Raia tunawalalamikia Maafisa wa Uhamiaji kwamba wanachelewesha huduma na wanakula Rushwa Leo hii wanabaini mla Rushwa kwa mwamvuli wa jina la wapambana na Rushwa then tunaangalia adhabu.
Kuhusu adhabu hii ni adhabu ambayo hata ukikamatwa lugalo leo wanafuata mbinu hizo kwa sababu jukumu la Kwanza la Askari nikulinda kikosi au eneo lake la kazi
Hakuna anayemuhurumia huyo mwanamke aliyekodi tax kumbe dreva tax ni tapeli, Nani anajua Kama wangefanikiwa usalama wa huyo mwanamke ungekuwa Nini? Let assume angembaka au akamtaka kimapenzi Kama fidia ya huduma aliyompa? Je angeenda kumuua?
Lakini pia tukumbuke hayo maeneo ya vituo vya polisi Kuna silaha na mambo mengine, je wamkamate askari mamluki ndani ya ofisi zao au vituo vyao wamwache kisa Kuna mahakama?
Kama alitoroka mikononi mwa Askari Kama inavyodaiwa je angekuwa na silaha hao askari wangebaki salama ?
Lakini pia kwa sisi tuliopita JKT miaka hiyo ya 1990 tulifundishwa kwamba kazi ya Askari ya Kwanza siyo kutoa huduma nikudhibiti ualifu! Mbinu mojawapo yakudhibiti ualifu siyo lele mama lazima nguvu ya ziada itumike ikiwemo mazoezi Kama aliyopewa kijana wetu hapo ambayo kwa watu lele mama wanaona kuwa ni adhabu kumbe Ni kumshusha pumzi mjinga huyu wa kihaya anayeneemeka kwa kutapeli watu. Bila kufanya hivi hakuna tofauti ya kituo Cha Polisi na msala wa stendi ambao unaweza ukijiingilia unavyotaka
Lakini pia tujiulize huyu mtu angekutana na wewe akataka kukutapeli let say yupo ndani ya fensi ukamshtukia angekuacha au angekuua? Na je ili kupambana naye ungesema tusubiri polisi waje wamkamate ndipo rule of law ifuate au ungepiga kelele wananchi watusaidie? Je wananchi wangetumia rule of law kumdhibiti? Kwa mfano huo huo tambua ofisi za umma zinakaliwa na binadamu wenye mifumo ileile ya raia yakumdhibiti mualifu, wao wamemwagia maji ila uraia angepigwa mapanga au kupigwa mawe
Jambo jingine, vijana wamechukua kauli ya rule of law Kama njia yakufanyia ualifu,.Kesi zinakwenda mahakamani zinamaliza miaka hakuna anayesikiliza wanapanga tarehe, kurekebisha mfumo lazima mambo yafuatayo yafanyike
1. Lazima wananchi waheshimu ofisi na vituo vya polisi na kuingia kwa nidhamu wakijua waliopo huko wapo kulinda uhai wao masaa yote.
2. Lakima tukubali kwamba si watu wote wanaokuja kwetu kama Askari ni askari wengine Ni majambazi na lazima tujifunze kuwatambua watu kabla ya kuwaamini
3. Tuache njia za mkato kutafuta huduma, tumewalea Hawa watu kwa sababu tunajua siyo maafisa wa serikali lakini tunawapa taarifa zetu wanatutumia wapendavyo na hata kutumia mwanya huo kutujua nakutuandalia mazingira ya uvamizi.
4. Tusiwaamini madreva tax nakuwa na namba zao Hadi kuwakaribisha ndani nakukujua kiundani, nafsi zao zimejaa mengi na niwachora dili wakubwa. Wanakupeleka benki usiwaambie naenda benki maana upo kwenye ATM wao wanakuitia kikosi kije kukumaliza.
Tusitetee ualifu kijana amefundishwa kwamba muda wa kutojulikana na kuwa na watu Kama walinzi wa sabaya umekwisha. Sasa hivi ukimzingua mama anakuzingia na ukiwazingua walinzi wetu wanakuzingua ili kesho wenzio waone kituo Cha Polisi Kama ziwa la moto