Naona hii ni hatua nzuri ingawa bado.
Kinachihitajika ni kusafiri saa 24.
Tunafahamu kuwa hapa nchini mwetu, ukiondoa mabasi, vyombo vingine vyote vinasafiri saa 24.
Hivi sasa baadhi ya njia/barabara zinazosemekana kuzuiwa kusafiri saa 24, mabasi yanasafiri hadi saa 6 au 7 usiku kisha yanaendelea na sadari saa 11 au 12 alfajiri.
Je, tuamini kuwa ajali ambazo "Wataalamu" wanazizuia, zinatokea muda huo wa kati ya saa 7 usiku na 11 alfajiri?
Nashauri wenye mabasi waruhusiwe kupanga muda wa kuanza na kumaliza safari zao.
Kwanza ni utaratibu mbaya kuruhusu mabasi kuanza safari kwa wakati mmoja kama ilivyo sasa kwa kuondoka saa 12 asubuhia.
Hivi hii ni 'Marathon'?
Kwa nini.mabasi yote yafuatane?
Yakishaondoka alfajiri unakuwa umekwama kusafiri.
Hapo ndipo tunaleta umaarufu na kuhitajiwa sana hizo Coaster za "Hakuna kulala"
Kwa kuwa mabasi ni biashara na ni huduma, waachwe kupanga muda ufaao.
Mfano, basi linaloondoka Dar au mkoani saa 12 jioni litapata wateja wengi kwa kuwa abiria ambao wanahitaji kwenda kuona familia zao wataondoka muda huo (siku ya Ijumaa) wafike waendako asubuhi na Jumapili jioni wapande mabasi kurudi na wafike waendako alfajiri ya Jumatatu na waingie kazini.
Tunakumbuka mabasi yalivyokuwa yakisafiri usiku kucha.
Tulisafiri nayo.
Wataalamu leteni suluhisho badala ya vikwazo.
Mnatuumiza kwa masharti yenu.
Mungu ibariki Tanzania.