LEMA: Baadhi ya wabunge kati ya 19 ni wake wa viongozi wakuu wa CHADEMA

LEMA: Baadhi ya wabunge kati ya 19 ni wake wa viongozi wakuu wa CHADEMA

“Unawezaje kwenye meza kuu Mwenyekiti unakaa na manaibu Katibu wakuu wawili ambao wake zao ni sehemu ya wabunge 19 waliopo bungeni, halafu Msigwa akawa hatari, mimi niliongea Mtwara kuwa wanapaswa kujiuzuru msitupe ugumu wa Maisha, haiwezekani wawe wanaanda nyaraka za Ushahidi za Kwenda mahakamani dhidi ya wake zao.”

“Inawezekanaje mbunge Msigwa ambaye mmekorofishana pengine kwa maneno ambayo hayana maana, mnashindwa kupatana halafu Halima Mdee ambaye walikipeleka chama Mahakamani, wanakuwa kwenye ‘Party’ yako ya kufunga mwaka.” Godbless Lema

View attachment 3201877
Kwani kambi ya Mbowe nasikia kina Sugu wenyewe wanasemaje kuhusu Mbowe kugombea?
 
Inasikitisha. Kwa mawazo yangu nadhani itakuwa heri kwa CDM kama Lissu atashinda uchaguzi. Yeye na timu yake ikishinda itawapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao wa kuongoza chama. Watapimwa kuanzia Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu mpaka wa 2030. 2030 watapimwa kutokana na track record yao.

Amandla...
 
Mimi nadhani Chadema mpaka sasa tumejidhihirishia kuwa hakuna hata demokrasia.

Halafu mambo yakuchambana hovyo yameishusha sana hadhi ya chama. Tumesikitishwa sana na hii minyukano ambayo haikuwa na maana.

Ila huwa wanasema acha inyeshe tujue panapovuja.
 
Mbowe atakuja na Ngojera zake mara nimekitoa Mbali Chama, Mara Nimetoa Mbali Lissu vitu ambayo Ni irrelevant kabisa, Ajibu Hoja hapa Hatutaki Hadithi zenye sympathies tunataka Facts kama izi Za Mkuu Lema
 
Kwani alichosema ni uongo? Mbona kasema aliwaambie wake wajihudhuru hujasikia?
Issue sio authenticity ya anachokisema ukizingatia anakisema / hakukisema wakati gani.., Unaweza ukasema ukweli ila mazingira yakakufanya ukawa tu kama Yuda (Hata kwenye Story, Yuda alivyombusu Yesu, ni kweli yule alikuwa ni Yesu), ingawa mazingira ndio yanapelekea leo hii akumbukwe either fondly au badly...
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom