Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mkuu,Tatizo haiko kwa LILIAN , liko kwa kwenye mfumo wa chuo ulioshindwa kumshawishi Lilian aone fursa inayoendana na anachosoma...pili Watoto wamesababisha au kuchangia wazaz Kula RUSHWA na KUIBA ili wawafurahishe watoto wao, Karo 4m Kwa mshahara wa 1m, unaweza ona gape Hilo na huyo ana watoto 3, pia ndo njia za kukwepa Kodi ili mtoto asome....Elimu Hailet maarifa but exposure do.
OME...
Umeandika "Tatizo haiko kwa LILIAN , liko kwa kwenye mfumo wa chuo ulioshindwa kumshawishi Lilian aone fursa inayoendana na anachosoma.."
Kwani ni lazima mtu kufanya kazi katika masomo aliyosomea?
Yani mpaka kwenye dunia ya leo inayobadilika sana kila mwaka yanakuja mambo mapya ya teknolojia mpya, bado tunategemea watu wafanye kazi kwenye nyanja za masomo waliyosomea tu?
Katika dunia hii ambayo teknolojia inaenda kwa kasi kubwa sana kuliko mitaala, si kwetu tu, dunia nzima, unategemea vipi watu wafanye kazi kwa kuangalia vitu walivyosomea tu?
Huoni kwamba haya ni mawazo ya mgando sana yaliyopitwa na wakati katika dunia ya leo?