Lissu: Mkataba na DP World Rais Samia ametukosea sana!

"furani" ndiyo mungu yuppi huyo?
Mimi najua sana kiarabu kuliko kiswahili [emoji1787][emoji1787][emoji1787] kwani ujui kiarabu ni lugha ya mtume mudi aleku musalamu[emoji1787][emoji1787][emoji1787] pia kumbuka sisi ngozi nyeusi kukifufuliwa tutafufuliwa waarabu peponi
 
We are doomed.....
 
Kwani Mama haupigi tena mwingi?[emoji1787][emoji1787]

Kuupiga mwingi siyo kipaji kama urefu au ufupi. Hata mgema akisifiwa tembo hutiwa maji.

Sifa Kwa binadamu mwenye nyama na roho hazijawahi kuwa "perpetual." Ndiyo maana wakasema "hujafa hujaumbika."

Ukibutua unavaliwa vizuri tu.
 
Nia ovu kutoka kwa viongozi wetu ilidhihirika pale walipoudanganya umma kwamba walichosaini sio mkataba. Wabunge pia bungeni wameidhinisha kitu wasichokijua, hawakuelewa kwamba wameidhinisha mkataba.
Wabunge wenyewe akina Msukuma, Jahpipo, Kibajaji
 
Nadhani Kuna watu wamedhamiria kuuvunja Muungano na kuhakikisha tunagombana lengo Uganda na Tanzania zisifaidi rasilimali zao za kuwainua kiuchumi.

Watashindwa na wanaotumiwa kutuchonganisha wataadhibiwa!
 
Maneno kuntu
Ujumbe maridhawa sana huu kwa huyu mama. Asipozisikia sauti zote hizi asije kulaumu mtu mambo yakimharibikia.
 
Dubai si nchi bali ni sehemu tu ya nchi iitwayo Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates - UAE), kwa Kiswahili hufupishwa Himarati. Ni kama ilivyo Dar es Salaam ni sehemu tu ndogo ya nchi ya Tanzania.

Ni aibu na fedheha kubwa kwa nchi yetu kuingia mkataba wa kutawaliwa na kisehemu tu cha nchi fulani.
 
Samia ana namna mbili za kujinusuru, si moja! Mbali na kuufuta mkataba, namna ya pili ni kujiuzulu urais kwa aibu aliyoiingiza nchi ili awapishe wazalendo wa kweli na wanaoweza kusimamia, kudhibiti, kuendesha na kuendeleza bandari zetu kwa ufanisi.
 
Nimemsikiliza Tundu Lissu akiwa kariakoo akishikashika vikaratasi flani akiita mkataba wa DP World, nilitegemea angeusoma mkataba wenyewe lakini alibaki kuongelea mauzuzshi mengi na matusi kwa rais. Huyu mtu ndio maana Magufuli alitaka kummaliza, ni mwongo, mzushi, mpotoshaji, ameshahongwa na ndio zake anafaidikaga ktk mazingira km haya. Nisubiri asome mkataba wenyewe wala hakuufungua kuonesha alikuwa anapotosha tu, ni mtu mtu hatari sana kwa ustawi wa nchi hii, Rais kuruhusu na kutoa uhuru wa aina ile sijui amejiandaaje kukabilana nao. Vitu alivyozungumza haviwezekani hata kwa akili ya kawaida.

Alivyo mnafki leo hakuzungumzia habari za Magufuli zaidi ya kujaribu kumsifu, hii inatokana na kusoma upepo kuwa akimsema Magufuli pengine wananchi wasingeelewa upotoshaji wake. Ila amewatukana mkapa na Kikwete na kuwarushia mauwongo mengi sana. Mimi nachoweza kumshauri Rais wangu apige kazi na mikataba km mingine ibaki siri ya serikali siyo lazima lwenda bungeni, watanzania wengi uwezo wao wa kuelewa na kupambanua mambo ni mdogo sana ila wakiona matokeo mazuri watakuelewa na kukusifu. Sasa hivi wananchi watachanganywa sana, ila huu uhuru uliopitiliza kiasi wa upotoshaji udhibitiwe. Mwisho rais we piga kazi ukiwasikiliza watakukwamisha baadaye waseme si mmeona ameshindwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…