Nimekuwa najiuliza Viwanja vya michezo vilivyopo mikoani ni vya nani?Jibu nililopata in viwanja vya Chama cha Mapinduzi CCM.
Bado nikazidi kujiuliza no lini CCM ilivijenga Na wakandarasi gani waliotumiwa Kwa majina kuvijenga? Jibu ni watanzania wakulima, wafanyabiashara Na watumishi wa Serikali Na mashirika ya umma.Kwa mfano, Mimi mwaka 1985 nilikuwa mjini sumbawanga kama mtumishi wa serikali ofisi ya MKUU wa mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa mkoa alikuwa Meja jenerali Tumainiel kiwelu.Mkuu huyu ndiye aliyetoa wazo la kuujenga uwanja unaoitwa "Nelson Mandela".
Mkuu huyu aliagiza kila mtanzania aliopo mkoani Rukwa Kwa maana ya wilaya zake lazima ashirika ktk ujenzi huo .
Wilaya zilichangisha wananchi wakulima wafugaji watumishi wafanyabiashara n.k michango yote ilipokelewa Na ofisi ya MKUU wa mkoa Kwa udhibiti.
Baada ya hiyo michango ambayo ilikuwa endelevu ikiwa in pamoja Na nyongeza ya bei kwenye bidhaa kama soda via Na mafuta.Ujenzi wa uwanja ulianza Kwa kushirikisha makampuni yote ya ukandarasi yaliyopo mkoa wa Rukwa Na mikoa ya jirani.
Pia aliwaleta wakimbizi wa Burundi waliokuwa kwenye kambi iliyopo katumba mpanda kwani wajenzi wazuri ambao waliweka kambi ndani ya majengo ya Idara ya ujenzi mjini sumbawanga.
Watumishi walikuwa wanashiriki kusogeza Tofari Kwa kila Idara hata watumishi wa afya manesi walishiriki mpaka ujenzi ulipokamilika Na kuitwa "Nelson Mandela Stadium.Pongezi Kwa Mzee wetu shujaa wa Uwanja wa Nelson Mandela Mzee Kiwelu.
Swali lang kubwa ni kwamba uwanja asilimia 100 umejengwa Kwa nguvu za wananchi iweje Leo uwanja huo uwe Mali ya CCM? Na kuwa Mali ya CCM watanzania wengine wananyimwa fursa ya kuutumia wakati uwanja ulijengwa Na watu wote bila kujali itikadi.
Mbona uwanja wa taiga mpya Na wa zamani CCM haijimilikishi?Tunaomba wadau tulisemee hili viwanja ambavyo CCM ilivitafuta ikachoresha Ramani ikafyatua Tofari Na kutangaza kandarasi viwe vya CCM lakini viwanja ambavyo watanzania wote wamevuja jasho viwe vya serikali kama Viwanja vya Taifa ili vyama vyetu vyote viweze kuvitumia bila ukiritiba wa CCM.