Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mi naona ni kila halimashauri ya wilaya au mkoa ishughulikie hilo swala viwanja na hii itafanya watu wapende vya kwao zaidi ya hapo tutaishia kulaumu tu ni bora kila halimashauri ishughulikie swala la viwanja hapa tutakuwa tumeweza...
Viwanja vingi vya soka nchini Tanzania vilijengwa wakati wa mfumo wa chama kimoja. Ama vilijegwa na waasisi wa TANU na ASP kwa kuhamasisha wananchi mbalimbalia ambao kwa wakati huo walikuwa ni wanachama wa CCM maana ndicho kilikuwa chama pekee. Kutokana na kuwa waasisi wa TANU na ASP ndio waliotoa hamasa kwa wananchi wakiwa ndani ya serikali ya CCM chama pekee kwa wakati ule ilipelekea viwanja vingi kupewa majina yao ama ya maswala mbalimbali ya nchi.
Mfano: Sheikh Abeid Aman Karume-Arusha, Sokoine-Mbeya, Jamhuri-Morogoro, CCM Kirumba-Mwanza, Jamhuri-Dodoma, Mkwakwani Tanga. Hayo ni baadhi tu ya majina ya viwanja hivi. Sasa kinanchoshangaza ni jinsi SISIM ilivyoshadidia na kujimilikisha viwanja hivi baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza.
Kama mfumo wetu wa Siasa ungekuwa madhubuti basi viwanja hivi vingeuzwa na faida kugawiwa wananchi au vyama mbali mbali. Lakini kwa kuwa lengo la kuendeleza michezo si kuuza au kubomoa viwanja. Ilipasa basi baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza viwanja hivi vingerudiswa serikalini ama kugeuzwa kuwa vya manispaa!!!! CCM kuving'ang'ania huo ni Ufisadi!!!!
Ipo siku viwanja vyetu vitarudi....
Hapo hawawezi kuponda, watakuwa wezi jeuri.Subiria magamba waje kukuponda.......
kuna habari zinaenea kwa kasi kubwa nchi nzima kuwa asilimia karibu tisini ya viwanja vya michezo vinamilikiwa na chama cha mapinduzi CCM. Kiwanja kama CCM kilumba, kambarage (shinyanga), jamhuri (morogoro) ali hassan mwinyi, shekh amri abeid (Arusha) nangwanda sijaona (mtwara) na vingine vingi eti ni vya ccm. jambo la kujiuliza hapa ni kwamba CCM walijenga kwa rasilimali zao ama kwa kodi za wananchi wakati wa chama kimoja? Hapa watanzania tuwe makini sana watu wachache wasijilimbikizie mali za watanzania.