumbe ni za kutafuta tena ohoooo.

Ni muda sasa wa kuzaliwa upya. Haimaanishi ulivyoishi tangu umezaliwa bhc unapaswa kuwa hivo hivo.
Na bahati mbaya mnapokosea ninyi watoto wa Mungu huwa mnadhani sie hatujawahi kuishi hayo maisha yenu, tunajua bible na quran vizur tu, ndani na nje.

Nkikuuliza tu kuhusu nje hapa najua hujui chochote, we unachokijua tu ni Nyoka aliongea, samaki alimeza watu, Jua lilisimama, bahari iliacha njia n. K.

Vua miwani hiyo.
 
tumemchoka Mungu wa mchongo asiyekuwa na haki wala faida,, Mungu ni kiziwi hasikii👽
Zamani alikuwa anasikia na kujibu kama ilivoandikwa, walivomaliza kuandika aliugua.

Ila bahati mbaya hakupona alifariki.

Sijui nani ailaze roho yake mahala pema pepon dah, 😥
Amen
 
teknolojia ambayo ni mpango wa shetani ndo imetufikisha hapa!!
Kwa akili kama hizi kwakweli tubadilike sana.

Huu uhafidhina wa dini ni wa hovyo sana.
Mpango wa shetani umekuwezesha kufuatilia uzi huu na umepost huo usaliti. Umemsaliti rafiki yetu shetani na kwakweli haikubaliki hii. Shetani kila mtu anampenda na anaurafiki naye.

Shetani ana vizuri kwa kweli.
Mungu alipowaumba hakuwa na nia ya ninyi watoto wake mfurahi.

Mimi kama mratibu wa matukio, naomba kuchukua nafasi hii kutangaza matokeo tusiwe wanafiki.
kiujumla battle la Mungu vs shetani, Shetani ni Mshindi kwa hakika. Hakuna mtoto wa Mungu anaweza kulisema hili. Lakini statistic zinaonesha. Ukibisha access tu mtaani kwako, access pia vifaa vya technology wangapi wanatumia. Kijana mtumishi anaogopa kuaproach mwanamke akiogopa kuzini lakini chumbani peke yake anacheck porn.

Niwaalike kila mmoja wenu kujitafakari.. Ni mabaya mangapi anayafanya na anahisi ni kinyume cha matakwa ya Mungu ukijumuisha pia kama unatumia technolojia zinazodaiwa ni mpango wa shetani.

Do the math.

Nb. Shetani na Mungu ni mawazo yetu sisi wanadamu.
Zawadi ya upako haitoki juu wala mahala popote, ila inatoka akilini mwako mwenyewe.
 
Kiuhalisia wengi sana wamepatwa na majanga mbali mbali ikiwemo kifo. Mfano mmoja alisimulia alipelekwa monchwari akiwa mzima nusu azikwe. Lakini pia katika mazingira yale huwezi kudumu maan utashambuliwa na wadudu tu mwisho wa siku utapata magonjwa ya ajabu. Lakini pia effect kubwa ya kukosa makazi na malazi ni humiliation kubwa sana kwa kila anaekuona njian well umetaja kariakoo mji unaotembelewa na umati wa watu je ni aibu kiasi gani. Ila ngono hufanywa sirini hakuna aibu na pia hakuna maradhi ya kusema utapata kisa hujafanya ngono na wanawake wengi zaidi zaidi wanaofanya na watu wengi ndo wako hatarini. Swali kwko je usipofanya ngono utakufa?
Maradhi kwako yapo katika makundi mangapi?
 
Halafu pia basic needs lazima watoto ndo wawe wahanga wakubwa kama ikikosekana mfano chakula mtoto hatakiwi kukosa mavazi na malazi vile vile enhee wewe ndugu yetu mtoto akikosa sex vipi kinatokea nn[emoji1787][emoji1787]
Hii ya kwako umetumia reference ipi?
Kitabu kichosema basic needs zinareflect watoto peke yake?

Embu mpitie kidogo mtaalamu mmoja anaitwa Maslow's Hierarchy of Needs.
 
L
Kasi ya watu kuwa Atheist yaani watu wasioamini uwepo wa Mungu ni kubwa sana siku hizi. Tulizoea kusikia mambo haya kwa wenzetu Ulaya na America, lakini atheism imehamia Africa na inakuwa kwa kasi kubwa mno.

Ni nini sababu za watu wengi hasa vijana kuacha kuamini katika uwepo wa Mungu na nguvu zake? Je, wimbi hili la kukosa imani kwa Mungu ndio sababu ya kuporomoka kwa maadili Afrika? Tujadili.
Labda Mungu wako.
 
Naamini kuwepo kwa Natural super power, lakini siamini katika mambo ya kipuuzi kama kutoa sadaka wala kushiriki ibada !
 
JAPO KUNA MAMBO/JAMBO LINALONIUMIZA NA MUNGU HANIPI, SIWEZ NIKAMKANA NAVUTA SUBIRA TUU AIKU IKIFIKA ATANIPA KWA MDA ANAOONA NI SAHIHI
 
Mungu ametuagiza tusamehe 7 mara 70, ila yeye kashindwa kumsamehe shetani. Ufafanuzi wa hili sijui ukoje.

Mungu alisema kuua ni dhambi lakini kwenye vitabu vya dini mara kadhaa Mungu ameua wale waliomchukiza.


Mungu Hana ugomvi na shetani. Ni wapi umesoma kua wana wana tofauti hadi amsamehe? Then unawezaje kusamehe kama huyo shetani hajakiri na kuomba msamaha na kua chini ya Mungu?

Soma kitabu cha Ayubu jinsi ambavyo shetani na Mungu wanazungumza kuhusu Ayubu Mtumishi wa Mungu. Ikiwa wangekua na magomvi wangezungumza vile?

Kinachowafanya wapishane ni wewe. Kila mmoja anakutaka wewe na wote hawataki kukupoteza. Hapo tu ndio tofauti yao. Ila shetani hukumu yake ishatolewa zamani inasubiri tu ukamilifu na yeye alisharizika na ndio maana anatafuta wa kuwapotosha wengi wa kwenda nae.

Sasa Kama yeye mwenyewe alisharidhika na hukumu yake na hayuko tayari kuomba msamaha. Asamehewe vipi?
 
Wengi hawana shida na Mungu. Wana shida na miungu-watu.
 
Mungu Hana ugomvi na shetani. Ni wapi umesoma kua wana wana tofauti hadi amsamehe? Then unawezaje kusamehe kama huyo shetani hajakiri na kuomba msamaha na kua chini ya Mungu?

Soma kitabu cha Ayubu jinsi ambavyo shetani na Mungu wanazungumza kuhusu Ayubu Mtumishi wa Mungu. Ikiwa wangekua na magomvi wangezungumza vile?

Kinachowafanya wapishane ni wewe. Kila mmoja anakutaka wewe na wote hawataki kukupoteza. Hapo tu ndio tofauti yao. Ila shetani hukumu yake ishatolewa zamani inasubiri tu ukamilifu na yeye alisharizika na ndio maana anatafuta wa kuwapotosha wengi wa kwenda nae.

Sasa Kama yeye mwenyewe alisharidhika na hukumu yake na hayuko tayari kuomba msamaha. Asamehewe vipi?
One sided story
 
[emoji1787][emoji1787]aisee hawa watu pasua kichwa. Halafu sasa wao ndo wanakuja kuleta umasikini kwenye jamii maan wengi wanashinda vijiwe vya bangi uzinzi na ulevi wa kupindukia. Huwa wanakuwaga na mageto yao ya kuvutia bangi unakuta wamejaza vitabu havieleweki eleweki wanabugia nusu nusu tu. Wengine utasikia maisha ni karata sijui zimefanyaje.
Labda unawazungumzia Rasta Farah sio atheists
 
Mhh
🤣🤣aisee hawa watu pasua kichwa. Halafu sasa wao ndo wanakuja kuleta umasikini kwenye jamii maan wengi wanashinda vijiwe vya bangi uzinzi na ulevi wa kupindukia. Huwa wanakuwaga na mageto yao ya kuvutia bangi unakuta wamejaza vitabu havieleweki eleweki wanabugia nusu nusu tu. Wengine utasikia maisha ni karata sijui zimefanyaje.
Mkuu mbona Mimi sivuti bange ??
Mheshimiwa umedanganya pakubwa


Kauli ni moja huyo jamaa mungu hayupo.
 
Back
Top Bottom