kuna habari zinaenea kwa kasi kubwa nchi nzima kuwa asilimia karibu tisini ya viwanja vya michezo vinamilikiwa na chama cha mapinduzi CCM. Kiwanja kama CCM kilumba, kambarage (shinyanga), jamhuri (morogoro) ali hassan mwinyi, shekh amri abeid (Arusha) nangwanda sijaona (mtwara) na vingine vingi eti ni vya ccm. jambo la kujiuliza hapa ni kwamba CCM walijenga kwa rasilimali zao ama kwa kodi za wananchi wakati wa chama kimoja? Hapa watanzania tuwe makini sana watu wachache wasijilimbikizie mali za watanzania.
waulize waonyeshe hati miliki za viwanja hivyo ndiyo utajua jasho la wananchi ktk nchi hii linaliwa na wababe wenye nguvu,na ndiyo sababu wako tayari hata kuondoa roho au maisha ya watu ili waendelee na mfumo wao wa utawala, wakijua kwamba akiingia mtu mwingine totauti, haya yote yatakuwa kwa manufaa ya wananchi wote.
kitu ambacho CCM hawataki kusikia au kuona kinatokea. Kimsingi viwanja hivi vilipaswa kuwa chini ya umiliki wa Halmashauri za miji kwa kuwa vilijengwa na wananchi wote wakati wa chama kimoja.
Ili vimhudumie kila mwananchi bila kujali itikadi za kisiasa na si chama fulani. Lakini CCM wamepora na kufanya mali yao. Waonyeshe Bill of quantity ili umma ujue walitumia pesa ngapi ktk huo mradi. Hakika iko siku watajibu kwa aibu kubwa.