Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Suala la mali za umma ambazo CCM ilijimilikisha kipindi cha kuanza siasa ya vyama vingi ni suala la muda tu! Na hii sio kwa viwanja tu, bali hata majengo na mali kadhaa. Hivi ipo siku vitarejea na pasipo udhuru. Niwakumbushe kipindi cha utawala wa G. W. Bush aliwahi kusema "its just a mater of time" akiamini kumpata gaidi Osama, na hata Raisi Obama alipoingia madarakani alirejea kauli ile ile ya Bush na hatimaye Osama alipatikana na kufa kifo cha AIBU. Ndivyo itakavyokuwa kwa CCM,chama changu kipendwa nilichokitumikia kwa miongo mingi.
 
Rais Magufuli akipewa uenyekiti wa chama,afanye jitihada kuvirejesha hivi viwanja serikalini na kukabidhi kwa halmashauri za maeneo husika.
Viwanja hivi vikirejeshwa Serikalini hata viwango vya michezo vitapanda,na viwanja vitatunzwa vizuri.!!!
Rais Magufuli akivirejesha hivi viwanja mikononi mwa umma,atakumbukwa daima na watanzania.
 
najua humu kuna watu wanamahaba mazito na ccm watatoa mapovu kutetea unyanganyi huu wa mchana kweupe kabisa
 
CCM ili jirithisha vitu vingi pamoja na majengo ambavyo vyote watanzania wote walichangia kwa hiyari au lazima. Kwa hiyo ulipoingia mfumo wa vyama vingi ilitakiwa hizi mali zikabidhiwe serikali za mikoa ili vyama vyote vianze sambamba
 
Mna kichaa. Mali ni za ccm na hati miliki zipo. Waliojenga ni wananchi (wana ccm na wasio). Asiyeridhika aseme alichangia nini arudishiwe. Wakati huo kama hukuwa mwanachama basi ulikuwa shabiki wa ccm. Wananchi walikipenda, walikiheshimu chama na ndo maana walikichangia kwa hiari yao. Msidanganywe na wanasiasa uchwara wa leo. Ulizeni umaarufu wa ccm ndani na nje ya Tz. Kwanini 80pc ya watz walikataa vyama vingi? Hao ndo walichangia raslimali za ccm. Halafu mnataka kuwanyang'anya. Tafuteni za kwenu. Acheni viroba.
 
CCM = chama cha majambazi halafu unauliza majambazi walizipata vipi mali ya umma?
 
Rais Magufuli akipewa uenyekiti wa chama,afanye jitihada kuvirejesha hivi viwanja serikalini na kukabidhi kwa halmashauri za maeneo husika.
Viwanja hivi vikirejeshwa Serikalini hata viwango vya michezo vitapanda,na viwanja vitatunzwa vizuri.!!!
Rais Magufuli akivirejesha hivi viwanja mikononi mwa umma,atakumbukwa daima na watanzania.
Magufuli hayupo kwa ajili ya nchi, yupo pale kwa ajili ya chama kwanza ndio kilichomuweka pale. Kwani alieviiba si Nyerere sasa unataka Magufuli amuende kinyume baba wa taifa.
 
Kwanza niwasaidie wale wanaotafakari kila kitu kwa upande mmoja tu. Mimi mpaka sasa naikubali kazi ya JPM.
Turudi kwenye maada. Viwanja vyote hivyo ni mali ya umma. Vimilikiwe na halmashauri za miji husika.
 
Ccm ni chama cha siasa kinachomiliki viwanja vingi sana nchini vya mpira wa migu, hivi viwanja vilihodhiwa na hiki chama wakati wa chama kimoja na wakati huo vilikua ni kama mali ya serikali au Mali ya umma! Baada ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi ccm walibaki kuvikumbatia viwanja hivi kama mali zao binafsi bila kuangalia njia jinsi walivyojimilikisha.


Haiwezekani Mali ya umma kumilikiwa na taasisi moja isiyokua ya umma, mbaya zaidi hivi viwanja vimekua kama maeneo ya wazi yasiyokua na mwenyewe.Wanufaika ni watu wachache tu ilihali ni Mali ya umma. Ipitiwe ipya mikataba ya milikishwaji wa viwanja hivyo.


Ni wakati mwafaka kuangalia sheria na utaratibu kwa mujibu wa katiba uhalali wa CCM ilivyojipatia rasirimali hizo! Utaratibu wa kisheria uliotumika ni upi? Kama utaratbu uliotumika sio sahihi baso Viwanja vimilikishwe halmashauri zote nchini ili viwe ni vyanzo vya mapato Tanzania yetu iende mbele.


Tusiishie tu kusema kua maeneo ya wazi yalioachwa hayaendelezwi yataifishwe bali hata viwanja hivi pia ni miongoni mwa maeneo ya wazi yasiondelezwa yamilikishwe halmashauri kuliko kuchakaa tu hovyo.
 
Viwanja ni vya TANU ambayo ni CCM, iweje virejeshwe serikali kuu au Halmashauri?
 
