Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Hebu niambie, ni wapi hapa duniani wanakojielewa ambako utaukuta huu usafiri wa bodaboda? Kama hakuna, tafakari..
Kama hoja ni kuendesha maisha, si hata wanaofanya ukahaba wanaendesha maisha kwa ukahaba wao.
Kwani lazima kuiga Kila kitu? Sio swala la kujielewa ni swala la mazingira ya Kila Nchi..

Harafu hii mode of transport imetokea miaka ya hivi karibuni pamoja na Bajaj na asili yake ni Asia.

Mwisho kwani pikipiki zinatengenezwa Kwa Ajili ya nini hasa?
 
Kuna watu wanafikiri kauli ya Lema kuhusu bodaboda inaweza kumpunguzia popularity na support toka kwa wafuasi wake hizo ni ndoto za mchana na huyo Gambo ajiandae kwani mama ameahidi hakutakuwa na mbeleko kama za enzi za mwendazake 2020 so ana kazi kubwa mno ya kufanya
 
Tupeni ridhaa muone mikakati yetu. Siyo miaka sirini yote ya uongozi hamna ubunifu wowote kazi yenu ni kuwasisitiza tu vijana wajiajiri. Kama mmeishiwa mbinu si mseme?
Wewe unasema kama nani hapo CHADEMA?
 
Vijana wanafanya bodaboda baada ya kukosa njia mbadala za kujitafutia vipato. USA, Canada, South Africa, Dubai kuna bodaboda? Hakuna, sababu ni kwamba kijana anapata ajira yenye staha, ya kufanya, na kipato cha kukidhi maisha yake.

Zamani kabla ya bodaboda hazijaanza, kulikuwa na asekdo, usafiri wa baiskeli. Hizi ni njia za kujiaptia vipato kwa watu kwenye nchi zenye ufukara na umaskini uliokithiri.

Hivi kweli usomeshe mtoto umtayarishe awe bodaboda!! Ulaana wake unaanzia hapo, kazi haina akiba ya NSSF, haina bima, wakubwa wakiamua hata mjini unazuiwa usiingie. Niambie mtoto gani wa mkubwa anafanya hiyo kazi. Kazi haina mkataba wa kazi, unaweza ukafukuzwa wakati wowote.

Ni kazi ya hovyo sana, acha kuwaza kimaskini, uchumi wako inabidi ukue ili uachane na hiyo kazi, ufanye kazi ya Uber, umiliki teksi kadhaa, na logistic company. Nina jamaa yangu, tulipotoka chuo, 2010, tukapata kazi, yeye baada ya muda, akazichanga pesa yake akanunua kakorola mkweche, akazama zake Arusha, akasema bora akafanye kazi ya kubeba watalii na wageni. 2020, tulipokutana, tayari ameishasajiri kampuni yake ya tours, anakodisha gari zake tatu, salon cars, na Noah. Inabidi uwaze hivyo, na huyu ni engineer, akiwa hana kazi anapiga kazi za ufundi.

Sasa wewe umeingia kwenye bodaboda, hukuwa na mbadala mwingine, na kwanini mbadala wako baada ya kupigika iwe bodaboda? Kwanini hukuenda USA, au mgodini, au viwandani, ukampiga pesa ndefu kwa kazi za kubeba boksi, sababu ni kwamba hizo fulsa hazipo, hata passport huna, mifumo sio rafiki kwako, hukopesheki. Ulaana wa bodaboda unaanzia hapo, na si bodaboda, hata ajira zingine kama kutembeza karanga, kuuza aiskrimu, kuuza mahindi ya kuchoma, zote ni laana tu, kipato chini ya milioni 1.5, ni umaskini tu.

Na bado vibration disease inawasubiri watakaofikisha miaka 45 na kuendelea.

Tena wakiwa hawana hata akiba ya tiba ukizingatia kazi yenyewe haimuwezeshi anayeifanya kuweka akiba.

Kuendesha bodaboda kama lifetime occupancy sio poa kwa kweli.

Asingetumia maneno yenye kutoa nafasi kwa wanaosubiri kupotosha kila kitu kwa faida za siasa chafu lakini ujumbe unabaki vile vile.
 
Kumuulewa Lema unahitaji kuwa na akili kwanza, Kama huna akili huwez kumuelewa Kama ambavyo we hukumuelewa

Mie nilitaka kuendesha Bodaboda, Yes bro wangu anaendesha Bodaboda lakini alinishauri nisifanye hiyo kazi daima, Japo yeye amejenga kwa kazi hiyo hiyo lakin haishi kuilaani na kutafuta mbadala

Hukumsikiliza Lema ukamuelewa, labda Kama ulimsikiliza basi uwezo wako Ni mdogo sana

Imagine mtu aendeshe Bodaboda miaka 30, yaan akimbize upepo miaka 30, sijui Kama ulielewa hoja ya Lema

You must be very stupid kusema Kuendesha Bodaboda Ni kazi ya kujivunia,

Hata uwe na nyumba, ukienda Bank ukawaambia una nyumba na kazi yako Ni Bodaboda kwahiyo wakupe mkopo, utapewa?
 
Acha kupotosha alivyokuwa anamaanisha.Rudia tena kumsikiliza.
Acha kuwalisha bodaboda maneno ya chuki dhidi ya Chadema
Mbona wa kwenu aliwahi kusema (wazuri hawafi)
 
Hata mi nasema ni laana Wala hajakosea. Hakuna anayetaka kuwa bodaboda Bali ni ccm kufeli kuwapa ajira vijana kwa hiyo bodaboda ni last option. Hivyo kwa kifupi ccm Haina mbinu za kuwakwamua vijana
Wewe ni mpumbavu si mjinga. CCM iko Malawi? Kenya? DRC? Rwanda?
Akili zako ni ndogo kama Lema tu
 
Hello!

Naona Lema ameanza kwa gia ya matusi kwa wanaojiita bodaboda. Lema amesema bodaboda sio kazi ila ni laana.

Hivi hizi si ni dharau kwa vijana wa bodaboda? Yaani watu wanaendesha familia kwa kazi hiyo halafu anakuja mtu anawadharau na kutukana eti wamelaaniwa?

Nyie wafuasi wa CHADEMA mnaposhabikia watu muwe mnajitambua. Hawa kina Lema wamekuwa wabunge hapo Arusha miaka 10, waliwafanyia nini cha maana?

Ujinga kama huu wa CHADEMA ndio kina Ruto walikuwa wanawadanganya Kenya badala yake hakuna cha maana anafanya; ameongeza tax, ameondoa ruzuku kwenye mafuta maisha yako juu, anakopa na alisema hatokopa, anaomba misaada ya chakula hadi Ukraine, mfumuko wa bei ndio usiseme nk.

Ujinga kama huu wa upinzani ulifanyika hata Malawi, kawaulize Wamalawi kama kuna nafuu wamepata, the likes ya Zambia.

Ukiwasikiliza CHADEMA huwa wanaota ila hawana strategy ya kile wanachoota, uje uwaulize watawatoa vipi Watanzania kwenye umaskini kama wanavyodai wakati hawana hata sera inayoeleweka.

Toka nimeanza kuwasikiliza CHADEMA zaidi ya Katiba Mpya na mambo ya Majimbo hakuna jipya, maana hizo political tools sio nyenzo za kuondoa watu kwenye umaskini.

Mwisho, ukiwasikiza ACT Wazalendo unaona content ila ukiwasikiza CHADEMA unaona ulalamishi na kuorodhesha matatizo ya Watanzania bila suluhisho.

Watanzania stukeni mnafanyiwa ngazi za kutengenezea watu maisha.

View attachment 2534553View attachment 2534613

Ni kawaida sana kwa mtu ambaye ameenda kuishi ulaya au Marekani kwa mara ya kwanza kuwa na maoni kama hayo. Ukitoka huko na kurudi nyumbani unaona hali zilivyo ughaibuni na nyumbani ni kama ardhi na mbingu. Tofauti ni kubwa sana, hivyo unakuwa na moto wa kubadili na kurekebisha mambo.

Bado akili yake haija weza ku balance hali.
Mumpe muda akili yake itasawazika tu, maoni na maneno yake yatakuwa tofauti.
 
Bodaboda na Bajaji na Machinga wakiwekewa utaratibu mzuri na miundombinu na wawe operational maeneo Fulani Fulani ni kazi ya kuingiza kipato..

Huko Vijijini ni usafiri muhimu sana,kwanza sijajua inakuaje laana.
Atoe mbadala kwanza kuliko kulaumu tu
Mi naona heri kuwa boda kuliko jambazi
Ukijihimu mbona wanapata si sawa na kukaa bure
 
Kumuulewa Lema unahitaji kuwa na akili kwanza, Kama huna akili huwez kumuelewa Kama ambavyo we hukumuelewa

Mie nilitaka kuendesha Bodaboda, Yes bro wangu anaendesha Bodaboda lakini alinishauri nisifanye hiyo kazi daima, Japo yeye amejenga kwa kazi hiyo hiyo lakin haishi kuilaani na kutafuta mbadala

Hukumsikiliza Lema ukamuelewa, labda Kama ulimsikiliza basi uwezo wako Ni mdogo sana

Imagine mtu aendeshe Bodaboda miaka 30, yaan akimbize upepo miaka 30, sijui Kama ulielewa hoja ya Lema

You must be very stupid kusema Kuendesha Bodaboda Ni kazi ya kujivunia,

Hata uwe na nyumba, ukienda Bank ukawaambia una nyumba na kazi yako Ni Bodaboda kwahiyo wakupe mkopo, utapewa?
Kusema kazi fulani ni laana wakati kazi yeyenyewe haivunji sheria za nchi ni kuwakosea heshima watu wanaofanya Hiyo kazi na lazima ujue sio kila mtu atakuwa dokta, mwanasheria, mwanasiasa n.k
 
Hebu niambie, ni wapi hapa duniani wanakojielewa ambako utaukuta huu usafiri wa bodaboda? Kama hakuna, tafakari..
Kama hoja ni kuendesha maisha, si hata wanaofanya ukahaba wanaendesha maisha kwa ukahaba wao.
 
Hello!

Naona Lema ameanza kwa gia ya matusi kwa wanaojiita bodaboda. Lema amesema bodaboda sio kazi ila ni laana.

Hivi hizi si ni dharau kwa vijana wa bodaboda? Yaani watu wanaendesha familia kwa kazi hiyo halafu anakuja mtu anawadharau na kutukana eti wamelaaniwa?

Nyie wafuasi wa CHADEMA mnaposhabikia watu muwe mnajitambua. Hawa kina Lema wamekuwa wabunge hapo Arusha miaka 10, waliwafanyia nini cha maana?

Ujinga kama huu wa CHADEMA ndio kina Ruto walikuwa wanawadanganya Kenya badala yake hakuna cha maana anafanya; ameongeza tax, ameondoa ruzuku kwenye mafuta maisha yako juu, anakopa na alisema hatokopa, anaomba misaada ya chakula hadi Ukraine, mfumuko wa bei ndio usiseme nk.

Ujinga kama huu wa upinzani ulifanyika hata Malawi, kawaulize Wamalawi kama kuna nafuu wamepata, the likes ya Zambia.

Ukiwasikiliza CHADEMA huwa wanaota ila hawana strategy ya kile wanachoota, uje uwaulize watawatoa vipi Watanzania kwenye umaskini kama wanavyodai wakati hawana hata sera inayoeleweka.

Toka nimeanza kuwasikiliza CHADEMA zaidi ya Katiba Mpya na mambo ya Majimbo hakuna jipya, maana hizo political tools sio nyenzo za kuondoa watu kwenye umaskini.

Mwisho, ukiwasikiza ACT Wazalendo unaona content ila ukiwasikiza CHADEMA unaona ulalamishi na kuorodhesha matatizo ya Watanzania bila suluhisho.

Watanzania stukeni mnafanyiwa ngazi za kutengenezea watu maisha.

View attachment 2534553View attachment 2534613
Umesahau kuweka namba ya sim.
Kwa andiko lako hili ni wazi kuwa hujawahi kutoka nje ya Afrika. Bodaboda siyo kazi ni vile tu CCM wamedunisha uchumi wa nchi mpaka vijana wanakosa kazi sahihi za kufanya. Nchi yoyote iliyoendelea au iliyostaraabika utakuta pikipiki inatumika kama usafiri binafsi na si usafiri wa uma.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom