LIssu: Bandari zote bara, DP World kauziwa


1. Ninakusoma kuwa #1 unakubaliana na Lissu kuwa hili ni hatari. Hili halina ubishi. Tuna Mungu mtu ikulu Kwa jina la Rais. Tulipo kaingia mkataba na DP World bila kutushirikisha.

2. #2 huna uhakika na yaliyomo, hivyo ni sawa kuchukua akisemacho Lissu kuwa mkataba umelalia kuwapa bandari zote za bara.

Ila hapa kwenye faida pana ukakasi. Bandari zote za kemondo bay, nansio ukerewe, ziwa Tanganyika, Nyasa, rukwa, Victoria huko ziwe na faida zaidi ila za Zanzibar?!

Kama ndivyo, kumbe wewe utaturejesha kwenye kuhoji huu muungano nini hasa faida yake?

3. #3 Haina tofauti kubwa na #2. Bado waongelea uwezekano wa tofauti za faida kwenye bandari bara na Zanzibar. La msingi kumbe litakuwa nini hasa faida ya muungano huu?

4. Rais ni mtanzania aliyezaliwa Zanzibar hata Lissu anasema hivyo. Kwamba hilo halina ubishi. Hilo ni kama Magufuli na Chato au Kanda ya ziwa. Hilo ni historical.

Ukakasi unakuja kunapokuwa na kuvutia nyumbani hapo hatuwezi kukaa kimya. Kumbuka daraja ziwa Victoria au Chato International airport.

5. Maslahi yatahusu Tanzania nzima na bara ni mnufaika zaidi. Hili linabishaniwa. Kwamba kupanga ni kuchagua na serikali ni mwakilishi tu, kulikoni kutaka kutulazimisha kama wana nzengo hatutaki?

LIssu anasema wenye nchi wananchi tusikilizwe. Zingatia msingi wa hoja:

"Walio wengi hawautaki mkataba huu."

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Wakija wataanza kuhamisha magpri. Kushambulia pesonality badala ya hona. hao wanakuja subiri

Wakuje tuwaone. Hoja hupingwa kwa hoja.

Bottom line Kuna mkataba hapa watanzania walio wengi hawautaki. Wanaweza kuamua kukomaa nao, ila malipo ni hapa hapa duniani.
 
Swala la bandari baadhi watu wamelichukulia kwa mtazamo hasi kwa sababu wanazozijua wenyewe na kuingiza mambo ya ukabila na udini, hivyo ndiyo chanzo kikuu cha ukakasi wa kuweza kulijadili swala hili kwa kutumia akili iliyo salama. Makubaliano yaliyotiwa saini ni IGA ambayo nikipitia kwenye kujua nini maana ya IGA nimepata kufahamu ni:-
An intergovernmental agreement (IGA) is an agreement made between the Commonwealth and state and territory governments. While IGAs are not legally binding, they express the commitment of governments to work together on certain objectives or goals.
Sasa vitu kama hivi vina shida gani?
Tusubiri tuone Project Agreement ili tuanze sasa kukosoa muda wa mkataba, ajira, faida n.k.
 
Hoja hupingwa kwa hoja:


Bandari zote bara zimeuzwa!

Kama ni kwa manufaa yetu, kwa nini siyo za Zenji?
Tundu Lissu yeye ni mkaazi wa Belgium ina muuma nini tena huku Tz?? Mama anaifungua nchi asubiri aone, hiyo bandari ya Dar es Salaam, mwaka 1896 ilianzishwa na mwarabu hivyo si mbaya akakabidhiwa tena maendeleo ni ya Tanzania hayana chama.
 
Hapa ndio najiuliza hoja ya Uzanzibar inakuja leo kwa kuwa tu rais ni mzanzibar au?
Maana kuna mambo mengi Serikali inaingia mikataba na hayasemwi kama huyu ni mzazibar au mtanganyika

Hoja ya uzanzibari inakuja kutokana na asili yake na maslahi zaidi yanakoonekana kuelekezwa.

Rejea daraja la kigongo - busisi, Chato national park, Chato international airport, teuzi mbalimbali nk. Chato na Kanda ya ziwa zikirejelewa sana awamu ile.
 
Nenda kasome objective of the agreement halafu urudi kucomment tena
 
Brazaj kwanini sisi tujadili anayoyasema Lisu na tusijadili kilichosainiwa baina ya serikali hizi mbili?
Tanzania na Dubai wamesaini kushirikiana katika kuendeleza na kuboresha bandari za Tanzania baharini na maziwani ila kwa makubaliano na TPA na DPW.

 
Maana ya mkataba usio na kikomo ni nini? Na kwanini wenyewe tu ndiyo wenye haki ya kusitisha mkataba na siyo pande zote.Haina maana tumeuzwa
 
Maana ya mkataba usio na kikomo ni nini? Na kwanini wenyewe tu ndiyo wenye haki ya kusitisha mkataba na siyo pande zote.Haina maana tumeuzwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…