Kwanini wanaume wengi wanaogopa kuoa wanawake wapambanaji na wanaojielewa?

Hakuna cha ubinafsi mkuu tatizo ni mgawanyo wa majukumu! Siku wanaume mkianza kufanya majukumu ya wanawake na kuyachukulia kama yenu basi na wanawake nao wataanza kufanya majukumu ya wanaume na kuyachukulia kama yao!
 
Hakuna cha ubinafsi mkuu tatizo ni mgawanyo wa majukumu! Siku wanaume mkianza kufanya majukumu ya wanawake na kuyachukulia kama yenu na wanawake nao wataanza kufanya majukumu ya wanaume na kuyachukulia kama yao!
Sasa ndani 1.4m ,unakaa nazo zaidi ya miezi miwili hata kutoa hela ya Pampas Tsh 500 kumnunulia mtoto unashindwa kweli?Wakati unajua mme wako kazi zake za kuungaunga na ndio maana kuna wengine hawataki wake zao wafanye kazi ,sasa hata 10% unacho ingiza hakionekani sasa hiyo kazi ina msaada gani the kwenye familia.

Unatetea upuuzi.
 
Kama mnajua maisha yanabadilika na kuna wakati mwanamke anaweza kumzidi kipato mumewe kwanini sasa bado mmekazana na huo mgawanyo wenu wa majukumu usio na kichwa wala miguu? Ndiyo maana nasema usimlaumu mtu kwa sababu hata wanaume mkiambiwa msaidie kazi za nyumbani huwa hamtaki hata kama mnaweza na muda mnao ila huwa mnataka wake zenu ndiyo wafanye kila kitu na bado majukumu yenu wawasaidie!
 
Endelea kukaza kichwa, ila kanzu haitokuja kufanana na dela.
 
Kasoma kapata kazi mkoa mwingine ataishi vipi kwa wazazi au walezi? Oeni wale waliofeli darasa saba mbona wapo wengi sana tena huko vijijini ndiyo wamejaa nendeni huko.
Mwanamke mpaka anapata kazi kabla ya kuolewa anakuwa tayari alishakosa sifa za kuolewa tayari.

Wanawake wa kuoa wengi bado hawajapata kazi in their early 20s.
 
Ukitaka kujua tabia ya mkeo filisika! Shida iko hapo kuwa wamama mkipata pesa hamtawaliki ndani ya nyumba.
 
System kwa jinsi ilivyo mwanamke anaeonekana mpambanaji anapitia mengi so huwa siyo mwaminifu then huwa hajitoi sana
 
Wanawake wa hivyo hawajielewi. Unafanya kazi ili iweje sasa. Mimi wala sinaga hizo, kama luku imeisha nanunua kwa hela yangu, ada za watoto nilikuwa nachangia, yaani kwz ujumla tulikuwa tunashirikiana kwz kila kitu. Ila ndio hivyo tena akapata mchepuko akarubuniwa, ila akapigwa na kitu kizito anajuta hadi leo. Maisha nikusaidiana kama mwanamke anajua thamani ya familia yake. Nafanya kazi na wanqwake wengi tu wanaojielewa.na wanachangia vizuri tu ustawi wa familia zao
 
Yaani mkiwa kama ivyo raha sana tamaa zinatugharimu sisi wanaume sometimes
 
Kasoma kapata kazi mkoa mwingine ataishi vipi kwa wazazi au walezi? Oeni wale waliofeli darasa saba mbona wapo wengi sana tena huko vijijini ndiyo wamejaa nendeni huko.
Halafu hawa wanzume bwana, wanawapeleka watoto zao wa kike shule za mamilioni ili wapate elimu nzuri na hatimaye wapate kazi nzuri halafu wanawadanyanya wenzao kuwa hawataki wanawake wapambanaji. Halafu hao hao hawataki kuwaowa watoto wa masikini kwa kuogopa vizinga.
 
Yaani mkiwa kama ivyo raha sana tamaa zinatugharimu sisi wanaume sometimes
Masuala ya usawa wa kijinsia naona tumeyachukulia vibaya. Kuwa mwanamke mwenye nafasi haimaanishi kumdharau mwenzako. Ustawi wa familia unajengwa na mume na mke, sio mmoja kumnyonya mwenzake. Nafasi zetu tuzitumie vizuri ili kumpungizia mwenza wako majukumu ya familia. Sasa mtu kazi nzuri halafu unataka upewe sijui hela za saloon, kucha etc . Mara moja moja akikupa fine lakini isiwe ndio ada.
 
Ukitaka kujua tabia ya mkeo filisika! Shida iko hapo kuwa wamama mkipata pesa hamtawaliki ndani ya nyumba.
Inategemea na mtu. Wengine tuliishi nao maisha ya kuungaunga kwa kiroho safi tu. Lakini alichonifanyia Mungu ndio anajua. Lakini na yeye alipatikana haswa
 
Sawa endeleeni kuishi kwenye hiyo hiyo mifano yenu wakati uhalisia huku ni tofauti! Endeleeni kuwangoja hao wanawake mnaowataka!
Mkienda against na nature ambayo Mungu kaiweka matokeo yake ndio haya, Single mother kibao, watoto wanakosa upendo wa familia iliyo kamilika, matokeo tunakuwa na kizazi ambacho hakina upendo na husitegemee kama kitakuwa kizazi cha kuwajibika kwenye familia.

Ila dunia ni yako chaguo ni lako kama umekaza fuvu endelea kukaza, ila 50/50 sio mpango wa Mungu.
 
Hamna huyo mwanamke, hayupo acha ufala chalii
 
Popote ulipokaa agiza kinywagi unachopenda nitumie lipa namba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…