Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
mkuu unajua hakuna garantii ya kuwatoa hawa jamaa hivi karibuni. inabidi tuanze kudai sasa hata kwa nguvu ya wananchi. wanavyozidi kuhodhi mali wanakuwa na incentives za kung'ang'ania madarakani hivyo kuwa ngumu kuwatoa. mambo mengine hayatakiwi kusubiri jamaa wang'oke.Hili suala ni gumu ccm wakiwa bado madarakani. Wameharibu mpaka kwenye mahakama kwa kuweka watu wao. Kuna majaji wamepewa kiushikaji na wanajua hawastahili. Kwa hiyo hili suala mahakamani lina nafasi ndogo sana. Ndio maana Kenya walisafisha mahakama baada ya kupata katiba mpya. Ilikuwa sehemu ya kutekeleza katiba hiyo.
Nikirudi kwenye maada, tusubiri ccm ing'olewe ndio tuanzishe huu mjadala. Viwanja vyote ccm Kirumba, Sokoine Mbeya, Majimajo Songea nk vimilikishe kwa halmashauri husika maana ni mali za wananchi wote. Viwanja vilijengwa wakati wa chama kimoja na rasilimali nyingi za serikali zilitumika.