PreGE2025 Lissu: Uchaguzi hautafanyika wananchi mkakubaliana na msimamo wetu mkaandamana siku ya uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu, chama hicho kitaitisha maandamano ya kuuzuia uchaguzi usifanyike.

IMG_3923.jpeg
Kauli hiyo ya Lissu, inajibu swali kuhusu mbinu ambayo chama hicho itaitumia kuzuia uchaguzi kuendana na ajenda yake ya 'No Reforms, No Election' (bila mabadiliko, hakuna uchaguzi).

Lissu amesema hayo leo, Jumatatu Aprili 7, 2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara katika ziara ya kutoa elimu kuhusu 'No Reforms, No Election.'

IMG_3925.jpeg

Amesema iwapo Serikali haitafanya mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi, chama hicho kitawahamasisha wananchi kuandamana kuuzuia uchaguzi usifanyike.

"Nani anayataka kuendelea na mateso ya CCM mpaka Kiama? Ndio maana sisi CHADEMA tunasema, kama hawataki mabadiliko kwenye mfumo wa uchaguzi, tuzuie uchaguzi usifanyike," amesema Lissu, huku akiwataka wananchi wa Masasi na Watanzania kwa ujumla kuunga mkono msimamo huo.

"Uchaguzi hautafanyika kwa sababu Lissu amesema tu! Hautafanyika kama wananchi wa Masasi na Watanzania wote mkikubaliana na msimamo wetu na kusema: uchaguzi huu hautafanyika, Hatutaenda kupiga kura, hatutaenda kujiandikisha, na siku ya kupiga kura tutaandamana. Watatufunga wote? Kuna sheria ya Tanzania inayosema lazima tushiriki kwenye chaguzi za kijinga?" amehoji.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu, chama hicho kitaitisha maandamano ya kuuzuia uchaguzi usifanyike.

View attachment 3296017
Kauli hiyo ya Lissu, inajibu swali kuhusu mbinu ambayo chama hicho itaitumia kuzuia uchaguzi kuendana na ajenda yake ya 'No Reforms, No Election' (bila mabadiliko, hakuna uchaguzi).

Lissu amesema hayo leo, Jumatatu Aprili 7, 2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara katika ziara ya kutoa elimu kuhusu 'No Reforms, No Election.'

View attachment 3296018Amesema iwapo Serikali haitafanya mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi, chama hicho kitawahamasisha wananchi kuandamana kuuzuia uchaguzi usifanyike.

"Hatutaenda kupiga kura, hatutaenda kujiandikisha, siku ya kupiga kura tutaandamana, watatufunga wote? Kuna sheria ya Tanzania inayosema lazima tushiriki kwenye chaguzi za kijinga?" amehoji.

Chanzo: Mwananchi
Labda anataka akimbilie tena kwa wanaume zake huko Ubelgiji
 
Lisu hajielewi unazuiaje haki ya mtu mwingine ya kikatiba ya kupiga kura anayetaka kupiga kura?

Lisu hana ubavu wa kuzuia utekelezaji wa katiba

Binafsi nitaenda kura na sioni yeyote wa kunizuia nisitekeleze haki yangu ya kikatiba ya kupiga kura
 
Tunafanya uchaguzi au uhuni?
Mimi binafsi naamini ni uchaguzi wewe kama huamini sio kesi

Sheria za uchaguzi hazilazimishi mtu kwenda kupiga kura lakini haziruhusu kumzuia mtu mwingine asipige kura

Lisu anachotaka kuzuia watu wengine wasipige kura hilo ni kinyume cha katiba ya nchi na Sheria za nchi

Na majeshi moja ya kazi zao walizoapa ni kulindq katiba iliyopo

Lisu na genge lake wanajaribu kuvunja katiba

Hilo jambo sio rahisi Lisu anawapotezeeni muda tu na kuwalisha ujinga
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amesema siku ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu, chama hicho kitaitisha maandamano ya kuuzuia uchaguzi usifanyike.

View attachment 3296017
Kauli hiyo ya Lissu, inajibu swali kuhusu mbinu ambayo chama hicho itaitumia kuzuia uchaguzi kuendana na ajenda yake ya 'No Reforms, No Election' (bila mabadiliko, hakuna uchaguzi).

Lissu amesema hayo leo, Jumatatu Aprili 7, 2025 wakati akihutubia mkutano wa hadhara Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara katika ziara ya kutoa elimu kuhusu 'No Reforms, No Election.'

View attachment 3296018Amesema iwapo Serikali haitafanya mabadiliko ya sheria na kanuni za uchaguzi, chama hicho kitawahamasisha wananchi kuandamana kuuzuia uchaguzi usifanyike.

"Hatutaenda kupiga kura, hatutaenda kujiandikisha, siku ya kupiga kura tutaandamana, watatufunga wote? Kuna sheria ya Tanzania inayosema lazima tushiriki kwenye chaguzi za kijinga?" amehoji.

Chanzo: Mwananchi
Tunashauri watoto wa Lisu na mke wake wawe msitari wa mbele tutamuunga mkono kabisa
 
Back
Top Bottom