Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Ni aibu kwa taifa kama hili eti viwanja vya mipira kila mkoa ni vya ccm
nashindwa kuelewa ni kwanini je hivi viwanja pesa ya kujengwa ilitoka mifukoni mwa ccm kweli...?
yani serikali viwanja vyao ni kama vipi tukitoa cha dar.......?

jamani naomba nijuzwe
 
Kwani ni nini cha ajabu hapo!? Mimi sishangazwi kabisa, Kwa nchi inayoongozwa na viongozi vilaza wasio na mipango wala uadilifu hili ni suala la kawaida kabisa. By the way wewe ulitegemea nini cha zaidi kutoka CCM!?
 
Chama Cha Mapinduzi, chama-dola, ni chama chenye nguvu zaidi hapa nchini. CCM wanamiliki angalau kiwanja kimoja cha michezo karibu kila mkoa. Viwanja hivi vimekuwa vikitumika hasa kwa ajili ya michezo ya ligi kuu ya soka. Ila tatizo ni hali ya viwanja hivyo, kuanzia kwenye majukwaa, mpaka vyooni, mpaka sehemu yenyewe ya kusakata. Kuna haja ya CCM kuwa 'serious' kibiashara kuzingatia ukweli kwamba ligi imechangamka. Kama hawataweza basi watafute wabia na wafanye maendeleo ya maeneo hayo ili yavutie. Kuna jamaa alinambia pale Mtwara CCM walikataa offer ya kuboresha Nangwanda Stadium, sijui waliona nini. Ila ni wazi kwamba CCM wana nafasi ya kuwa mafanikio makubwa kibiashara kama wakiamua kuyaendeleza maeneo hayo.
 
Chumba cha kupumzikia wachezaji kwny uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Mjini Tabora wamemkodisha bibi mwny Nursery School pale kuchemshia uji wa watoto ( wanafunzi) Asubuhi. Huyu Bibi nae sijui tumwite mbia au is?
 
Hivi viwanja navyo ni majipu yanayotakiwa kutumbuliwa. Please MAGU, virudishe viwanja hivi ili viwe chini ya halmashauri kama nchi za wenzetu wanavyofanya ili vipangiwe bajeti ya matunzo! Mfano jana kiwanja cha kirumba nilivyokiona simba ikicheza na toto ni aibu kubwa uwanja huo!
 
Chumba cha kupumzikia wachezaji kwny uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Mjini Tabora wamemkodisha bibi mwny Nursery School pale kuchemshia uji wa watoto ( wanafunzi) Asubuhi. Huyu Bibi nae sijui tumwite mbia au is?

hahaha!!! hivi viwanja vinadhalilisha soka.
 
CCM wasipofanya haraka kurekebisah hali ya mambo ktk viwanja vyao, tutawatangaza rasmi kuwa adui namba moja wa maendeleo ya michezo nchini hususani mpira wa miguu. Hali kama ile ya CCM Kirumba Mwanza jana kati ya Toto na Simba inatia aibu na kinyaa.
 
Nimekuwa nikijiuliza siku nyingi kuhusu hivi viwanja vya michezo hususan vya mpira wa miguu ambavyo viko chini ya CCM ( chama cha mapinduzi). Nijuavyo viwanja hivi vilijengwa enzi za chama kimoja na madhumuni ya kujengwa ilikuwa ni kuimarisha michezo kwa kila mkoa. Mifano ni; CCM KIRUMBA jijini MWANZA, CCM manispaa ya MUSOMA nk. Baada ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi viwanja karibu zote bado ni mali ya CCM.
Sawli langu ni, CCM wanachangia kiasi gani cha kodi kulipia katika Halmashauri ambamo viwanja hivi vipo? Na je TRA kama wakala wa serikali wa kukusanya pato la taifa wana rekodi gani ya CCM kulipia kutokana makusanyo wakati wa tafrija au mechi zinazochezwa katika viwanja hivi? Kama kati ya hayo maswali 2, hakuna jibu ni kwa nini visbinafsishwe kuwa mali ya umma? Swali la 3 ni kwa nini hivi viwanja haviendelelezwi?
 
