Niseme ametukosea sana, au pia naweza kusema ametutukana kabisa. Kitendo cha kuwapa wageni mamlaka kamili wajitawale ndani ya nchi yetu, kama sio tusi kwa wale waliopigania uhuru sijui niite ni kitu gani tena..
Atambue tu huko alipo, anatakiwa kutuomba radhi watanganyika, aende pia kwenye makaburi ya wazee wetu waliopigania uhuru wetu awaombe radhi, kisha baada ya hapo auvunje ule mkataba wa kinyonyaji unaomtweza mtanganyika ndani ya mipaka ya nchi yake.
Asijisanganye na majibu mepesi ya kuziba masikio, ajue tu anaotuambia hayo ni watu wazima wenye akili zetu timamu, ameshakosea mwanzo kusaini ule mkataba, asiendelee kukosea zaidi, werevu tutazidi kumuona asivyojielewa.