Kwanini siku hizi vijana wengi mnamchukia Mungu, mmegombana nae?

Kwanini siku hizi vijana wengi mnamchukia Mungu, mmegombana nae?

Kasi ya watu kuwa Atheist yaani watu wasioamini uwepo wa Mungu ni kubwa sana siku hizi. Tulizoea kusikia mambo haya kwa wenzetu Ulaya na America, lakini atheism imehamia Africa na inakuwa kwa kasi kubwa mno.

Ni nini sababu za watu wengi hasa vijana kuacha kuamini katika uwepo wa Mungu na nguvu zake? Je, wimbi hili la kukosa imani kwa Mungu ndio sababu ya kuporomoka kwa maadili Afrika? Tujadili.
Kwani kutokuamini Mungu ni kumchukia? Hebu acha kuwasonga waioamini
 
Ukiona mtu anaingiza story za ushoga pasipo husika,tambua huyo mtu ni shoga.
Sijaingiza pasipohusika nime-link na mukhtadha wa mlengwa km haujaelewa ni ngumu sana kukuelewesha, kwa hio wale wanaozungumzia ushoga msikitini na makanisani hadi huko bungeni wote mashoga au sio wote wanapigwa vitasa kwenye bunyero ?
 
Sasa nafsi huwa inapokea vitu?
thibitisha nafsi ndio MUNGU?
Ndio nafsi ndio hupokea na sio mwili. Mungu ni nafsi kwamba yeye sio kitu ni nafsi kama ulivyo wewe.
 
MITHALI 22:6
Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

Maombolezo 5:7
Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao.

MITHALI 10:1
Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye; Bali mwana mpumbavu ni mzigo wa mamaye.

ISAYA 54:12-13
Nami nitaifanya minara yako ya akiki nyekundu, na malango yako ya almasi, na mipaka yako yote ya mawe yapendezayo.
Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.

YEREMIA 22: 29-30
Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana.
Bwana asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Tuanzie hapa, nani aliyeandika maandishi haya???
 
Hasara anayo maana nisipofuata amri zake atanichoma moto, so energy aliyotumia kuniumba inakua wasted
Kwahyo shuleni wakiweka option kufaulu na kufeli kwamba ukifaulu unaenda chuo kikuu na ukifeli unarudi mtaani wewe huwa unawambia wamekuonea? Leteni hoja fikirishi kila machaguo duniani yana matokeo ya pande mbili.
 
Freewill?? Ukichagua asiyoyapenda anakurusha motoni. Hivi kwa nini nguvu anayotumia mungu kuandaa moto wa milele kwa wale tusiomuelewa/amini asingeitumia kumalizana na shetani once & for all?? Au kwa nini asiitumie nguvu hiyo kulinda amani ya dunia dhidi ya watu wanompigania katika ulimwengu huu??
Wewe una tofauti gani na shetani? Kwann Mungu asianze na wewe ila aanze na shetani?
 
Sababu kubwa mbili
Ya kwanza mungu hana faida duniani maana maovu yapo pale pale watu wanaiba watu wanaua watu wana dhulumiwa mfano hapa nchini kwetu tuliona wazi uchaguzi wa 2020 viongozi wengi waliingia madarakani kwa wizi wa kura na hakuna hata kiongozi hata mmoja wa dini aliekemea ule wizi wa kura je mungu anaruhusu kuiba sana sana tuliona masheikh na mapadri na wachungaji waliuenda kumpongeza raiasi aliyeiba kura kukaa madarakani maana yake dini zinabariki wizi

Jambo la pili elimu vijana wengi wana elimu kushinda wazazi wao hivyo wanakuwa wameelimika na kujua dini ni mpango maalumu wa kumtawala mtu kifikra na kimawazo wala hakuna jipya
Kumtawala kivipi kifikra? Mbona wapagani nd wanaotawala waafrica mpaka leo kwa misaada ya neti madawa na smartphone(ukoloni mamboleo).waafrica mnatawaliwa kwa kuoneshwa sijui watu wana malamborghini mandege binafsi sijui cha ajabu mnaanza kuwaabudu hao matajiri wakati mnaishia kuwa masikini wa kutupwa tu. Eti maatheist utasikia ukiacha dini utakuwa na ela muone Ellon sasa unamuuliza wewe mbona huamini je ni tajiri namba ngap duniani anatoa macho tu.
 
Kumtawala kivipi kifikra? Mbona wapagani nd wanaotawala waafrica mpaka leo kwa misaada ya neti madawa na smartphone(ukoloni mamboleo).waafrica mnatawaliwa kwa kuoneshwa sijui watu wana malamborghini mandege binafsi sijui cha ajabu mnaanza kuwaabudu hao matajiri wakati mnaishia kuwa masikini wa kutupwa tu. Eti maatheist utasikia ukiacha dini utakuwa na ela muone Ellon sasa unamuuliza wewe mbona huamini je ni tajiri namba ngap duniani anatoa macho tu.
Mkuu hapa bongo hakuna atheist ni wafuata mikumbo tu
 
Nipe kitabu ulichosoma kinachosema Sex sio basic need?
vipo vingi ambavyo ni basic needs mfano malazi mtu akikosa anakufa?
Sasa ukikosa malazi kwanini usife hujui kuna magonjwa hali ya hewa na wanyama wakali vibaka. Lakini ukikosa sex kifo kinatokeaje?
 
Mungu wetu mwenye upendo Ameamua watu wauane tu hakuna wa kumuhoji kwa sababu yeye ni mpenda haki 😀 😀 😀 😀
Sasa kwenye kuuana si huwa mnamalizana maatheist wenyewe mnataka tena Mungu aingilie mambo yenu kwanini sasa😁😁Maan wa Mungu wameagizwa wasiuane na wanafuata hawauani wanaishi kwa kupendana.
 
Mkuu hapa bongo hakuna atheist ni wafuata mikumbo tu
Kabisa aisee yani wao ni waabudu watu ila utasikia hakuna Mungu. Utasikia technology mpaka stick za kuchokonolea meno wanaletewa ila utasikia sisi tuko na technology hatufuati dini.
 
Back
Top Bottom