CCM imepora mali ya wanainchi kupitia transformation ya kutoka chama kimoja na kwenda vyama vingi, hata hivyo bado haki itapatikana wanainchi watakapofunguka macho
 
Hapo kwenye kodi nadhani ni Jipu sijawai kusikia viwanja vya mikoani vikitajwa kulipa kodi zaidi ya Timu za mpira wa miguu kulipishwa kodi. Hilo ni jipu
 
Ili kuziongezea halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji ni halali kabisa zimilikishwe viwanja vyote vya michezo vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi nchi nzima . Viwanja hivi vilijengwa kwa wananchi kukatwa mishahara na wafanyabiashara kulipishwa viwango vilivyopangwa pia bei za bia, soda, kanga na vitenge kuongozwa. Hayo yalifanyika wakati wa awamu za kwanza na za pili za serikali ya chama kimoja. Kwa hiyo ccm wakubali kuviachia ili viwe kwa manufaa wananchi wote. Halmashauri zenye viwanja hivyo pitisheni maazimio ili Mhe Rais afute hati zilizoko na kuwamilikisheni.
 
Hoja yako ni ya msingi, naunga mkono. Lakini je huyu wa CCM ndo afute hati miliki za viwanja vyake?
 
Hoja ya msingi ni kuwa ccm hawakuvijenga na kuwa wananchi wote bila ubaguzi wanayo haki ya kufaidI jasho lao. Kwa hiyo mabaraza ya madiwani wapitishe maazimio ya kubadili miliki na kumpelekea rais. Hapo tutadhibitIsha kauli yake kuwa yeye ni Rais wetu wote na siyo wa ccm. Madiwani na wabunge wa ccm msiwe wabinafsi katika hoja kama hizi.
 
Nimekuwa najiuliza Viwanja vya michezo vilivyopo mikoani ni vya nani?Jibu nililopata in viwanja vya Chama cha Mapinduzi CCM.

Bado nikazidi kujiuliza no lini CCM ilivijenga Na wakandarasi gani waliotumiwa Kwa majina kuvijenga? Jibu ni watanzania wakulima, wafanyabiashara Na watumishi wa Serikali Na mashirika ya umma.Kwa mfano, Mimi mwaka 1985 nilikuwa mjini sumbawanga kama mtumishi wa serikali ofisi ya MKUU wa mkoa wa Rukwa.

Mkuu wa mkoa alikuwa Meja jenerali Tumainiel kiwelu.Mkuu huyu ndiye aliyetoa wazo la kuujenga uwanja unaoitwa "Nelson Mandela".
Mkuu huyu aliagiza kila mtanzania aliopo mkoani Rukwa Kwa maana ya wilaya zake lazima ashirika ktk ujenzi huo .

Wilaya zilichangisha wananchi wakulima wafugaji watumishi wafanyabiashara n.k michango yote ilipokelewa Na ofisi ya MKUU wa mkoa Kwa udhibiti.

Baada ya hiyo michango ambayo ilikuwa endelevu ikiwa in pamoja Na nyongeza ya bei kwenye bidhaa kama soda via Na mafuta.Ujenzi wa uwanja ulianza Kwa kushirikisha makampuni yote ya ukandarasi yaliyopo mkoa wa Rukwa Na mikoa ya jirani.

Pia aliwaleta wakimbizi wa Burundi waliokuwa kwenye kambi iliyopo katumba mpanda kwani wajenzi wazuri ambao waliweka kambi ndani ya majengo ya Idara ya ujenzi mjini sumbawanga.

Watumishi walikuwa wanashiriki kusogeza Tofari Kwa kila Idara hata watumishi wa afya manesi walishiriki mpaka ujenzi ulipokamilika Na kuitwa "Nelson Mandela Stadium.Pongezi Kwa Mzee wetu shujaa wa Uwanja wa Nelson Mandela Mzee Kiwelu.

Swali lang kubwa ni kwamba uwanja asilimia 100 umejengwa Kwa nguvu za wananchi iweje Leo uwanja huo uwe Mali ya CCM? Na kuwa Mali ya CCM watanzania wengine wananyimwa fursa ya kuutumia wakati uwanja ulijengwa Na watu wote bila kujali itikadi.

Mbona uwanja wa taiga mpya Na wa zamani CCM haijimilikishi?Tunaomba wadau tulisemee hili viwanja ambavyo CCM ilivitafuta ikachoresha Ramani ikafyatua Tofari Na kutangaza kandarasi viwe vya CCM lakini viwanja ambavyo watanzania wote wamevuja jasho viwe vya serikali kama Viwanja vya Taifa ili vyama vyetu vyote viweze kuvitumia bila ukiritiba wa CCM.
 
