Lukuvi na Kabudi waitwa Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia nje ya Muundo wa Serikali
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri.
View attachment 2075769
Rais Samia kasema watu Wasimpake matope Lukuvi. Wala Wasimsingizie kwamba anaenda kugombea Uspika bali Wamuache amsaidie kazi Ikulu ya Kusimamia hawa Mawaziri Vijana aliowateua.

"Wengine wameanza kumletea [William Lukuvi] meseji za ajabu ajabu wakijua atagombea Uspika, hatogombea. Ana kazi na mimi. Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.kasema Rais Samia

Rais Samia amesema Kabudi atakuwa na Kazi moja tu Ikulu, Kusimamia kupitia na Kushughulikia Mikataba yote ambayo Serikali inaingia.

"Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki...Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba." amesema Rais Samia Suluhu

Amesema hizi kazi hazipo kwenye Muundo wa Serikali lakini anaona ni Msaada Mkubwa Kwake.

MY TAKE:

Je, Kassim Majaliwa na Mkuchika Wameshindwa kumsaidia rais? Kwanini Lukuvi na Kabudi wawe juu yao?

Kapteni George Huruma Mkuchika yeye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) na Waziri Mkuu ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Anawakilisha serikali katika bunge la taifa. Yuko chini ya mamlaka ya rais.
Kwa hiyo Kitila, Mwambe na Waitara ndio wasaliti kuelekea 2025?
 
Salaam Wakuu,

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi na Aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, wametakiwa kwenda Ikulu kumsaidia kazi Rais Samia ya kuwasimamia Mawaziri.
View attachment 2075769
Rais Samia kasema watu Wasimpake matope Lukuvi. Wala Wasimsingizie kwamba anaenda kugombea Uspika bali Wamuache amsaidie kazi Ikulu ya Kusimamia hawa Mawaziri Vijana aliowateua.

"Wengine wameanza kumletea [William Lukuvi] meseji za ajabu ajabu wakijua atagombea Uspika, hatogombea. Ana kazi na mimi. Kaka yangu Lukuvi, yeye ana kazi na mimi, mtaisikia baadaye. Lakini namvuta Ikulu, kazi yetu ni kuwasimamia nyinyi.kasema Rais Samia

Rais Samia amesema Kabudi atakuwa na Kazi moja tu Ikulu, Kusimamia kupitia na Kushughulikia Mikataba yote ambayo Serikali inaingia.

"Kabudi amefanya kazi nzuri sana kusimamia majadiliano ya serikali na mashirika, na ndiyo kazi ninayotaka nimkabidhi sasa kindakindaki...Mashirika yote, kazi zote zitakazoingia ubia na serikali, Kabudi ataongoza hiyo timu. Kwa hiyo yeye ni baba mikataba." amesema Rais Samia Suluhu

Amesema hizi kazi hazipo kwenye Muundo wa Serikali lakini anaona ni Msaada Mkubwa Kwake.
kazi ya lukuvi, waziri mkuu atafanya kazi gani au nayeye atakuwa chini yalukuvi? Kwa hii ya kabudi sawa, nashauri apitie na ile yenye viulizo ili kutoa sintofahamu
 
Walalamikaji pokeeni 💉💉💉🤣🤣🤣

Ila mliandika mengi haswa juu ya Kabudi.. kama nawaona mnatamani mjifukie na upinzani koko.. wa nchini🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Kazi iendelee...
 
Ameamua kuwaosha baada ya watu kuongea saana kwenue Mitandao ya kijamii! Kikubwa Mama ajaribu kupuuza mihemko ya watu wa mitandaoni itamharibia kama atakuwa kila kelele ya mtandaoni anataka kuitolea ufafanuzi! Sijaona haja ya kulisema hilo
Stop that thinking, mitandao Ni one great source of information kilichopo Ni kuchuja habari hizo by using common sense
 
Kweli Rais ana madaraka makubwa. Kwa hiyo anacreate ajira special kwa hawa wazee wawili. Halafu Samia yupo addicted na mitandao. Anasoma sana mitandao. Lukuvi atakuwa mshauri wa Rais ama?Kabudi tumeambiwa anaongonza majadiliano ya mikataba. Stupid.Wakifa na kaburini awafuate. Maana as if bila wao nchi haiendi. Stupid
Mbona umepanic kwani tatizo nini Rais apangiwi ujue
 
Samia mjanja sana hizi zote ni mbinu za kuelekea 2025, hao kawavuta karibu aangalie mienendo yao, vinginevyo atuambie hao jamaa wanaweza vipi kutimiza majukumu yao bila kuingiliana na mawaziri wa wizara husika, mamlaka yao ni yapi kwa sheria ipi?

Hizi kazi zisizo na kichwa wala miguu mwishowe mtu anaondolewa kimyakimya bila kuambiwa yeyote. Hili litafanyika baada ya lengo la kuingia ikulu 2025 kutimia, au kuonekana linakaribia kutimia.
 
.
20220110_125107.jpg
 
Tatizo la mama Samia anataka kumfuraahisha kila mtu! Hayuko tayari kufanya maamzi! Ndo tabia za watu wa pwani za unafiki! Amewatoa wa nini? Ikulu wanaenda kufanya nini? Ameongeza baraza la mawaziri la nini? Mzigo wa serkali ni mkubwa maana mawaziri na washauri ni wengi! Mama fanya maamzi bila kuwa accountable utapata taabu sana! Nakukumbusha huwezi kupendwa na kila mtu!
Waswahili shukrani huwa hamna hata kidogo. Ni kulalamika kwa kwenda mbele.
 
Ameamua kuwaosha baada ya watu kuongea saana kwenue Mitandao ya kijamii! Kikubwa Mama ajaribu kupuuza mihemko ya watu wa mitandaoni itamharibia kama atakuwa kila kelele ya mtandaoni anataka kuitolea ufafanuzi! Sijaona haja ya kulisema hilo
Umeumia baada ya kusikia hivyo?
 
Mwanasheria Mkuu wa serikali kazi yake ni ipi? Kabudi anaenda kua boss wa AG?
 
Huyu ndiye mwenye kazi ambayo Rais ataitangaza hivi karibuni, Kazi hiyo Mimi na wewe hatuijui huenda hi mpaka spika mpya atangazwe, huenda mpaka Bunge liridhie hiyo kazi mpya, huenda.....
 
Samia mjanja sana, hao kawavuta karibu aangalie mienendo yao, vinginevyo atuambie hao jamaa wanaweza vipi kutimiza majukumu yao bila kuingiliana na mawaziri wa wizara husika.
Vigezo na masharti kuzingatiwa.
Ujanja ndio Akili yenyewe.
 
Back
Top Bottom