Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Hebu niambie, ni wapi hapa duniani wanakojielewa ambako utaukuta huu usafiri wa bodaboda? Kama hakuna, tafakari..
Kama hoja ni kuendesha maisha, si hata wanaofanya ukahaba wanaendesha maisha kwa ukahaba wao.
Kwani lazima kuiga Kila kitu? Sio swala la kujielewa ni swala la mazingira ya Kila Nchi..

Harafu hii mode of transport imetokea miaka ya hivi karibuni pamoja na Bajaj na asili yake ni Asia.

Mwisho kwani pikipiki zinatengenezwa Kwa Ajili ya nini hasa?
 
Kuna watu wanafikiri kauli ya Lema kuhusu bodaboda inaweza kumpunguzia popularity na support toka kwa wafuasi wake hizo ni ndoto za mchana na huyo Gambo ajiandae kwani mama ameahidi hakutakuwa na mbeleko kama za enzi za mwendazake 2020 so ana kazi kubwa mno ya kufanya
 
Tupeni ridhaa muone mikakati yetu. Siyo miaka sirini yote ya uongozi hamna ubunifu wowote kazi yenu ni kuwasisitiza tu vijana wajiajiri. Kama mmeishiwa mbinu si mseme?
Wewe unasema kama nani hapo CHADEMA?
 

Na bado vibration disease inawasubiri watakaofikisha miaka 45 na kuendelea.

Tena wakiwa hawana hata akiba ya tiba ukizingatia kazi yenyewe haimuwezeshi anayeifanya kuweka akiba.

Kuendesha bodaboda kama lifetime occupancy sio poa kwa kweli.

Asingetumia maneno yenye kutoa nafasi kwa wanaosubiri kupotosha kila kitu kwa faida za siasa chafu lakini ujumbe unabaki vile vile.
 
Kumuulewa Lema unahitaji kuwa na akili kwanza, Kama huna akili huwez kumuelewa Kama ambavyo we hukumuelewa

Mie nilitaka kuendesha Bodaboda, Yes bro wangu anaendesha Bodaboda lakini alinishauri nisifanye hiyo kazi daima, Japo yeye amejenga kwa kazi hiyo hiyo lakin haishi kuilaani na kutafuta mbadala

Hukumsikiliza Lema ukamuelewa, labda Kama ulimsikiliza basi uwezo wako Ni mdogo sana

Imagine mtu aendeshe Bodaboda miaka 30, yaan akimbize upepo miaka 30, sijui Kama ulielewa hoja ya Lema

You must be very stupid kusema Kuendesha Bodaboda Ni kazi ya kujivunia,


Hata uwe na nyumba, ukienda Bank ukawaambia una nyumba na kazi yako Ni Bodaboda kwahiyo wakupe mkopo, utapewa?
 
Acha kupotosha alivyokuwa anamaanisha.Rudia tena kumsikiliza.
Acha kuwalisha bodaboda maneno ya chuki dhidi ya Chadema
Mbona wa kwenu aliwahi kusema (wazuri hawafi)
 
Hata mi nasema ni laana Wala hajakosea. Hakuna anayetaka kuwa bodaboda Bali ni ccm kufeli kuwapa ajira vijana kwa hiyo bodaboda ni last option. Hivyo kwa kifupi ccm Haina mbinu za kuwakwamua vijana
Wewe ni mpumbavu si mjinga. CCM iko Malawi? Kenya? DRC? Rwanda?
Akili zako ni ndogo kama Lema tu
 

Ni kawaida sana kwa mtu ambaye ameenda kuishi ulaya au Marekani kwa mara ya kwanza kuwa na maoni kama hayo. Ukitoka huko na kurudi nyumbani unaona hali zilivyo ughaibuni na nyumbani ni kama ardhi na mbingu. Tofauti ni kubwa sana, hivyo unakuwa na moto wa kubadili na kurekebisha mambo.

Bado akili yake haija weza ku balance hali.
Mumpe muda akili yake itasawazika tu, maoni na maneno yake yatakuwa tofauti.
 
Bodaboda na Bajaji na Machinga wakiwekewa utaratibu mzuri na miundombinu na wawe operational maeneo Fulani Fulani ni kazi ya kuingiza kipato..

Huko Vijijini ni usafiri muhimu sana,kwanza sijajua inakuaje laana.
Atoe mbadala kwanza kuliko kulaumu tu
Mi naona heri kuwa boda kuliko jambazi
Ukijihimu mbona wanapata si sawa na kukaa bure
 
Kusema kazi fulani ni laana wakati kazi yeyenyewe haivunji sheria za nchi ni kuwakosea heshima watu wanaofanya Hiyo kazi na lazima ujue sio kila mtu atakuwa dokta, mwanasheria, mwanasiasa n.k
 
Hebu niambie, ni wapi hapa duniani wanakojielewa ambako utaukuta huu usafiri wa bodaboda? Kama hakuna, tafakari..
Kama hoja ni kuendesha maisha, si hata wanaofanya ukahaba wanaendesha maisha kwa ukahaba wao.
 
Umesahau kuweka namba ya sim.
Kwa andiko lako hili ni wazi kuwa hujawahi kutoka nje ya Afrika. Bodaboda siyo kazi ni vile tu CCM wamedunisha uchumi wa nchi mpaka vijana wanakosa kazi sahihi za kufanya. Nchi yoyote iliyoendelea au iliyostaraabika utakuta pikipiki inatumika kama usafiri binafsi na si usafiri wa uma.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…