Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

kuna habari zinaenea kwa kasi kubwa nchi nzima kuwa asilimia karibu tisini ya viwanja vya michezo vinamilikiwa na chama cha mapinduzi CCM. Kiwanja kama CCM kilumba, kambarage (shinyanga), jamhuri (morogoro) ali hassan mwinyi, shekh amri abeid (Arusha) nangwanda sijaona (mtwara) na vingine vingi eti ni vya ccm. jambo la kujiuliza hapa ni kwamba CCM walijenga kwa rasilimali zao ama kwa kodi za wananchi wakati wa chama kimoja? Hapa watanzania tuwe makini sana watu wachache wasijilimbikizie mali za watanzania.



waulize waonyeshe hati miliki za viwanja hivyo ndiyo utajua jasho la wananchi ktk nchi hii linaliwa na wababe wenye nguvu,na ndiyo sababu wako tayari hata kuondoa roho au maisha ya watu ili waendelee na mfumo wao wa utawala, wakijua kwamba akiingia mtu mwingine totauti, haya yote yatakuwa kwa manufaa ya wananchi wote.

kitu ambacho CCM hawataki kusikia au kuona kinatokea. Kimsingi viwanja hivi vilipaswa kuwa chini ya umiliki wa Halmashauri za miji kwa kuwa vilijengwa na wananchi wote wakati wa chama kimoja.

Ili vimhudumie kila mwananchi bila kujali itikadi za kisiasa na si chama fulani. Lakini CCM wamepora na kufanya mali yao. Waonyeshe Bill of quantity ili umma ujue walitumia pesa ngapi ktk huo mradi. Hakika iko siku watajibu kwa aibu kubwa.
 
Magamba hawawezi kurudisha viwanja hivi, ni chanzo muhimu sana cha mapato yao. Nimewasikia mara kadhaa wakigoma kutoa matamko kuhus mali hiz za Watzanania wote
1. CCM Kirumba/Nyamagana - Mwanza
2. Sokoine Stadium - Mbeya
3. Sheikh Amri Abeid - Arusha
4. Kaitaba - Kagera
5. Mkwakwani - Tanga
6. Jamhuri - Mjikasoro Pwani

CCM kambarage shinyanga pia ni wa ccm, warudishe mali za umma
 
Hivi viwanja ifanyike Kama Udom....ambapo ulikuwa ukumbi wa chimwaga ...zamani wengine hamjuwi ...Chama Kimoja Kila kiongozi Akitembelea mikoani Atapewa michango.
1. Michango wa kuendelea Ukombozi Kusini mwa Afrika
2. Michango ya Ujenzi wa Makao Makuu ya Chama Dodoma

Kwenye mikoa nako kulikuwa na michango ya pesa na nguvu kujenga ofisi za Chama Mikoani,wilayani ,kata ...na Zaidi viwanja Vya michezo...hii ilikuwa pamoja na kuongeza bei kwenye mazao ...na vinywaaji....Hakuna mwananchi Leo ambayee
Ukommbozi,Ofisi na viwanja hivyo Hana jasho..hata wakikuambia hukuwepo...waaambie kuna jasho la wazazi wako.....

Lazima viwanja Vya michezo vyote na baadhi ya ofisi zirudishwe halmashauri....tena bora wafanye kwa hiari.....wakichelewaa....Kama KANU wataishia kuporwa Kila kitu........Mali watakazobaki nazo watakiwe kudhibitisha hazikutokana na jasho la umma...
 
Hakuna anayebisha kwamba viwanja vyote na majumba yanayomilikiwa na CCM yalijengwa kwa michango isiyo ya hiyari ya wananchi wakati wa chama kimoja.

Kwa akili za kawaida tu, CCM ilikuwa ikabidhi viwanja vile kwa Halmashauri na isingekuwa vibaya sana hata kama wangebaki na nyumba na miradi mingine baada ya nchi kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.

Lakini kwa kuutumia mwanya wa wananchi kutoelewa haki zao chama hiki kinachotegemea serikali kuishi si tu kimeng'ang'ania kumiliki kila kitu; bali kimekuwa kikiutumia uwezo huo ulioporwa toka umma kuvinyanyasa vyama vingine.

Kimsingi CCM inaweza pokonywa mali zote hizo zenye jasho la umma kama watapelekwa Mahakamani kudaiwa ingawa kwa mwenendo wa Mahakama zetu haitakuwa ajabu pia Mahakama ikatoa maamuzi tata kama yale ya kuidhinishwa kwa mgombea binafsi!

Hilo likitokea sasa; masaa ya CCM kupumua yanaweza hesabika labda wakaibe tena BOT na fedha za wastaafu kule Hazina na kusaini mikataba ya chini ya zuria kama walivyozowea.
 
CCM walipora viwanja hivyo na kujimilikisha wenyewe wakati uhalisia ni kwamba viwanja hivyo ni mali ya serikali, mali ya watanzania. Ikumbukwe kuwa vilijengwa wakati wa mfumo wa chama kimoja ambapo chama na serikali ilikuwa kitu kimoja. Kwa wakati ule hatukuona shida yoyote kiwanja kuitwa kwa mfano "CCM Kirumba" kwa sababu chama kilikuwa kimeshika hatamu. Nakumbuka vyema miaka 1980 mwanzoni wakati uwanja wa Kirumba unajengwa, mkulima alikatwa kiasi fulani cha pesa kwenye kilo ya pamba iliyouza kwenye chama cha ushirika kuchangia ujenzi huo.

Mimi nafikiri kuna haja ya wanaharakati, wapinzani na wapenda maendeleo wengine wenye weledi wa sheria kuifunguilia mashitaka mahakamani CCM kwa kupora mali ya umma kwa njia ya udanganyifu au kesi ya uhujumu uchumi. Hili linaweza kufanyika sasa au baada ya CCM kuondoka madarakani. Naamini CCM watakuwa na kesi ya kujibu.
 
mi nashindwa kuelewa................
kwanini CLUB BILICANAS inamilikiwa na FREEMAN AIKAELI MBOWE????
 
aluta continua, viwanja vya michezo na mali nyingine zote lazima zirudishwe,
wamezoea kuiba hata kitu ambacho kipo peupe wanapora!,
 
mi nashindwa kuelewa................
kwanini CLUB BILICANAS inamilikiwa na FREEMAN AIKAELI MBOWE????

jiulize pia kwanini mohamed interprise inamilikiwa na mohamed dewji, na azam mmiliki wake ni bakharesa
ccm lazima mrudishe mali zetu
 
jiulize pia kwanini mohamed interprise inamilikiwa na mohamed dewji, na azam mmiliki wake ni bakharesa
ccm lazima mrudishe mali zetu
nayo imerithi kaka. wakati akina mbowe wanajifunza U-DJ wenzao walikuwa wanahamasisha wananchi kujenga....lol
 
Kikubwa nani mwenye hati miliki, Hivi kuna mtu anajua hati miliki ya mipaka ya Tanganyika anayo mjerumani maana ndiye aliyepima ramani 1884 na haijabatilishwa

unapotea njia kk, mpima ramani co mmliki wa ramani, ramani nyingi za tz zimepimwa na mashirika makubwa duniani lakini sio ramani zao,
hata mipaka ya tanganyika kupimwa na mjerumani co kwamba tanganyika ni ya wajerumani.
cha mcngi ccm rudisheni mali zetu au la tutachukua wenyewe.
 
Ni jeuri ya ccm kuwa madarakani, wanaamua watakavyo.
 
Hivi viwanja ni vya watanzania,kipindi kile wananchi walikuwa wanachangishwa pesa na kufanyishwa kazi ili kukamilisha miradi hii,iweje leo waseme vyakwao?
Au wathibitishe kuwa wote waliokuwa wanajitolea kujenga na pesa zao walikuwa wana ccm?
Babu yangu aliniambia walifanyishwa kazi sana kwenye hivyo viwanja hasa yeye alikuwa pale mwanza
 
Tangu nakua nimekuwa nikisikia kuwa viwanja vya mpira vilivyopo mikoani vinamilikiwa na chama tawala CCM mfano CCM Kirumba Mwanza, Shekh Amri Abeid Karume Shinyanga, Ally Hassan Mwinyi Tabora, Sokoine Mbeya, uwanja wa Jamhuri Dodoma, Majimaji Songea sina uhakika! viwanja vilijengwa na chama au na serikali?
 
Havikujengwa na chama hata kiwanja kimoja mkuu ccm wamepora tu.
 
Ni kwanini vinamilikiwa na CCM na sio CUF? Kwanini CCM na sio Watanzania.. Najaribu kujiuliza tu, inamaana vyote vilijengwa kuanzia mwaka 1977> kuja juu? Na je pesa ya kujenga ilipatikana wapi? Au ni michango ya wanachama? Na je kwa miaka hyo uwezo wa wananchi kifedha ulikuwaje mpaka waweze kuchanga mamilioni? Ukizingatia population ilikuwa ndogo.. Au walifadhiliwa? Na nani?

Just curious to know!!

Tujadiliane..
 
vilijengwa kwa hali na mali za wananchi, vipato vilikua chini lkn ari ilikua juu
 
Back
Top Bottom