Wakristo Wakatoliki ndio ambao wahanga wakubwa wa kadhia hii, majengo yao mengi yalitwaliwa na utawala wa Nyerere hapa nchini. Mali ardhi na majengo ya Waislamu zilizochukuliwa na Serikali ni chache sana ukilinganisha na za Wakristo. Endapo kama ardhi hizo zote zitarejeshwa tena mikononi mwa wamiliku wake wa awali, madhara take ni kwamba WAHANGA wakubwa watakuwa Waislamu kwa sababu waislamu wengi zaidi watakosa shule na vyuo vya kusoma, watakosa huduma za afya kwa kuwa vyuo, shule na hospitali nyingi za Serikali zilizopo hapa nchini ziliporwa kutoka kwa Wakristo nabzitarejrshwa kwa Wakristo mahali ambako Waislamu hawana nafasi ya kuingia. Mfano hai ni Mimi mwenyewe, katija shule zote sita nilizosoma pamoja na Waislamu hapa nchini(Msingi shule 2+Sekondari 4), zote ziliporwa na Nyerere kutoka kwa madhehebu ya dini ua Kikristo, specifically Wakristo Wakatoliki, na baadhi ya Shule hadi leo zipo zimezungukwa na Eneo la kanisa na majengo ya Ofisi za Maaskofu, shule zipo katikati.