Lissu na Muungano wa mchongo, aeleza kutekwa kwa Jumbe

Lissu na Muungano wa mchongo, aeleza kutekwa kwa Jumbe

Huo muungano hauwezi kusimama ukichambuliwa na kujadiliwa kwa uwazi, una matobo mengi tangu mwanzo.
Waumini wake wanataka uwe kama dini, usihojiwe.

Muungano wa watawala usiotakiwa na wananchi wa nchi mbili husika hauwezi kudumu, kuna siku utasambaratika
Ninakubaliana na wewe.

Kwa maoni yangu: Muungano ulio asisiwa 1964 ulikuwa na "matobo" kwa sababu zilizofahamika; lakini matobo hayo hayakuwa yamelenga kutufikisha hapa tulipofikia leo; kwa Zanzibar kujitangazia baadhi ya mambo bila ya ushiriki wa serikali ya Muungano na Bunge lake.
Kwa mfano: Katiba ya Zanzibar haikuwemo kwenye maswala ya Muungano 1964, na wala katiba hiyo ilipoanzishwa sikumbuki kama serikali au Bunge la Muungano zilihusishwa kuhusu uwepo wa Katiba hiyo. Hili ni 'tobo' ambalo ni wazi halikuwemo kwenye muungano wa mwanzo.

Kuna mifano mingine kadhaa, ambayo imetokana na kilichobatizwa na kundi lisilokuwa na nia njema ya muungano kuwa "Kero za Muungano." Hilo kundi siku zote limehakikisha Muungano usifanikiwe, lakini lililporuhusiwa kuweka ajenda zake, matokeo ndiyo haya tunayoyaona leo. Zanzibar kuwa na mamlaka makubwa, hata kiasi cha kudhani kuwa ndio watawala wa Tanzania.

Kwa hiyo, kwa maoni yangu, Muungano upo kama ulivyo sasa, siyo kwa matakwa yaliyonuiwa toka mwanzo, bali ni udhaifu wa viongozi walioruhusu maoni ya kundi lisilotaka Muungano kushika hatamu ndani ya Muungano wenyewe.

Muungano ulivyokuwa tokea mwanzo, matarajio yalikuwa kwamba baada ya kuondokana na hofu zilizokuwepo upande mmoja, i.e., Zanzibar kumezwa na Tanganyika, Muungano ungeelekea kuwa taifa moja, badala ya sehemu moja kuendelea na kuimarisha uZanzibar wao. Badala yake, uZanzibar ndio umepaliliwa kwa nguvu zaidi na sehemu moja na kuuvuruga Muungano ulionuiwa toka mwanzo.
 
Mkataba wa Muungano sio kwamba haukupata ridha za wananchi WA Zanzibar Tu, hata wa Tanganyika pia hawakupiga kura
Lakini hili halina maana kuwa kama haikuwezekana wakati huo, kwa sababu maalum, sasa hivi haliwezi kufanyika. Kwa hiyo, suruhisho zuri ni kuwauliza wananchi sasa hivi kama wanautaka muungano. Sioni sababu kamwe ya kuzuia hili lisifanyike sasa.
 
Kwa nini tuwe na serikali nyingine ndani ya Muungano kama ilivyo sasa wakati Muungano ni Serikali moja?

Yaani kwenye familia yako unaweza kuruhusu mtu mwingine awe Baba ambaye atacontrol baadhi ya wanafamilia huku wewe ndio ukiwa Top controller wa wote?
One country two systems
 
Kwani hicho kinachoitwa Muungani ni lazima? Kama Muungano wa kweli usio wa kinyonyaji (parasitic) unashindikana, kila mtu achukue njia yake
Hayati Karume alisema Muungano ni kama koti !
Likikubana unalivua. 😅🙏🙏 !

Na Hayati Nyerere alisemaga dhambi ya Ubaguzi huwa inaendelea tu ni sawa na mtu akila nyama ya mtu huwezi kuacha !! 😅🙏 !
 
Tundu Lissu akielezea kuhusu muungano wa mchongo.

Aelezea kuhusu wapinga muungano wa kizanzibari kutekwa na kuwekwa vizuizini, Jumbe na wenzake.

Sikilizeni hapa cheche zake.
MUUNGANO WETU UPO IMARA NA THABITI KABISA HAKUNA MENDE WALA KIZUKA WA KUUCHOKONOA WALA KUUBOMOA, THIS IS A MUTUAL BONDS, HUYU GAY SIJUI KWA NINI ANAWASHWA WASHWA ZAIDI KIPINDI HIKI, ARUDI UBELGIJI.
 
Hayati Karume alisema Muungano ni kama koti !
Likikubana unalivua. 😅🙏🙏 !

Na Hayati Nyerere alisemaga dhambi ya Ubaguzi huwa inaendelea tu ni sawa na mtu akila nyama ya mtu huwezi kuacha !! 😅🙏 !
Kwani huu tulionao ni Muungano au ni mtoto kunyonya kwa mama? Hakuna Muungano hapa, tuungane kweli chini ya Rais mmoja au mtoto akajitegemee, ameshaluwa mkubwa, kaota ndevu sasa..
 
Back
Top Bottom