Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Jaribuni kufikiria kidogo, kwanini Bongo Kuna bodaboda, Dubai, Marekani, Canada hakuna bodaboda? Kwanini kijana wa Tanzania, akose ajira ya maana viwandani,akimbilie bodaboda kama mbadala wa kusongesha maisha?
Kuna wakati ni heri kijana akaendesha bodaboda kwa kipato cha kawaida na risks nyingi kuliko kwenda pale Kiboko kuwa mfanyakazi wa kiwanda cha bomba(hollow sections) na nondo. Trust me!
 
Ww km unakataa sio laana ni maoni yako na lema katoa maoni yake katiba unawapa uruhu nyie wote kutoa maone na fikla zake
Aache kudharau kazi za watu,Kwa nini hakukodisha magari badala yake akakofisha bodaboda?
 
Najiulizaga Hawa bodaboda wakifika miaka 45 na kuendelea itakuwaje?🏃🏃
 
Nabii fake wa siku za mwisho 😁😁
 
Umemsikiliza Lema ila bahati mbaya hujamuelewa,pole sana
 
Lema amegundua tatizo kuwa ni mindset zetu.

Hongera sana Kamanda.
 
Lema kwa kuwa yeye amelipwa pesa za bure basi anataka kila mtu iwe hivyo. Bodaboda ni kazi nzuri
 
Umaskini ni LAANA.

Bt Maskini kama boda, matching guys nk Si LAANA maana wao wanapitia hapo kupanda juu kujikwamua kimaisha.

LAANA ni kuamini kuwa BODA ni AJIRA ya kudumu Kwa vijana kuepuka UNEMPLOYMENT problem.

Lema Yuko sawa kabisa.
 
Umemaliza mkuu..sina haja ya kuwajibu hawa wajinga tena. Wanadhani waendesha bodaboda wanapenda hiyo kazi,hawapendi kufanya kazi viwandani wapate mishahara mikubwa, bima,afya, mikopo... Haya majinga ya ccm hayajui
 
Lema kwa kuwa yeye amelipwa pesa za bure basi anataka kila mtu iwe hivyo. Bodaboda ni kazi nzuri
Ni mtoto wa waziri, RC, DC au kiongozi gani wa umma anayefanya kazi ya kuendesha bodaboda??
 
- Hoja yake ni kwamba serikali imeshindwa kutengeneza mazingira ya kutoa ajira rasmi na za staha.
Kama anaona serikali imeshindwa kutengeneza mazingira wezeshi ya ajira staha yeye kama mwanasiasa na Moja ya kiongozi wa Chadema, chama chake pamoja na yeye Wana Maoni gani au sera zipi zitakazotengeneza hizo kazi za staha si tu unabeza kazi za watu na mwisho utoi solution wewe utakuwa una tofauti gani na chama tawala?
 
Kama ni ujinga, huu ni ujinga uliopitiliza.
Watu wamefika kumpokea kwa Bodaboda, baada ya muda mfupi unaanza kuwaita wana laana.
Lema anatakiwa kuomba radhi haraka sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…