Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Hili suala ni gumu ccm wakiwa bado madarakani. Wameharibu mpaka kwenye mahakama kwa kuweka watu wao. Kuna majaji wamepewa kiushikaji na wanajua hawastahili. Kwa hiyo hili suala mahakamani lina nafasi ndogo sana. Ndio maana Kenya walisafisha mahakama baada ya kupata katiba mpya. Ilikuwa sehemu ya kutekeleza katiba hiyo.

Nikirudi kwenye maada, tusubiri ccm ing'olewe ndio tuanzishe huu mjadala. Viwanja vyote ccm Kirumba, Sokoine Mbeya, Majimajo Songea nk vimilikishe kwa halmashauri husika maana ni mali za wananchi wote. Viwanja vilijengwa wakati wa chama kimoja na rasilimali nyingi za serikali zilitumika.
mkuu unajua hakuna garantii ya kuwatoa hawa jamaa hivi karibuni. inabidi tuanze kudai sasa hata kwa nguvu ya wananchi. wanavyozidi kuhodhi mali wanakuwa na incentives za kung'ang'ania madarakani hivyo kuwa ngumu kuwatoa. mambo mengine hayatakiwi kusubiri jamaa wang'oke.
 
Basi ingefaa uwanja mmojawapo utumike kama case study mahakamani tuone itakuwa vipi. Ushahidi ukusanywe jinsi uwanja ulivyojengwa kwa nguvu za wananchi wote. Wakati mwingine vinjwaji viliongezwa bei kukusanya fedha za ujenzi. Hiyo ni sawa na kodi kwa watu wote. Nani alianzishe?
 
ningependa mbunge wa mbeya mjini Sugu alianzishe. anaonekana kama anaweza kashkashi na anasupport kubwa ya wananchi.
 
Kuna viwanja kama sokoine Mbeya na Kirumba Mwanza. Hivi viwanja vilijengwa wakati wa chama kimoja na wananchi wote. Vilipokuja vyama vingi wengine wakatoka CCM na walipaswa kupata mgawo wa mali hiyo. Pia wengi walioshiriki ujenzi hawakuwa hata na kadi. Ni wakati wa hawa jamaa kurudisha mali kwa wananchi.

Pia kuna shule za wazazi na viwanja vya sabasaba. KAMA KUNA MALI YA WANANCHI AMBAYO UNAJUA CCM WANAJIMILIKISHA ITAJE HAPA
Sawa,sasa warudishiwe wananchi wa CCM ama CHADEMA?
 
ningependa mbunge wa mbeya mjini Sugu alianzishe. anaonekana kama anaweza kashkashi na anasupport kubwa ya wananchi.

Inabidi asaidiwe na wana sheria hasa katika kukusanya ushahidi muhimu na kupata watu wa kwenda kutoa ushahidi mahakamani.
Kwa mfano, kuna receipt za ongezeko la bei wakati huo kwenye vinywaji au za kuwasilisha fedha hizo
Barua au kumbukumbu zozote za kuwataka wananchi kwenda kwenye ujenzi huo
Umiliki wa maeneo hayo kabla ccm hawajayatwa - je walinunua hivyo viwanja?

Hizo taarifa muhimu zikiwekwa sawa, ni rahisi kushinda. Baadaye kutumia ushindi wa kimojawapo kwenye viwanja vingine.
 
ushahidi ndiyo muhimu kuliko vyote. hawa jamaa kama walivyo wanyonyaji wengine hawawezi kwenda chini kirahisi. watakuja na hati, barua kwa wanachama kuhimiza ujenzi na mambo kedekede, haitakuwa rahisi.
 
viwanja sio hivyo tu viwanja vyote vilivyopo mikoani na wilaya asilimia kubwa ccm wamijimilikisha bila uhalali wowote, haitaji hata kuwa na ushahidi mwingi wa makaratasi, viwanja hivyo vilijengwa kipindi cha chama kimoja serikali moja, ilipaswa tulipo ingia mfumo wa vyama vingi 1992 mali zote ambazo zilikuwa zinamilikiwa na ccm Enzi za chama kimoja serikali moja zirudi serikalini, bahati mbaya hilo halikufanyika
 
kama hayakufanywa enzi za Nyerere na akiwa hai alipong`atuka.....basi mpaka waingie upinzani...
 
Hi viwanja vinge baki kuwa vina milikiwa na Manispaa
Mwenge walikubali kurudisha serikalini.Kutorudisha viwanja ni hila, tena baadhi ya maeneo wamelazimisha kujimilikisha!
Had hi ya nchi kimichezo imeporomoka kwa sababu viwanja havitunzwi na kutumika kwa utaratibu unaojenga Sera ya michezo ya nchi.
Kulazimishwa warejeshe Kwenye halmashauri za maeneo husika ndio ufumbuzi wa kudumu.
Hili suala lipelekwe kwa msajili wa vyama.il I kuondoa katika Mali zinazomilikiwa name C CM.
 
kama hayakufanywa enzi za Nyerere na akiwa hai alipong`atuka.....basi mpaka waingie upinzani...

Kwa bahati mbaya zaidi hivyo viwanja vilichukuliwa enzi zake.
 
kama hayakufanywa enzi za Nyerere na akiwa hai alipong`atuka.....basi mpaka waingie upinzani...
kama kisheria wananchi wanahaki basi hata leo inawezekana. Nyerere mwaka 1992 hakuwa na nguvu sana hata kama angetaka viwanja virudishwe angewezashindwa.
 
viwanja sio hivyo tu viwanja vyote vilivyopo mikoani na wilaya asilimia kubwa ccm wamijimilikisha bila uhalali wowote, haitaji hata kuwa na ushahidi mwingi wa makaratasi, viwanja hivyo vilijengwa kipindi cha chama kimoja serikali moja, ilipaswa tulipo ingia mfumo wa vyama vingi 1992 mali zote ambazo zilikuwa zinamilikiwa na ccm Enzi za chama kimoja serikali moja zirudi serikalini, bahati mbaya hilo halikufanyika

kwan vinatumiwa na wana ccm peke yao?
 
Back
Top Bottom