Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

kama kisheria wananchi wanahaki basi hata leo inawezekana. Nyerere mwaka 1992 hakuwa na nguvu sana hata kama angetaka viwanja virudishwe angewezashindwa.

bado ushawishi alikuwa nao,KWA WATU WA MAKTABA...je hakuna hotuba yake,maandiko/mahojiano alipowahi kuliongelea hili?nini ulikuwa msimamo wake?...
 
bado ushawishi alikuwa nao,KWA WATU WA MAKTABA...je hakuna hotuba yake,maandiko/mahojiano alipowahi kuliongelea hili?nini ulikuwa msimamo wake?...

Tyta ndugu umefilisika siku hizi nini...idara ya pichanaona umebinafsisha
 
Ndio maana viwanja vyenyewe vibovu kumbe wanavimiliki hawa wakoloni wa kijani
 
Kuna viwanja kama sokoine Mbeya na Kirumba Mwanza. Hivi viwanja vilijengwa wakati wa chama kimoja na wananchi wote. Vilipokuja vyama vingi wengine wakatoka CCM na walipaswa kupata mgawo wa mali hiyo. Pia wengi walioshiriki ujenzi hawakuwa hata na kadi. Ni wakati wa hawa jamaa kurudisha mali kwa wananchi.

Pia kuna shule za wazazi na viwanja vya sabasaba. KAMA KUNA MALI YA WANANCHI AMBAYO UNAJUA CCM WANAJIMILIKISHA ITAJE HAPA

nyie ndiyo maana hamuaminiki kupewa nchi. badala ya kumwaga sera zenu mnakalia kuwaza mali za ccm. Mbona hamuulizi mashamba ya kahawa ya mwasisi wa cdm, mzee ... pale USA river Arusha
 
bado ushawishi alikuwa nao,KWA WATU WA MAKTABA...je hakuna hotuba yake,maandiko/mahojiano alipowahi kuliongelea hili?nini ulikuwa msimamo wake?...

Akizungumza na waandishi wa habari mwaka 1999, Mwalimu Nyerere alisema bado alikuwa hajaona kasoro ya Azimio la Arusha. “Mimi bado natembea nalo (Azimio la Arusha). Nalisoma tena na tena kugundua kama kuna cha kubadili. Labda ningeboresha Kiswahili nilichokitumia, lakini Azimio lenyewe bado ni thabiti. Nisingebadili hata neno moja,” anasema Mwalimu Nyerere.
KUFA AZIMIO LA ARUSHA:Nyerere alivyotofautiana na Mwinyi - Makala - mwananchi.co.tz

bado ushawishi alikuwa nao,KWA WATU WA MAKTABA...je hakuna hotuba yake,maandiko/mahojiano alipowahi kuliongelea hili?nini ulikuwa msimamo wake?...
alitaka kuzuia NBC isiuzwe ila alishindwa. lakini huyu naye kuna mambo mengi sana aliikosea hivyo hatuwezi kumchukulia kama msingi kwenye kila maamuzi tunayofanya.
 
nyie ndiyo maana hamuaminiki kupewa nchi. badala ya kumwaga sera zenu mnakalia kuwaza mali za ccm. Mbona hamuulizi mashamba ya kahawa ya mwasisi wa cdm, mzee ... pale USA river Arusha

kwanza hizo siyo mali za ccm. pili, kuna shida gani kumiliki shamba la kahawa?
 
