Waulize ANC, Mandela aliongozaje ANC akiwa Tanzania na akiwa gerezani.
Kwanza siyo kweli kuwa Lisu anaishi Ubelgiji. Anayeishi Ubelgiji kwa sasa ni mkewe. Lisu muda mwingi yupo TZ. Watoto wake ni watu wazima, wameamua kuishi US.
Felix Tchisekedi wakati anaenda kugombea Urais wa DRC, alitokea Ubelgiji alikokuwa anaishi.
Kuna mazingira ambayo, hasa kwa nchi za kiafrika, wapigania haki na demokrasia ni lazima uwe na makazi nje ya nchi yako.
Fikiria nchi kama Tanzania ambayo hata ajira tu ya Serikali, ikijulikana wewe unaunga mkono vyama vya upinzani unafukuzwa kazi au huwezi kuajiriwa, kama ni mfanyabiashara, watahakilisha unafilisiwa. Ukiwa maskini, wanajua utarudi kulamba nyayo zao. Hivyo ukiweza kupata ajira nje ya nchi au biashara zako zikawa nje ya nchi, ni tahadhari muhimu sana.