Kwanini Viongozi kutokea Zanzibar wanapenda kuuza ardhi ya Tanganyika?

Acheni sumu ya ubaguzi, mnapanda kitu kibaya sana. Kilicho binafsidpshwa ni uendeshaji na siyo ardhi wala bandari yenyewe.
Sumu ya ubaguzi wanaipanda wenyewe.Hivi unajua zipo asilimia 30 ya ajira kwaajili wa waZanzibar katika taasisi zote za muungano.

Huyu Mama akipewa miaka 5 tena tatizo la ajira Zanzibar litakuwa limemalizia.Fikiri wizara ya ULINZI JWTZ,wizara ya Mambo ya ndani Polisi,uhamiaji,magereza.....Taasisi kama BOT,TRA..... Watanganyika ni 59 million dhidi ya 1,8 million hapo uswa upo.

Na sasa wanaifanya TANGANYIKA landlocked country !!!!!.
 
waajiriwe tu si watanzania wenzetu
 
Na wewe umepata mgao wa karamagi wa ticts!?..kwamba uwekezaji huu utaifanya Tanzania kuwa landlocked!?..shule ulienda kunywa kamasi tu
 
Huyu ni Freeman Mbowe na maoni yake. Mnataka kuja na hoja zilizofilisika kwamba Tanganyika inaibiwa na Zanzibar.

Vipi kuhusu ufisadi wa miaka na miaka uliofanywa enzi za hayati Mkapa, akaja Kikwete na wenyewe tumeusahau?.

Mkataba haujasainiwa na muda wowote tunaweza kuukata. Vipi kuhusu madhara ya hizi chuki tunazozipalilia, nani atayaondoa wakati maji yakiwa yameshamwagika?.

Tunakimbilia akili za kipumbavu za kibaguzi lakini hatuna suluhisho ikiwa huu ubaguzi utakwenda mbali na kuuharibu Utanzania wetu.
 
Ukishauza Bandari zote,maana yake umeshatawaliwa.

Huna uwezo wa kuagiza Chakula Wala silaha wakati wa Vita.

Khalafu fikiria hivyo vita viwe dhidi yao!!!

Zamani biashara ya utumwa mambo yalikuwa hivi hivi. Babu zetu wakikimbia maporini kujificha wasiuzwe utumwani lakini wapi, watemi wanatuma watu wao kuwa kamata huko na kuwarudisha wawauze kwa Waarabu. Ndivyo ilivyo hivi sasa wako wanaosema bandari imeenda kwa miaka 100 anatokea msemaji sio kweli si miaka 100 mpuuze huo uzushi. Kumbe mkataba hauna muda maalumu yaweza kuwa hata miaka 200 au mpaka mwisho wa dunia.

Serikali inayo weza kukopa Mabilioni/Trilioni kuboresha bandari. Inakiri hadharani haaiwezi kuweka mfumo wa kuajiri Wafanyakazi wenye uwezo na waaminifu na kudhibiti ama kufukuza wafanyakazi wasio waaminifu/wezi wa bandari. Haiwezi kukopa ikapata vifaa vya kuongeza ufanisi wa utendaji wa bandari. Hizi ni kauli za dharau iliyo kubuhu na kuona walio kuaminini muwaongoze ni kama hayawani wasiojielewa.
 
Mkataba umesema ni Land LinkedπŸ˜…πŸ˜…
 
Wanaccm tumeng'ang'ania katiba hii ambayo ni vigumu hata chama kuwajibisha viongozi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…