Nimemsikiliza Tundu Lissu akiwa kariakoo akishikashika vikaratasi flani akiita mkataba wa DP World, nilitegemea angeusoma mkataba wenyewe lakini alibaki kuongelea mauzuzshi mengi na matusi kwa rais. Huyu mtu ndio maana Magufuli alitaka kummaliza, ni mwongo, mzushi, mpotoshaji, ameshahongwa na ndio zake anafaidikaga ktk mazingira km haya. Nisubiri asome mkataba wenyewe wala hakuufungua kuonesha alikuwa anapotosha tu, ni mtu mtu hatari sana kwa ustawi wa nchi hii, Rais kuruhusu na kutoa uhuru wa aina ile sijui amejiandaaje kukabilana nao. Vitu alivyozungumza haviwezekani hata kwa akili ya kawaida.
Alivyo mnafki leo hakuzungumzia habari za Magufuli zaidi ya kujaribu kumsifu, hii inatokana na kusoma upepo kuwa akimsema Magufuli pengine wananchi wasingeelewa upotoshaji wake. Ila amewatukana mkapa na Kikwete na kuwarushia mauwongo mengi sana. Mimi nachoweza kumshauri Rais wangu apige kazi na mikataba km mingine ibaki siri ya serikali siyo lazima lwenda bungeni, watanzania wengi uwezo wao wa kuelewa na kupambanua mambo ni mdogo sana ila wakiona matokeo mazuri watakuelewa na kukusifu. Sasa hivi wananchi watachanganywa sana, ila huu uhuru uliopitiliza kiasi wa upotoshaji udhibitiwe. Mwisho rais we piga kazi ukiwasikiliza watakukwamisha baadaye waseme si mmeona ameshindwa?