LATRA waruhusu Mabasi kuanza safari saa 9 Usiku

Hebu tumia ubongo kufikiri, kazi ya kulinda usalama kwenye Barabara za Jamhuri ni kazi za Police wanatakiwa wafanye patrol 24 hrs kama yalivyo mataifa mengine.
Najua,lakini hoja yangu inawezekana huo ulinzi ukapatikana kwa uhakika na kwa muda wote?
Matukio mengi ya uporaji na uhalifu mwingine hutokea barabarani mara kwa mara na sote uwa tunasikia,je wamejipanga vyema kuendana na hizo ratiba mpya za mabasi?
Uwe unaelewa hoja sio kubisha bisha tu na kutukana ukifikiri huo ndio ujanja kumbe bwege tu.
 
Jamani ni bus gani linalotaka nduki ya hatari Nina safari ya kutoka arusha to dar
Nataka bus la saa 9 niingie dar na kugeuza jioni
 
Nchi jirani viwango vya barabara viko juu,

Barabara zao zinawaka taa usiku.

Bongo hiyo hakunaga!
 
Matukio mengi ya uporaji na uhalifu mwingine hutokea barabarani mara kwa mara na sote uwa tunasikia,je wamejipanga vyema kuendana na hizo ratiba mpya za mabasi?
Mimi ni dereva wa Lori ha huwa natembea usiku na mchana matukio ya utekaji sio mengi na polisi wanawaweza vizuri sana.
 
Wazo zuri. Lakini Sasa madereva wetu hawa mmh!
Labda kuwe na ufuatiliaji katika kila kituo. Wawe wanapimwa Kama hawajapiga kamnyweso.
Dar - songea,
Chuma ikitoka mbezi saa 9, saa 2 usiku inaingia shule ya Tanga. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Msosi wa usiku unakuta uko mezani.
 
Matokeo ya kulazimisha mambo huwa mabaya. Ajali zitakuwa nyingi sana na matukio ya magari kutekwa na majambazi yataongezeka.

Tuwe wavumilivu, SGR itatupa usalama zaidi kusafiri usiku.
Huwezi tibu kidonda Hadi uwe nacho. Magari yatembee 24hrs then changamoto zitakazojitokeza baada ya hapo ndio wenye dhamana wajipange kupambana nazo
Tusitishane wewe ni muoga hata wa maisha yako binafsi kwenye kufanya maamuzi.
 
Kila mwanasiasa ni mmiliki wa mabasi tutarajie kusikia mengi.
 
ni wazo zuri lakini balaa linaanzia kwa watu wenyewe wanaoendesha hayo mabasi, mapolisi tunaowategemea kwenye controling, miundo mbinu yenyewe ya barabara, aina ya mabus yenyewe na wamiliki wake.
 
Nadhani ni suala la muda tu, maana kuna mambo hayaepukiki kwenye dunia hii inayokwenda kwa kasi ajabu.

Ilianza saa 12 mara saa 11, sasa ni saa 9 kutoka popote pale ndani ya Tanzania kuelekea mikoa mingine ili mradi ukidhi vigezo hasa kigezo cha LATRA kukuruhusu.

Mamlaka ya usafiri ya udhibiti wa usafiri ardhini nchini imewaagiza wamiliki wa mabasi wanaopenda kuanza safari muda huo wa saa tisa usiku wafike katika Ofisi zao kuomba upya leseni.

Salum Pazzy anayekaimu kitengo cha uhusiano na mawasiliano cha LATRA amesema, ni lazima madereva wasajiliwe ili kuwa na taarifa zao za msingi.

Kwa maoni yangu, angalau kidogo mnasogea japo bado sana maana tunapaswa kusafiri 24hrs katika dunia inayopungua ukubwa kila siku, ikiwa watu hawalali kwa sasa wakikimbia huko na huko.
Screen Shot 2023-06-02 at 13.29.33.png
 
Afadhali sasa maana inakera sana mtu kufika kituoni saa 8 usiku lakini unalazimishwa kusubiri hadi saa 12 asubuhi ndipo gari iruhusiwe. Kwa mbaaaali naanza kuona matumaini.
 
ni wazo zuri lakini balaa linaanzia kwa watu wenyewe wanaoendesha hayo mabasi, mapolisi tunaowategemea kwenye controling, miundo mbinu yenyewe ya barabara, aina ya mabus yenyewe na wamiliki wake.
Wakiendesha mchana , Mapolisi, miundombinu na madereva wanabadilika?
 
Kwani hiyo saa 11 yanaanza safari?! Abiria tutaweza kuwepo hiyo saa 9 Kwa ajili ya safari?!
 
Bm wameanza toka March , 2023 na mabasi yanajaa, Wakatu unaumwa wenzako wanapona, wakati unasubiri liive wenzio wanakula na chumvi, wakati unatembea wenzio wanakimbia, wakati unawaza wenzio wanatenda "Wachagga kila siku wako mbele hatua 3 zaidi yetu watu wa kusini".

Sikudhihaki ila utakuwa mtoto wa mika ya 2000's, toka tumepata uhuru mpaka mwaka 1998 safari za Treni kutoka Arusha-Moshi-Tanga zilikuwa saa 11 jioni mpaka asubuhi.

Safari za mabasi ilikuwa kuanzia saa 12 jioni na kufika asubuhi[nikufahamishi ] namna tunavyosonga mbele ndio akili zetu zilikuwa zinadumaa na safari zikalazimishwa ziwe mchana.
huu si utaratibu mpya, ulikuwepo kabla haujatungishwa mimba[ukiwa kiunoni kwa mshua wako].
 
Asante kwa shule yako. Ni kweli mimi ni wa 2000's
 
Mwaka 19990-95 tulipanda mabasi haya kutoka Arusha kuja Dar,
1. Fresh ya Shamba.
2. SUKIWA,
3. Njuweni
4. Shabaha,
5. Mkombozi,
6. Bazuu.
7. Oxygen.
8. Ngorika.
9. Mfahamiko.
11. Sukiwa.
12. Dar express.
13. SAWAYA [Kilimanjaro Express]
14. Marangu [Marangu coach].
15. Air Msae.
16. Buffalo.
 
Ni kweli mi ni wa 2000's ila huo mwaka mliokuwa mnayapanda naona kama umetupiga!!!
 
Back
Top Bottom