Maafisa uhamiaji Walivyomtesa mtuhumiwa, Je, Sheria inawaruhusu?

Raia tunawalalamikia Maafisa wa Uhamiaji kwamba wanachelewesha huduma na wanakula Rushwa Leo hii wanabaini mla Rushwa kwa mwamvuli wa jina la wapambana na Rushwa then tunaangalia adhabu.

Kuhusu adhabu hii ni adhabu ambayo hata ukikamatwa lugalo leo wanafuata mbinu hizo kwa sababu jukumu la Kwanza la Askari nikulinda kikosi au eneo lake la kazi

Hakuna anayemuhurumia huyo mwanamke aliyekodi tax kumbe dreva tax ni tapeli, Nani anajua Kama wangefanikiwa usalama wa huyo mwanamke ungekuwa Nini? Let assume angembaka au akamtaka kimapenzi Kama fidia ya huduma aliyompa? Je angeenda kumuua?

Lakini pia tukumbuke hayo maeneo ya vituo vya polisi Kuna silaha na mambo mengine, je wamkamate askari mamluki ndani ya ofisi zao au vituo vyao wamwache kisa Kuna mahakama?

Kama alitoroka mikononi mwa Askari Kama inavyodaiwa je angekuwa na silaha hao askari wangebaki salama ?

Lakini pia kwa sisi tuliopita JKT miaka hiyo ya 1990 tulifundishwa kwamba kazi ya Askari ya Kwanza siyo kutoa huduma nikudhibiti ualifu! Mbinu mojawapo yakudhibiti ualifu siyo lele mama lazima nguvu ya ziada itumike ikiwemo mazoezi Kama aliyopewa kijana wetu hapo ambayo kwa watu lele mama wanaona kuwa ni adhabu kumbe Ni kumshusha pumzi mjinga huyu wa kihaya anayeneemeka kwa kutapeli watu. Bila kufanya hivi hakuna tofauti ya kituo Cha Polisi na msala wa stendi ambao unaweza ukijiingilia unavyotaka

Lakini pia tujiulize huyu mtu angekutana na wewe akataka kukutapeli let say yupo ndani ya fensi ukamshtukia angekuacha au angekuua? Na je ili kupambana naye ungesema tusubiri polisi waje wamkamate ndipo rule of law ifuate au ungepiga kelele wananchi watusaidie? Je wananchi wangetumia rule of law kumdhibiti? Kwa mfano huo huo tambua ofisi za umma zinakaliwa na binadamu wenye mifumo ileile ya raia yakumdhibiti mualifu, wao wamemwagia maji ila uraia angepigwa mapanga au kupigwa mawe

Jambo jingine, vijana wamechukua kauli ya rule of law Kama njia yakufanyia ualifu,.Kesi zinakwenda mahakamani zinamaliza miaka hakuna anayesikiliza wanapanga tarehe, kurekebisha mfumo lazima mambo yafuatayo yafanyike
1. Lazima wananchi waheshimu ofisi na vituo vya polisi na kuingia kwa nidhamu wakijua waliopo huko wapo kulinda uhai wao masaa yote.
2. Lakima tukubali kwamba si watu wote wanaokuja kwetu kama Askari ni askari wengine Ni majambazi na lazima tujifunze kuwatambua watu kabla ya kuwaamini
3. Tuache njia za mkato kutafuta huduma, tumewalea Hawa watu kwa sababu tunajua siyo maafisa wa serikali lakini tunawapa taarifa zetu wanatutumia wapendavyo na hata kutumia mwanya huo kutujua nakutuandalia mazingira ya uvamizi.
4. Tusiwaamini madreva tax nakuwa na namba zao Hadi kuwakaribisha ndani nakukujua kiundani, nafsi zao zimejaa mengi na niwachora dili wakubwa. Wanakupeleka benki usiwaambie naenda benki maana upo kwenye ATM wao wanakuitia kikosi kije kukumaliza.

Tusitetee ualifu kijana amefundishwa kwamba muda wa kutojulikana na kuwa na watu Kama walinzi wa sabaya umekwisha. Sasa hivi ukimzingua mama anakuzingia na ukiwazingua walinzi wetu wanakuzingua ili kesho wenzio waone kituo Cha Polisi Kama ziwa la moto
 
Unadanganya hadharani?takukuru bandia unajua ni kosa la jinai?Tena uhamiaji?huyu angepewa choice angesema arushwe kichura aende kwake!Baada ya yale walitakiwa wamsamehe ingestahili.
Kama amedanganya hadharani kwa maana ya ofisi ya uhamiaji, wajibu wenu ni kumkamata kufahamisha kosa lake, kwa ushahidi mlionao mnamfikisha mahakamani, huko ndiko kwenye Mamlaka za kutoa adhabu, sio nyie uhamiaji.... Mmetenda kosa, ni sharti muadhibiwe pia.
 
Hapana Huyu jamaa nimesoma naye na ni afisa serikalini kuna kitu kinaitwa rights of the accused, rights to be heard...ndiyo mana kuna mahakama...tusiingiliane kimajukumu
Yeye ameridhika na adhabu aliyopewa mkuu!
 
huyu jamaa naye sijui yukoje anakubaliaje huu ujinga si bora hata mtu apigwe hadi kufa lakini sio huu ujinga,nilijua hata badaya hapo ameadhibiwa anaondoka eti kapigwa bingu tena kwaiyo hapo amefanya kazi bure sio sawa mhe rais kazi kwako ,mtu kama amekosea sheria ndio imushuglikie .
 
Askari wa Uhamiaji wamemuadhibu mtu kwa kumgalalaza kwenye matope kwa kumtuhumu kuwa amesema uongo kitendo ambacho ni kinyume cha sheria! Uhamiaji wamechukua sheria mkononi badala ya kumfikisha mahakamani!

Raia tunawalalamikia Maafisa wa Uhamiaji kwamba wanachelewesha huduma na wanakula Rushwa Leo hii wanabaini mla Rushwa kwa mwamvuli wa jina la wapambana na Rushwa then tunaangalia adhabu.

Kuhusu adhabu hii ni adhabu ambayo hata ukikamatwa lugalo leo wanafuata mbinu hizo kwa sababu jukumu la Kwanza la Askari nikulinda kikosi au eneo lake la kazi

Hakuna anayemuhurumia huyo mwanamke aliyekodi tax kumbe dreva tax ni tapeli, Nani anajua Kama wangefanikiwa usalama wa huyo mwanamke ungekuwa Nini? Let assume angembaka au akamtaka kimapenzi Kama fidia ya huduma aliyompa? Je angeenda kumuua?

Lakini pia tukumbuke hayo maeneo ya vituo vya polisi Kuna silaha na mambo mengine, je wamkamate askari mamluki ndani ya ofisi zao au vituo vyao wamwache kisa Kuna mahakama?

Kama alitoroka mikononi mwa Askari Kama inavyodaiwa je angekuwa na silaha hao askari wangebaki salama ?

Lakini pia kwa sisi tuliopita JKT miaka hiyo ya 1990 tulifundishwa kwamba kazi ya Askari ya Kwanza siyo kutoa huduma nikudhibiti ualifu! Mbinu mojawapo yakudhibiti ualifu siyo lele mama lazima nguvu ya ziada itumike ikiwemo mazoezi Kama aliyopewa kijana wetu hapo ambayo kwa watu lele mama wanaona kuwa ni adhabu kumbe Ni kumshusha pumzi mjinga huyu wa kihaya anayeneemeka kwa kutapeli watu. Bila kufanya hivi hakuna tofauti ya kituo Cha Polisi na msala wa stendi ambao unaweza ukijiingilia unavyotaka

Lakini pia tujiulize huyu mtu angekutana na wewe akataka kukutapeli let say yupo ndani ya fensi ukamshtukia angekuacha au angekuua? Na je ili kupambana naye ungesema tusubiri polisi waje wamkamate ndipo rule of law ifuate au ungepiga kelele wananchi watusaidie? Je wananchi wangetumia rule of law kumdhibiti? Kwa mfano huo huo tambua ofisi za umma zinakaliwa na binadamu wenye mifumo ileile ya raia yakumdhibiti mualifu, wao wamemwagia maji ila uraia angepigwa mapanga au kupigwa mawe

Jambo jingine, vijana wamechukua kauli ya rule of law Kama njia yakufanyia ualifu,.Kesi zinakwenda mahakamani zinamaliza miaka hakuna anayesikiliza wanapanga tarehe, kurekebisha mfumo lazima mambo yafuatayo yafanyike
1. Lazima wananchi waheshimu ofisi na vituo vya polisi na kuingia kwa nidhamu wakijua waliopo huko wapo kulinda uhai wao masaa yote.
2. Lakima tukubali kwamba si watu wote wanaokuja kwetu kama Askari ni askari wengine Ni majambazi na lazima tujifunze kuwatambua watu kabla ya kuwaamini
3. Tuache njia za mkato kutafuta huduma, tumewalea Hawa watu kwa sababu tunajua siyo maafisa wa serikali lakini tunawapa taarifa zetu wanatutumia wapendavyo na hata kutumia mwanya huo kutujua nakutuandalia mazingira ya uvamizi.
4. Tusiwaamini madreva tax nakuwa na namba zao Hadi kuwakaribisha ndani nakukujua kiundani, nafsi zao zimejaa mengi na niwachora dili wakubwa. Wanakupeleka benki usiwaambie naenda benki maana upo kwenye ATM wao wanakuitia kikosi kije kukumaliza.

Tusitetee ualifu kijana amefundishwa kwamba muda wa kutojulikana na kuwa na watu Kama walinzi wa sabaya umekwisha. Sasa hivi ukimzingua mama anakuzingia na ukiwazingua walinzi wetu wanakuzingua ili kesho wenzio waone kituo Cha Polisi Kama ziwa la moto
Nimewahi kukuta mawazo ya kishenzi na ya kipumbavu lakini haya ya kwako yametia fora. Bila shaka na wewe ni moja katika walioshangilia kutekwa, kuteswa na kuuawa kwa wananchi katika utawala wa kikatili uliopita ambao tunajitahidi kuusahau. Washamba na limbukeni waliokuwa na mambo hayo ya kishenzi waliishi wakati wa zama za mawe, shenzi waahed!

Kama sheria zetu za namna ya kushughulikia wahalifu unadhani zina mapungufu, una haki ya kudai zibadilishwe ili kuziba mianya inayowezesha wahalifu kutopata hukumu stahili. Chini ya mwendazake wapumbavu kama wewe ndio walikuwa wanapiga vigelegele pale Katiba ilipokuwa ikisiginwa eti kwa kisingizio cha maendeleo. Amka, tuko katika karne ya ishirini na moja.
 
Hii imekaa vizuri sana, wapo watu wameanza kudharau mamlaka za serikali kisa tu JPM hayupo. Huyu Kama ameweza kuingia ofisi nyeti hivyo nakudanganya eti anatoka TAKUKURU ameshadhulumu watu wangapi? Yawezekana huyu mtu ni jambaza au muhalifu ni vyema tukapata taarifa rasmi.

Kuingia kwenye vyombo Kama TAKUKURU ukijua siyo mtumishi wa chombo hicho then utegemee kutoka salama hicho chombo kitakuwa kimekufa.

Hawa watu ndiyo wanaotuibia kwa sms za namba zisizofahamika. Na wakikukamata usiku ndo utajua haki za binadamu au la.

Vibaka wamezagaa kila kona imefika wakati Sasa wanajitutumia Hadi kwenye vyombo vya dola, no. Vyombo vyetu vijiimarishe kuwashughulikia Hawa watu la sivyo wakiruhusiwa kutetewa tutawapa kiburi.

Mtu hata bia haishuki kisa vibaka Kama Hawa, juzi wamepiga mtu mbezi mara kituo Cha mafuta wamenyang'anya silaha......kwanini haya yatokee Kama siyo kujaribu nguvu ya utawala mpya
Huyo ni masalia ya wasiojulikana.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Hii mada tumeijadili humu kutwa nzima ya leo? Umechekewa wapi mkuu? Kwahiyo huu uzi utafutwa ama kuunganishwa.
Quote
 
Hata kama kungekuwa na uhakika, sheria imeweka utaratibu kwa mtu anayedhaniwa kutenda kosa la jinai na haikuweka utaratibu wa kwamba mtu akikamatwa kwa kudhaniwa amefanya kosa fulani la jinai atapelekwa kwa vyombo husika ili achukuliwe hatua za kisheria. Kujichukulia sheria mkononi hasa kwa watumishi wa serikali ni precedent mbaya kwa raia wa kawaida kufuata sheria. Kwa maoni yangu wote walioshiriki kufanya hivyo wanapaswa wachukuliwe hatua za kisheria, ikiwa ni pamoja na mtu aliyeteseswa ingawa nadhani kwamba atakuwa anahukumiwa kwa mara ya pili - kwa kuteswa na baadaye kushtakiwa na akipatikana na kosa kulipa faini au kufungwa au vyote viwili.
 
Hao maofisa wamekosea kuachia sura zao zionekane, inaweza ikawacost jamaa akiamua kwenda mahakamani.
Lakini kibaka hapaswi huruma, hapo ana bahati hakuchezea kichapo.
 
Alipenda mwenyewe kufanya adhabu anayo haki ya kukataa sema siku zote ukishafumaniwa huna nguvu
 
Hao maofisa wamekosea kuachia sura zao zionekane, inaweza ikawacost jamaa akiamua kwenda mahakamani.
Lakini kibaka hapaswi huruma, hapo ana bahati hakuchezea kichapo.
Zinaitwa sifa za kijinga badala ya kuangalia maisha yako unatafuta sifa,yalifaa awamu iliyopita na vyeo wangepewa
 
Back
Top Bottom