CCM jamani hivyo viwanja vilijengwa Na watanzania wote sio wana CCM virudisheni Serikalini
 
Thread nzuri sana, viwanja vya CCM vimegeuka magofu, mateja wanavutia bangi mchana kutwa. Mheshimiwa Nape Nnauye tafadhali sana yasome mawazo na maoni ya wananchi kupitia uzi huu. Rwanda wameweza kuandaa CHAN kwa kutumia viwanja vinne tu, sisi tuna rundo la viwanja ambavyo havikarabatiwi, serikali inaona ufahari katika kuvitumia kwenye shughuli za kuzima mbio za mwenge na sherehe za Mei Mosi.
 
Hamashauri na Manispaa mbalimbali, sasa zinataka haki itendeke ili kujiongezea kipato waweze kuhudumia jamii yao kwa miundombinu bora, shule na Hospitali za Viwango vizuri. Ndiyo maana Magufuli aliposhinda Urais walishangilia sana kwani CCM iliwanyanyasa sana kwa kuwanyang'anya haki yao.

Kabla ya vyama vingi, Jamii za kitanzania, walikuwa wanajingoza kwa kujitafuta vyanzo mbadala vya mapato. Walijenga Viwanja vya Michezo, Nyumba za Kupangisha, Maduka n.k. Tena kila mwananchi alishiriki kujenga, eidha kwa kutoa mchango au kutumia nguvu zao kwa amri ya Serikali sio chama.

Mfano, aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Rukwa Meja jenerali Tumainiel kiwelu. Mkuu huyu ndiye aliyetoa wazo la kuujenga uwanja unaoitwa "Nelson Mandela".

Mkuu huyu aliagiza kila mtanzania aliopo mkoani Rukwa Kwa maana ya wilaya zake lazima ashirika ktk ujenzi huo .

Wilaya zilichangisha wananchi wakulima wafugaji watumishi wafanyabiashara n.k michango yote ilipokelewa Na ofisi ya MKUU wa mkoa Kwa udhibiti.

Baada ya hiyo michango ambayo ilikuwa endelevu ikiwa in pamoja Na nyongeza ya bei kwenye bidhaa kama soda via Na mafuta.Ujenzi wa uwanja ulianza Kwa kushirikisha makampuni yote ya ukandarasi yaliyopo mkoa wa Rukwa Na mikoa ya jirani.

Pia aliwaleta wakimbizi wa Burundi waliokuwa kwenye kambi iliyopo katumba mpanda kwani wajenzi wazuri ambao waliweka kambi ndani ya majengo ya Idara ya ujenzi mjini sumbawanga.

Watumishi walikuwa wanashiriki kusogeza Tofari Kwa kila Idara hata watumishi wa afya manesi walishiriki mpaka ujenzi ulipokamilika Na kuitwa "Nelson Mandela Stadium.Pongezi Kwa Mzee wetu shujaa wa Uwanja wa Nelson Mandela Mzee Kiwelu.

Ajabu baada ya vyama Vingi mwa 1992, zilinguvu za Watanzania wakasema zilikuwa nguvu za CCM hivyo Vitu vyote vikarudi CCM. Umma ukabaki mikono mitupu na vitega uchumi vyao vikaanza kuteteleka na huo ndo ukawa Mwanzo wa Umasikini wa kutupwa wa Watanzania walio Wengi.

Na majina walibadilisha sijui wakaita CCM kilumba n.k.
images (5).jpg

Hizi mali za Umma bora Zirudishwe kwa Umma ziendeshwe na ALAT kama vyanzo vyao vya mapato kwani wanafanya kazi nzuri sana.

Mbaya zaidi, Vitega Uchumi hivyo ambavyo CCM walipora, havilipi kodi wala mchango wowote, hata Mwenge ukija wananchi ndio wanachangia.

Nashauri Mali zote ambazo zilikuwa za CCM au kujengwa kwa nguvu ya wananchi au fedha za serikali wakati wa chama kimoja zitarudishwa mikononi mwa umma. Mali walizozipata kwa nguvu ya wana CCM baada ya 1992 zitaangaliwa na kupimwa kuona kama hazikutumia hata shilingi moja toka fedha za umma.
IMG_2448.JPG

Hii itarudisha Imani kwa Wananchi na kuendeleza Mshikamano. Vijana wa chama kimoja walifanya makubwa kuliko vijana wa Sasa. Hawa Vijana wa sasa wanatumia Urithi wa babu tu na kujitapa wana maendeleo wakati waliojenga wapo barabarani Ombaomba wengine Wamewekwa kwenye majumba ya kulelea wazee bila huduma yoyote.
wazee 2.JPG

matonya ombaomba. (1).jpg

Waliotumia nguvu zao wakijua zitawasaidia uzeeni, Sasa hivi wanahangaika. Mbaya zaidi wale waliotumia haki yao ya kujiunga na upinzani ndo kwaanza wanaonekana kama hawana haki ya kukaa nchini wala kufaidi Mema ya nchi waliopanda wenyewe.

Kama kulima kote tumelima wote, Hata kupanda Kote tumepanda wote, Kupalilia tumepalilia wote, Aah nashangaa sasa Mbona hatuvuni wote CCM ni nini kimewasibu?

Bado naamini Rais Magufuli akipata uenyekiti atafanya jambo kwaajili ya Masikini waliompigia kura.

Hii itamsaidia pia kutimiza ahadi zake. Ikibidi CCM wapelekwe mahakama za kifisadi. Wamefisadi nchi
 
Back
Top Bottom