Vijana wanafanya bodaboda baada ya kukosa njia mbadala za kujitafutia vipato,
USA,CAnada,South Afrika,Dubai Kuna bodaboda?hakuna,sababu ni kwamba kijana anapata ajira yenye staha,ya kufanya,na kipato Cha kukidhi maisha yake.
Zamani kabla ya bodaboda hazijaanza kulikuwa na asekdo,usafiri wa baiskeli.
Hizi ni njia za kujiaptia vipato kwa watu kwenye nchi zenye ufukara na umaskini uliokithiri.
Hivi kweli usomeshe mtoto umtayarishe awe bodaboda!!
Ulaana wake unaanzia hapo,kazi Haina akiba ya nssf,Haina bima,wakubwa wakiamua hata mjini unazuiwa usiingie,
Niambie mtoto gani wa mkubwa anafanya hiyo kazi.
Kazi Haina mkataba wa kazi,unaweza ukafukuzwa wakati wowote.
Ni kazi ya hovyo sana,acha kuwaza kimaskini,uchumi wako inabidi ukue,Ili uachane na hiyo kazi,ufanya kazi ya Uber,umiriki teksi kadhaa,na logistic company,
Nina jamaa yangu,tulipotoka chuo,2010,tukapata kazi,yeye baada ya muda,akazichanga pesa yake akanunua kakorola mkweche,akazama zake Arusha,akasema Bora akafanye kazi ya kubeba watalii,na wageni,2020,tulipokutana tayari ameishasajiri kampuni yake ya tours,anakodisha gari zake tatu,salon cars,na Noah,inabidi uwaze hivyo,na huyu ni engineer,akiwa Hana kazi anapiga kazi za ufundi.
Sasa wewe umeingia kwenye bodaboda,hukuwa na mbadala mwingine,na kwanini mbadala wako baada ya kupigika iwe bodaboda?kwanini hukuenda USA,,au mgodini,au viwandani,ukampiga pesa ndefu kwa kazi za kubeba boksi,sababu ni kwamba hizo fulsa hazipo,hata passport huna,mifumo sio rafiki kwako,hukopesheki,ulaana wa bodaboda unaanzia hapo,na si bodaboda,hata ajira zingine kama kutembeza Karanga,kuuza aiskrimu,kuuza mahindi ya kuchoma,zote ni laana tu,kipato chini ya milioni 1.5,ni umaskini tu