Mkuu madiwani wa moshi walijaribu ccm wakakimbilia mahakamani mkuu
soma hapa hii habri iliandikwa tarehe 3 april 2011 Vuta ni kuvute baina ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi juu ya viwanja viwili vinavyotumiwa na CCM imeendelea kugonganisha pande zote katika Manispaa ya Moshi.
Mvutano huo kwa sasa umeifanya Chadema mkoani Kilimanjaro kutoa muda wa siku 30 kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bernadetta Kinabo, na Katibu wa CCM mkoa, Steven Kazidi, kufuta kauli zao za kusema kuwa chama hicho kinafanya uchochezi na kina haja ya kumwaga damu, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mwenyekiti wa Chadema mkoani hapa na Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, alitoa kauli hiyo jana katika tamko la chama hicho lililotolewa mbele ya waandishi wa habari na madiwani wa Chadema wa Manispaa hiyo.
Kabla ya Mbunge huyo kutoa tamko hilo, Katibu wa Chadema mkoani hapa, Basil Lema, alitoa tamko la chama la kulaani kauli zilizotolewa na viongozi hao za kudai kuwa chama hicho kimejipanga kupeleka wananchi 50 kwa kila diwani siku ya Baraza la madiwani kwa ajili yakufanya vurugu, jambo ambalo si kweli.
Alisema Mkurugenzi huyo alidai kuwa chama hicho kupitia madiwani wake wamejipanga kufanya vurugu na kuharibu majengo na mali za Halmashauri ya Manispaa na kwamba mali hizo ndio wanazozisimamia iweje waziharibu. "Napenda kutamka kwa maneno ya masikitiko yangu kwake kwa namna alivyoonyesha na anavyoonyesha dharau ya wazi kwa mstahiki Meya, Michael Jaffary na madiwani wa Manispaa, kwa hakika lazima kuna mtu yuko nyuma yake katika kutekeleza dharau hii, haiwezekani kiburi hiki kikakosa mizizi mirefu kutoka katika mfumo wa utawala wa nchi," alisema Lema.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI