Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Kama kweli jk ni mpenda michezo arudishe viwanja hivi serikalini au avitoe kwa kampuni kama NHC ili iviboreshe na kuviendesha kwa ubora zaidi
 
mi naona ni kila halimashauri ya wilaya au mkoa ishughulikie hilo swala viwanja na hii itafanya watu wapende vya kwao zaidi ya hapo tutaishia kulaumu tu ni bora kila halimashauri ishughulikie swala la viwanja hapa tutakuwa tumeweza...

ni kweli bora vikabidhiwe kwa h.ya wilaya
 
Viwanja vingi vya soka nchini Tanzania vilijengwa wakati wa mfumo wa chama kimoja. Ama vilijegwa na waasisi wa TANU na ASP kwa kuhamasisha wananchi mbalimbalia ambao kwa wakati huo walikuwa ni wanachama wa CCM maana ndicho kilikuwa chama pekee. Kutokana na kuwa waasisi wa TANU na ASP ndio waliotoa hamasa kwa wananchi wakiwa ndani ya serikali ya CCM chama pekee kwa wakati ule ilipelekea viwanja vingi kupewa majina yao ama ya maswala mbalimbali ya nchi.

Mfano: Sheikh Abeid Aman Karume-Arusha, Sokoine-Mbeya, Jamhuri-Morogoro, CCM Kirumba-Mwanza, Jamhuri-Dodoma, Mkwakwani Tanga. Hayo ni baadhi tu ya majina ya viwanja hivi. Sasa kinanchoshangaza ni jinsi SISIM ilivyoshadidia na kujimilikisha viwanja hivi baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza.

Kama mfumo wetu wa Siasa ungekuwa madhubuti basi viwanja hivi vingeuzwa na faida kugawiwa wananchi au vyama mbali mbali. Lakini kwa kuwa lengo la kuendeleza michezo si kuuza au kubomoa viwanja. Ilipasa basi baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza viwanja hivi vingerudiswa serikalini ama kugeuzwa kuwa vya manispaa!!!! CCM kuving'ang'ania huo ni Ufisadi!!!!

Ipo siku viwanja vyetu vitarudi....
 
Viwanja vingi vya soka nchini Tanzania vilijengwa wakati wa mfumo wa chama kimoja. Ama vilijegwa na waasisi wa TANU na ASP kwa kuhamasisha wananchi mbalimbalia ambao kwa wakati huo walikuwa ni wanachama wa CCM maana ndicho kilikuwa chama pekee. Kutokana na kuwa waasisi wa TANU na ASP ndio waliotoa hamasa kwa wananchi wakiwa ndani ya serikali ya CCM chama pekee kwa wakati ule ilipelekea viwanja vingi kupewa majina yao ama ya maswala mbalimbali ya nchi.

Mfano: Sheikh Abeid Aman Karume-Arusha, Sokoine-Mbeya, Jamhuri-Morogoro, CCM Kirumba-Mwanza, Jamhuri-Dodoma, Mkwakwani Tanga. Hayo ni baadhi tu ya majina ya viwanja hivi. Sasa kinanchoshangaza ni jinsi SISIM ilivyoshadidia na kujimilikisha viwanja hivi baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza.

Kama mfumo wetu wa Siasa ungekuwa madhubuti basi viwanja hivi vingeuzwa na faida kugawiwa wananchi au vyama mbali mbali. Lakini kwa kuwa lengo la kuendeleza michezo si kuuza au kubomoa viwanja. Ilipasa basi baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza viwanja hivi vingerudiswa serikalini ama kugeuzwa kuwa vya manispaa!!!! CCM kuving'ang'ania huo ni Ufisadi!!!!

Ipo siku viwanja vyetu vitarudi....

Wala siyo siku nyingi ndugu , viwanja vile ni mali ya watz wote , hakuna asiyejua hilo .
 
Imeandikwa na Dk. Noordin Jella, BiharamuloJumanne, Machi 12, 2013 14:26
Tanzania ilikuwa nchi inayofuata mfumo wa chama kimoja hadi mwaka 1992, wakati nchi wahisani za magharibi ziliposhinikiza nchi zote duniani zinazoendelea, kuanzisha mfumo wa vyama vingi kama ishara ya kujenga misingi bora ya demokrasia kwa jamii.

Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilikuwa haihitaji sana mfumo wa vyama vingi, lakini kwa kuhofia kunyimwa misaada na nchi wahisani, ikabidi ikubali kuanzisha mfumo wa vyama vingi.

Lakini vyama vya upinzani havikuanzishwa kwa kufuata taratibu za uanzishwaji wa mfumo huo.

Hivyo, tukaanzisha vyama vya upinzani ambavyo havina sauti zaidi ya kupewa fursa ya kuhubiri majukwaani.

Wakati wa mfumo wa chama kimoja cha CCM tulikuwa tunasema chama kimeshika hatamu. Kwamba chama ndicho kinachoongoza Serikali, na kwa bahati mbaya tukaunganisha Serikali na chama kikawa kitu kimoja; kila ofisi ya Serikali kukawa na tawi la CCM na viongozi wa chama ndani ya wizara na idara mbalimbali za Serikali, ndiyo wakawa wabunifu na viongozi wakuu wa shughuli za Serikali.

Chama kikawa na sauti kwenye kila idara ya Serikali, kwa kupanga na kusimamia majukumu ya idara hizo bila kujali uwezo wa viongozi hao wa chama kitaaluma!

Wakati tumesema chama kimeshika hatamu pia tukasema pesa za chama hazifanyiwi ukaguzi wa mahesabu, na tunajua fika kwamba chama hakina biashara yoyote ile inayoweza kukiwezesha kupata mapato ya kujiendesha, bali kilikuwa kinategemea kupewa pesa ya walipakodi kutoka hazina!

Kwa utaratibu huu chama kikawa kimetoa mwanya wa ufisadi ndani ya chama chenyewe, kwenye idara za serikali na jamii kwa ujumla. Katika mazingira hayo ukawekwa utaratibu wa kuchukua pesa za walipakodi kutoka hazina na kuzipeleka kwenye chama kugharamia matumizi mbalimbali yakiwamo ya chama.

Kutokana na hali hiyo, kila mtu akawa anajitahidi ajiunge na chama na agombee uongozi wa ngazi ya juu ili aweze kupata mwanya wa kutumia fedha hizo.

Wakati chama kimeshika hatamu, kiliweza kuchukua pia baadhi ya mali za umma ambazo ni pamoja na majengo ya Serikali kwa ajili ya kuyafanyia shughuli mbalimbali za kichama, viwanja na mashamba kwa kutumia kigezo kwamba Serikali na chama ni kitu kimoja.

CCM pia kilichukua baadhi ya magari ya Serikali na kuyamiliki, na wakati mwingine ilichukua pesa hazina na kununua magari mapya kwa ajili ya chama. Ilichukua pia kiwanda cha uchapishaji cha KIUTA na kukifanya mali yake. Kiwanda hicho ndicho kilichokuwa kinamiliki magazeti ya Uhuru na Mzalendo.

Kuna baadhi ya mali za Serikali ambazo zilichukuliwa na chama, lakini zimeangukia mikononi mwa ‘wajanja’ wachache na wameshazifanya mali zao binafsi!

Mwaka 1992 nchi ilianza kufuata mfumo wa vyama vingi, lakini bado CCM imeendelea kushika hatamu kwa kuendelea kuvifanya baadhi ya vyombo vya dola kuwa kama idara ndani ya chama hicho, hivyo kuvifanya vyama vya upinzani kukosa nguvu nchini.

Mazingira kama haya yamevifanya vyama vya upinzani wakati mwingine vionekane kama si vyama halali kikatiba, na hivyo kuvifanya viwe dhaifu katika suala zima la kuthibitisha kuwapo kwao na kutetea maslahi ya umma.

Ndiyo maana pamoja na nchi kukumbwa na kashfa nyingi za ubadhirifu wa mali za umma, vyama vya upinzani havijaweza kukemea ufisadi ipasavyo. Matokeo yake baadhi ya rasilimali za nchi zinahujumiwa na watumishi wasio waadilifu. Pesa ya EPA imepotea hivi hivi. Kulikuwapo pia habari za twiga kusafirishwa mchana kweupe - tena kupitia kiwanja cha ndege cha kimataifa, kwamba eti wamepata soko huko Uarabuni.

Makontena ya pembe za tembo wa Tanzania yamekamatwa huko China na Vietnam, lakini wahusika hawajachukuliwa hatua zinazostahili. Wachina wamevuna magogo huko Lindi na Mtwara hadi wamepeleka mirunda ya miti adimu ya Mpingo makontena kwa makontena.

Vyama vya upinzani vimenyamaza kimya vinasubiri eti kwanza viingie madaraka ndipo vianze kuyashughulikia! Mtaingiaje madaraka wakati hamjatambuliwa ipasavyo? Sasa mtatumia miujiza gani mshinde uchaguzi?

Wakati tunaanzisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, siasa za kikomunisti zilikuwa zimeshakufa duniani, mwasisi wa mfumo huu wa vyama vingi alikuwa Mwalimu Nyerere pamoja na kwamba alikuwa ameshastaafu, lakini ilitokea tu tukajikuta yeye tena ndiye mwasisi wa mfumo huu.

Kiutaratibu alipaswa akivunje chama cha kikomunisti cha CCM na mali zote za chama hicho zirudishwe serikalini, ndipo sasa awaruhusu wanasiasa na wanaharakati kuunda mfumo wa vyama vingi, ili vyama vyote viwe na nguvu sawa na viwe na uwezo wa kutetea haki za wananchi na maslahi ya Taifa kwa ujumla.

Binafsi ninapendekeza kuwa katika kipindi hiki ambacho tunaitafuta Katiba mpya tuhakikishe kwamba tunakitenganisha chama tawala na Serikali, pia kuhakikisha CCM inarejesha mali ilizochukua kutoka serikalini na hazina na kuzirejesha serikalini.

Tukifanya hivyo, tutakuwa tumejenga mazingira mazuri ya demokrasia ya kweli hapa nchini, pia tutavipa nguvu vyama vya upinzani viweze kusimama imara na kutetea maslahi ya umma.

Mwandishi wa makala haya, Dk. Noordin Jella (PhD in Economics), ni Mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu Huria, Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa sasa ni Mwandishi wa Kujitegemea na Mchambuzi wa masuala ya siasa. Anapatikana kwa email: norjella@yahoo.com.
Simu: +255 782 000 131
 
Yeah... Siku zake ni 40; Kina NAPE na MWINGULU wataanza kutembea kwa MIGUU na kupanda DALADALA kwanza wameifanya CCM chama cha KIBEPARI kisichojali wananchi walio wengi; Wao Matumbo yanajitokeza... Wanazaa na Wanawake Mbalimbali hakuna SHIDA pesa za CHAMA ziko...
 
Sahihi kabisa. kosa lililofanyika awali kabisa ni kutobadilisha katiba kipindi kile cha 1992 kuelekea 1995. Mapendekezo yaliyotolewa na mjumbe ni mazuri lakini time and space ndio swala la msingi. tuwaulize kwanza viongozi wa upinzani wana msimamo gani kuhusiana na masuala kama haya.
Asante
 
Wakati mfumo wa chama kimoja haikuwa rahisi kujua miradi ya umma na ya chama. Miradi iliyoanzishwa kwa ajili ya chama ilikuwa na dhumuni moja: kuhamasisha sera ya chama kimoja. Ndio maana ulikuwa ukichaguliwa mwenyekiti wa chama mkoa, ukuu wa mkoa unakuja automatic.

Tulipobadili mfumo na kuingia mfumo wa vyama vingi miradi iliyojengwa kwa ajili ya chama lakini kimsingi ni ya umma ilibaki kuwa ya chama.

Mfano viwanja vya mpira na ofisi za uongozi kama mkuu wa mkoa. Kulikuwa hakuna haja ya kujenga viwanja viwili sehemu moja yani cha chama na serikali, kulikuwa hakuna haja ya kujenga ofisi ya mkuu wa mkoa na mwenyekiti wa mkoa wa chama: ilikuwa ni kitu kimoja.

Wazo langu ni kwamba miradi mikubwa kama viwanja virudishwe viwe mali ya umma, haiwezekani mikoa yote viwanja viwe vya CCM, viwanja viwe mali ya umma chini ya halmashauri za mikoa.

Ofisi wanaweza kuchukua lakini si viwanja. Wengi mtakuwa mnafahamu baada ya mfumo wa vyama vingi katibu wa CCM wilaya alikuwa na ofisi kuliko mkuu wa mkoa.

Tuige KENYA: baada ya kibaki kuingia madarakani aliuchukua ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jomo Kenyatta toka KANU. Alisema ni mali ya wakenya, ni jasho la wakenya chini ya mfumo wa lazima wa chama kimoja
 
Hii itawezekana hadi hapo watakapo chukua nchi watu wengine.
 
Mkuu madiwani wa moshi walijaribu ccm wakakimbilia mahakamani mkuu
soma hapa hii habri iliandikwa tarehe 3 april 2011 Vuta ni kuvute baina ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi juu ya viwanja viwili vinavyotumiwa na CCM imeendelea kugonganisha pande zote katika Manispaa ya Moshi.

Mvutano huo kwa sasa umeifanya Chadema mkoani Kilimanjaro kutoa muda wa siku 30 kwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bernadetta Kinabo, na Katibu wa CCM mkoa, Steven Kazidi, kufuta kauli zao za kusema kuwa chama hicho kinafanya uchochezi na kina haja ya kumwaga damu, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mwenyekiti wa Chadema mkoani hapa na Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, alitoa kauli hiyo jana katika tamko la chama hicho lililotolewa mbele ya waandishi wa habari na madiwani wa Chadema wa Manispaa hiyo.

Kabla ya Mbunge huyo kutoa tamko hilo, Katibu wa Chadema mkoani hapa, Basil Lema, alitoa tamko la chama la kulaani kauli zilizotolewa na viongozi hao za kudai kuwa chama hicho kimejipanga kupeleka wananchi 50 kwa kila diwani siku ya Baraza la madiwani kwa ajili yakufanya vurugu, jambo ambalo si kweli.

Alisema Mkurugenzi huyo alidai kuwa chama hicho kupitia madiwani wake wamejipanga kufanya vurugu na kuharibu majengo na mali za Halmashauri ya Manispaa na kwamba mali hizo ndio wanazozisimamia iweje waziharibu. "Napenda kutamka kwa maneno ya masikitiko yangu kwake kwa namna alivyoonyesha na anavyoonyesha dharau ya wazi kwa mstahiki Meya, Michael Jaffary na madiwani wa Manispaa, kwa hakika lazima kuna mtu yuko nyuma yake katika kutekeleza dharau hii, haiwezekani kiburi hiki kikakosa mizizi mirefu kutoka katika mfumo wa utawala wa nchi," alisema Lema.


CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
katika ustaarabu wa kawaida ktk siasa ilipaswa iwe hivyo. Mali zote zilizotokana na jasho la Watanzania wote wakati wa chama kimoja, zingerudishwa ktk Halmashauri za miji ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote.

Ila CCM kwa ubabe na kutojitambua kuwa kila jambo ktk dunia hii liko subject ktk kubadilika, hawawezi kabisa kuachia mali hizo pamoja na kwamba serikali ni ya CCM.

Wangekuwa waungwana wangeachia vitu vingine vinavyowahusu watanzania wote bila kujali itikadi kuondoa mvutano usio wa lazima.
 
Kuna habari zinaenea kwa kasi kubwa nchi nzima kuwa asilimia karibu tisini ya viwanja vya michezo vinamilikiwa na chama cha mapinduzi CCM.

Kiwanja kama CCM kilumba, kambarage (shinyanga), jamhuri (morogoro) ali hassan mwinyi, shekh amri abeid (Arusha) nangwanda sijaona (mtwara) na vingine vingi eti ni vya ccm.

Jambo la kujiuliza hapa ni kwamba CCM walijenga kwa rasilimali zao ama kwa kodi za wananchi wakati wa chama kimoja? Hapa watanzania tuwe makini sana watu wachache wasijilimbikizie mali za watanzania.
 
Tutawanyang'anya tu subiri tuwatimue madarakani
 
kuna habari zinaenea kwa kasi kubwa nchi nzima kuwa asilimia karibu tisini ya viwanja vya michezo vinamilikiwa na chama cha mapinduzi CCM. Kiwanja kama CCM kilumba, kambarage (shinyanga), jamhuri (morogoro) ali hassan mwinyi, shekh amri abeid (Arusha) nangwanda sijaona (mtwara) na vingine vingi eti ni vya ccm. jambo la kujiuliza hapa ni kwamba CCM walijenga kwa rasilimali zao ama kwa kodi za wananchi wakati wa chama kimoja? Hapa watanzania tuwe makini sana watu wachache wasijilimbikizie mali za watanzania.

Umesahau MAJIMAJI; Songea; SOKOINE; Mbeya; KATAVI; Rukwa... walikuwa wanacota pesa kwa kukata kwenye mishahara na wafanyabiashara kodi mara mbili... kwahiyo sio vyao

Itakuwa kama KANU... walijipa KASARANI; KENYATTA CONFERENCE CENTER lakini walishindwa kutetea Mahakamani walipoanguka Madarakani...
 
Kikubwa nani mwenye hati miliki, Hivi kuna mtu anajua hati miliki ya mipaka ya Tanganyika anayo mjerumani maana ndiye aliyepima ramani 1884 na haijabatilishwa
 
Back
Top Bottom