Alafu hao hao ccm wameuza open space kwa kiwango kikubwa,
UWanja wa biafra ccm wameuharibu watakuwa kwenye mkakati wa kuuza tu
 
Alafu hao hao ccm wameuza open space kwa kiwango kikubwa,
UWanja wa biafra ccm wameuharibu watakuwa kwenye mkakati wa kuuza tu

Chadema wanapata ruzuku ya milioni 200 kila mwezi wanashindwa kununua nyumba ya ofisi..wanabanana tu pale kwa kuwa nyumba ni ya mtei kodi milioni 10 kwa mwezi wanalipa ya mwaka! Wapigaji watupu
 
Chadema wanapata ruzuku ya milioni 200 kila mwezi wanashindwa kununua nyumba ya ofisi..wanabanana tu pale kwa kuwa nyumba ni ya mtei kodi milioni 10 kwa mwezi wanalipa ya mwaka! Wapigaji watupu
unamaoni gani kuhusu viwanja vya michezo ambavyo ccm wamejimilikisha?
 
Kuna viwanja kama sokoine Mbeya na Kirumba Mwanza. Hivi viwanja vilijengwa wakati wa chama kimoja na wananchi wote. Vilipokuja vyama vingi wengine wakatoka CCM na walipaswa kupata mgawo wa mali hiyo. Pia wengi walioshiriki ujenzi hawakuwa hata na kadi. Ni wakati wa hawa jamaa kurudisha mali kwa wananchi.

Pia kuna shule za wazazi na viwanja vya sabasaba. KAMA KUNA MALI YA WANANCHI AMBAYO UNAJUA CCM WANAJIMILIKISHA ITAJE HAPA

Bila mabadiliko kutokea, ni ngumu sana. Hawa jamaa ni wezi sana wanatuibia wananchi. Badala iwe mali ya serikali, wamejimilikisha wao hasa viongozi maana hata wanaojiita wanachama wa CCM, hawambulii kitu. Vinawanufaisha wachache tu. Nawapa pole hata hao mashabiki wao, wanakalia kuwapigia mafisadi debe, huku wao hata kandambili hawana. Shame on them
 
wanatunyonya hasa. hivi viwanja vya sabasaba dar nani mmiliki?
 
Tena Dar es salaam ndo kuna vi-open space kibao vinavyotambulika kama vya CCM na biashara ya parking zinafanywa kwenye hizo open spaces bila hata ya kulipa kodi. Undani wa umiliki wa hivi viwanja wanaujua wenyewe CCM.
 
Subiri serikali huru ijayo kitaeleweka tu, kipi ni mali ya serikali na kipi ni mali za ccm.
 
Ccm was#@/ sana yaani hawajui umuhimu wa open space, sehemu hizo watoto ndy wangekuwa wanaenda kucheza lakini mpaka sasa watoto hawana pakwenda badala yake wanacheza sehemu sizo sehemu ambazo ni hatari
 
CAF imeipa Tanzania uenyeji wa kuandaa faniali za michuano ya Mpira wa Miguu chini ya miaka 17 mwaka 2019. Tunashukuru kwa nafasi tuliyopewa nadhani itakuwa njia nyingine ya kuupeleka mpira wetu kule ambako wenzetu wako.

Unaweza ukaona 2019 kama ni mbali sana, lakini kwa maandalizi ni miaka michache sana. Pamoja na kuindaa timu yetu, maandalizi ya viwanja pia huwa ni sehemu ya michuano hii kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Tunajua viwanja vya michezo vingi hapa nchini vilijengwa kwa nguvu za wananchi wakati wa mfumo wa chama kimoja.. Kwa kipindi kile ilikuwa ngumu kutofautisha kati ya Mali ya Chama na Mali ya Umma.. Bahati mbaya baada ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi CCM ilijimilikisha viwanja hivi kienyeji..

kuanzia CCM Kirumba, Jamhuri Dodoma na Morogoro, Mkwakwani Tanga, Sokoine Mbeya na vingine vingi..

Ni muda mwafaka sasa CCM ikarudisha viwanja hivi Serikalini ili viweze kuhudumiwa na kufanyiwa ukarabati mkubwa kwa ajili ya maandalizi ya fainali hizi za vijana.!!

CHONDE CHONDE CCM rudisheni viwanja vyetu ili viweze kuhudumiwa na Serikali kwa manufaa ya michuzo Tanzania!!
 
Back
Top Bottom