Hii ishu napinga kabisa, viwanja vyote hivyo ni mali ya umma. Vinatakiwa viwe chini ya halmashauri na manispaa.
Kwa sababu vilijengwa chini ya utawala wa chama kimoja haimaanishi ni vya ccm, ndio maana vingine vinaharibika sababu havipati matunzo.
Utafutwe utaratibu vinyang'anywe na viitwe majina ya mikoa vilipo.
 
ccm haikuwahi kujenga viwanja hivyo; viwanja karibu nchi nzima vilijengwa kwa mtindo huo huo wa Rukwa, kilichofanyika ni Ccm; true to type; walivikwapua wakajimilikisha, sasa huko tuendako hili swala litakuja kukaa sawa kama kule kenya ambako Chama mfu cha huko; KANU, kilijimilikisha jengo la mikutano KICC lakini baada ya NARC chini ya Kibaki kuchukua nchi walilirejesha mikononi mwa umma. Ni swala la wakati tu!
 
Ukweli usiokuwa na shaka viwanja vyote ni vya umma kama ilivyo kwa shule za TAPA, ingawa ukweli ndio huo lakini hivi sasa CCM wamevaa miwani ya mbao pamoja na kwamba vimewashinda kuviendeleza viwanja na shule zao za TAPA walizotaifisha au walizotuzulumu lakini tushukuru kwani baadae wanainchi wataona kuwa shule na viwanja haviwasaidii bali ni tamaa na uroho wa CCM usiojali jamii husika
 
Nimekuwa najiuliza Viwanja vya michezo vilivyopo mikoani ni vya nani?Jibu nililopata in viwanja vya Chama cha Mapinduzi CCM.

Bado nikazidi kujiuliza no lini CCM ilivijenga Na wakandarasi gani waliotumiwa Kwa majina kuvijenga? Jibu ni watanzania wakulima, wafanyabiashara Na watumishi wa Serikali Na mashirika ya umma.Kwa mfano, Mimi mwaka 1985 nilikuwa mjini sumbawanga kama mtumishi wa serikali ofisi ya MKUU wa mkoa wa Rukwa.

Mkuu wa mkoa alikuwa Meja jenerali Tumainiel kiwelu.Mkuu huyu ndiye aliyetoa wazo la kuujenga uwanja unaoitwa "Nelson Mandela".
Mkuu huyu aliagiza kila mtanzania aliopo mkoani Rukwa Kwa maana ya wilaya zake lazima ashirika ktk ujenzi huo .

Wilaya zilichangisha wananchi wakulima wafugaji watumishi wafanyabiashara n.k michango yote ilipokelewa Na ofisi ya MKUU wa mkoa Kwa udhibiti.

Baada ya hiyo michango ambayo ilikuwa endelevu ikiwa in pamoja Na nyongeza ya bei kwenye bidhaa kama soda via Na mafuta.Ujenzi wa uwanja ulianza Kwa kushirikisha makampuni yote ya ukandarasi yaliyopo mkoa wa Rukwa Na mikoa ya jirani.

Pia aliwaleta wakimbizi wa Burundi waliokuwa kwenye kambi iliyopo katumba mpanda kwani wajenzi wazuri ambao waliweka kambi ndani ya majengo ya Idara ya ujenzi mjini sumbawanga.

Watumishi walikuwa wanashiriki kusogeza Tofari Kwa kila Idara hata watumishi wa afya manesi walishiriki mpaka ujenzi ulipokamilika Na kuitwa "Nelson Mandela Stadium.Pongezi Kwa Mzee wetu shujaa wa Uwanja wa Nelson Mandela Mzee Kiwelu.

Swali lang kubwa ni kwamba uwanja asilimia 100 umejengwa Kwa nguvu za wananchi iweje Leo uwanja huo uwe Mali ya CCM? Na kuwa Mali ya CCM watanzania wengine wananyimwa fursa ya kuutumia wakati uwanja ulijengwa Na watu wote bila kujali itikadi.

Mbona uwanja wa taiga mpya Na wa zamani CCM haijimilikishi?Tunaomba wadau tulisemee hili viwanja ambavyo CCM ilivitafuta ikachoresha Ramani ikafyatua Tofari Na kutangaza kandarasi viwe vya CCM lakini viwanja ambavyo watanzania wote wamevuja jasho viwe vya serikali kama Viwanja vya Taifa ili vyama vyetu vyote viweze kuvitumia bila ukiritiba wa CCM.
Hivyo viwanja vilipaswa kuwa vya halmashauri
 
Hii ishu napinga kabisa, viwanja vyote hivyo ni mali ya umma. Vinatakiwa viwe chini ya halmashauri na manispaa.
Kwa sababu vilijengwa chini ya utawala wa chama kimoja haimaanishi ni vya ccm, ndio maana vingine vinaharibika sababu havipati matunzo.
Utafutwe utaratibu vinyang'anywe na viitwe majina ya mikoa vilipo.

Leo nakuunga mkono upo sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom