Lissu atangaza mgomo wa kula chakula kuanzia Jumatatu, 26/10/2026

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251

Mwenyekiti amesema kuanzia Jumatatu ya tarehe 26/10/2026 anaanza mgomo wa kutokula chakula kwa sababu amenyimwa haki yake ya kukutana na Mawakili kwa sababu anasimamia maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania huo ambao ulitolewa wiki iliyopita kuwa ana haki ya kukutana na mawakili.

"Hayo ameyaeleza Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Rugemeleza Nshala alizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 24, 2026 jijini Dar es Salaam.

Dkt. Nshala amesema uamuzi wa Lissu umetokana na mawakili wake ambao ni Nashon Nkungu na Paul Kisabo kwenda gerezani kwa lengo la kumuona Lissu lakini uongozi wa Gereza la Ukonga liliwaambia kuwa utaratibu utatumika kama ule uliokataliwa na Mahakama kuwa Naibu Mkuu wa Gereza, Mwanasheria na Maafisa wengine watakuwepo katika chumba wanachozungumza na Lissu.

Dkt. Nshala amesema Lissu alikataa kuzungumza na mawakili wake akisema utaratibu ulioagizwa na Mahakama kuwa maafisa wakae umbali wanaoweza kuona na sio kusikia umekiukwa.

Baada ya hapo Dkt. Nshala anasema alienda gerezani mwenyewe ambapo aliambiwa kuwa hawezi kuonana na Lissu kwa sababu amesema hayupo tayari kuzungumza ndipo alipokataa ujumbe huo na kutaka kuonana na Lissu lakini hata alipofanikiwa kuonana nae msimamo ulikuwa ule ule kuwa hawezi kuzungumza mpaka amri ya Mahakama ifuatwe.Jambo TV inaendelea na jitihada za kulitafuta Jeshi la Magereza ili kupata ufafanuzi wa tuhuma hizi.

Pia soma: Mawakili wa Lissu waibuka kidedea, Gereza la Ukonga lapewa maagizo
 
ok.
well done,

nakumbuka aliwahi kua anaenda nakontena la ubwabwa na maharagwe, hadi kizimbani, hivi alikua kapatwa na nini siku zile? :pedroP:

halafu,
ukiona binadamu alie hai anakataa mambo ya dunia hii kama vile kula chakula, kunywa maji n.k, ujue anatamani mambo ya mbinguni :pedroP:

binafsi namtakia kila la kheri kwenye jambo hilo la hiyari analoanza rasmi j3 tar.26.10.2030, I hope atamaliza rasmi kama kiki ya kuatract public sympathy 29.10.2026 right?

well done fr.charz kitma for this cript🐒
 
Zikipita siku tatu mtamuona tu atavamia masufuria ya ugali hapo ukonga yeye mwenyewe bila kulazimishwa.
Mawazo ya kiongozi wenu aliyemtia ndani pasina kosa, alifikiri ujinga kama huu wa kwako eti akitiwa ndani miezi kadhaa atakubaliana na matakwa yake, Leo Lissu anamaliza mwaka na miezi na hana mpango wa kupiga goti kwa shetani kama mlivyo baadhi huko CCM

Sikiliza we kijana, si Kila binadamu lazima afanane na wewe!

Kuna watu wanajua kifo kipo na hawakiogopi, ila Kuna nyinyi mnaojua kifo kipo ila mnakiogopa, na nyinyi ndio watu wapumbavu kuwahi kutokea duniani

Mpo tayari kuhongwa chochote ili muamgamize wengine

Stupid!
 
Back
Top Bottom