Lupaso, Mtwara: Rais Mstaafu, Hayati Benjamin William Mkapa azikwa kwa Heshima
Labda ana tafuta atoke na kiki gani aje tu na wheelchair kiki hiyo itabamba!
 
ITV walionyesha picha ya gari la Chadema likiwa nje ya uwanja watu wamelizunguka na kukata picha/ilihitaji umakini sana kuweza kuigundua picha hiyo ni jambo ambalo lilichukua sekunde kadhaa tuu....
 
Duhhhh....
Nimasikia miakenda zaidi ya 17, bado naendelea kuzisikiliza miakenda
 
Hii kitu inanifikirisha hata mimi,
Nyerere anaenziwa sana Tz, ndie baba wa taifa letu haina ubishi lakini mbona watoto wake wametengwa? Sijasikia Waziri Nyerere wala RC Nyerere, kuna nini nyuma ya pazia?
Wajuvi mtujuze.
Kinachoniumiza hawa watawala wala hawawapi hata teuzi , yaan nabaki kushangaa tyuuh km sio kustaajabu.
 
Mkuu Roving Journalist ,kongole sana kwa kazi yako ya kutuhabarisha humu jukwaani. Kwa kweli unajitahidi sana sana kutupa kinachojiri kwenye matukio makubwa ya kitaifa yanayotokea huko nyumbani.

Umekuwa msaada mkubwa sana kihabari kwa sisi tulio mbali na nyumbani.

Mungu akubariki sana mkuu.
 
Duhhhh....
Nimasikia miakenda zaidi ya 17, bado naendelea kuzisikiliza miakenda
Profesa anashindwa kujua kuwa sio watanzania wote wanaoelewa, sana sana hata hawa wanafunzi waliotoa mashuleni waje hapa.

Hata kusoma ni shida, bora angepewa hata mwanafunzi wa sekondari asome huu wasifu.

Sent from my SM-G930F using JamiiForums mobile app
 
Wale wale wazungusha mikono. Kwani hujui nchi jirani wana lockdown.
Mgeni kutoka nje ya nchi tofauti na mabalozi ni Waziri Mkuu wa Burundi tu! Tatizo ni corona au diplomasia yetu imeshuka kiasi hiki? Tujitafakari na tujisahihishe!
 
Salaam Wakuu,

Leo ni siku ya Kwanza kati ya Tatu ya kuuaga Mwili wa Aliyekuwa rais wa Tanzania Benjamin Wiliam Mkapa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar Es Salaam.

Tutaendelea kujuzana kile Kinachojiri.

Stay tuned.



=====

UPDATES:

======

View attachment 1517152View attachment 1517154
0910hrs: Mwili wa Marehemu upo Njiani kutoka Hospitali ya Jeshi Lugalo kuelekea Uwanja wa Uhuru Temeke. Ambapo kazi hii inaongozwa na Jeshi la Ulinzi (JWTZ).

Mwili ukifika Uwanja wa Taifa, kutakuwepo na Misa itakayoongozwa na Askofu Tercius Ngalekumtwa.

0935hrs: Msafara wa Mwili wa rais Mstaafu Mkapa, bado upo njiani kutokea Jeshini Lugalo Kawe Dar Es Salaam kupitia barabara ya Hassan Mwinyi, Katikati ya Mji hadi Temeke.
View attachment 1517174
Kila Sehemu Msafara unapopita, Wananchi wamejipanga barabarani kuaga na kutoa heshima zao za mwisho.

0945hrs: Mwili Wa Marehemu Mkapa ndo unaingia Viwanja vya Uhuru Temeke
View attachment 1517216
View attachment 1517194
Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mama Anna Mkapa, akiwa tayari kwenye Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kushiriki Misa na kuuaga mwili wa Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa
View attachment 1517195
Rais Magufuli na Makamu wa Rais Samia Suluhu wakiwa tayari wamewasili katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Misa na kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.
View attachment 1517197
1000hrs: Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa ukishushwa kutoka katika Gari maalum ndani ya Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuanza kwa misa ya kumuaga.

WAKATI HUO HUO;
View attachment 1517198
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wakiendelea na shughuli ya ujenzi wa kaburi atakwamozikwa Rais Mstaafu, Marehemu Benjamin Mkapa.

Kiongozi huyo atazikwa kijijini kwao Lupaso, mkoani Mtwara, Julai 29 mwaka huu.

Shughuli za kuuaga mwili wake zinaendelea Dar es Salaam.

1140HRS: Ibada ya kuaga Mwili wa rais Mstaafu Benjamin Mkapa inaelendelea Uwanja wa Uhuru.

MSEMAJI WA FAMILIA: RAIS MKAPA ALIKUTWA NA MALARIA

William Erio, Msemaji wa familia amesema Rais Mstaafu Benjamini Mkapa alipatwa na Malaria Jumatano na akalazwa na kuanza matibabu

Siku ya alhamisi alikuwa anaendelea vizuri, na akaendelea kufuatilia uchaguzi wa kura za maoni uliokuwa unaonyesha mubashara

Baada ya muda, aliinuka alitaka kutoka, alivyoinuka akarudi kukaa na akainamisha kichwa, na akathibitika amefariki kwa mshituko wa moyo, ‘Cardiac arrest’

Msemaji wa familia amewataka watu kuheshimu ukweli huo, na sio kuzusha mambo yasiyo na ukweli kwenye mitandao.

KASEMA;

"Nitoe shukrani kwa Serikali kwa ambavyo wamekuwa pamoja nasi na kushughulikia msiba huu na wanavyoendelea kushughulikia, tunawashukuru kwa uamuzi wa kuanza shughuli ya kuaga kwa Misa Takatifu, tunawashukuru Maaskofu kwa kukubali kuendesha Misa”- William Urio,

“Mzee Mkapa alikuwa hajisikii vizuri akaenda Hospitali akaonekana alikuwa na Malaria akaanza matibabu akalazwa Jumatano,Alhamisi mchana aliendelea vizuri nilikuwa nae hadi saa mbili alikuwa anaangalia Live ya chaguzi za wagombea Ubunge Viti Maalum CCM”-

“Mzee Mkapa Alhamisi usiku baada ya kutazama LIVE ya chaguzi Viti Maalum akasikiliza taarifa ya habari, baadaye aliinuka akitaka kutoka akakaa akainamisha kichwa, walipokuja kumpima wakathibitisha kuwa amefariki, sababu ya kifo cha Mzee Mkapa ni mshtuko wa moyo”-

“Chanzo cha kifo cha Mkapa alipata mshtuko wa moyo, tumeona ni vizuri tuliseme hili kwasababu kumeanza kuwa na manenomaneno kila Mtu akijifanya Nabii katika mitandao ya kijamii na kwingine, tumuenzi Mzee wetu aliyetangulia mbele za haki kwa kuukubali ukweli huo"


View attachment 1517651View attachment 1517650
PICHA: Kutoka Uwanja wa Uhuru DSM ambako imefanyika Misa Takatifu ya kuuaga mwili wa Marehemu Mzee Mkapa kisha Watanzania mbalimbali kupata nafasi ya kupita karibu na Jeneza na kutoa heshima zao za mwisho, haya ndio matukio mbalimbali ya picha uwanjani.

yote sawa ila IBADA YA WAFU mungu amekataa.
 
Huyu waziri mkuu Burundi atakuwa aliishi Tanzania. Maana anaongea kiswahili cha Tanzania kabisa.
 
ITV walionyesha picha ya gari la Chadema likiwa nje ya uwanja watu wamelizunguka na kukata picha/ilihitaji umakini sana kuweza kuigundua picha hiyo ni jambo ambalo lilichukua sekunde kadhaa tuu....
Ha ha haaaa yani wameogopa wangeendelea kulionyesha hilo gari Abbas i angewashuhulikia
 
Hii hapa

wanafunzi.jpeg

Wanafunzi uwanja wa Uhuru 28/7/2020​
 
Back
Top Bottom