Maaskofu wa Katoliki wakataa mchango wa Shilingi milioni 5.6 kutoka kwa Ruto kwa kanisa la Soweto
Michango ya Mama yule hasa kwenda Katoliki imekuwa mingi sana siku za hivi karibuni, why kwenda Katoliki pekee?

TEC na KKKT bila aibu wanaipokea hiyo michango kila siku ..... halafu pembeni unawasikia TEC wanabwabwaja.
 
Kama wamejielewa na kuanza kujirudi ni uamuzi sahihi maana hali ingezidi kuwa mbaya kwao na kwa wafuasi wa ukristo.
Hatahivyo wamechelewa sana,walijiingiza wenyewe kumpigia debe ruto nchi nzima kwa kumwita chaguo la Mungu,sasa wanauliuzwa huyo mliyesema ni chaguo la Mungu kawa muongo tena?
 
Maaskofu hao wamedema sio sawa Kwa Wanasiasa kugeuza mimbari za kanisa kama majukwaa ya kujinadi kisiasa na kwamba pesa hizo za Wanasiasa ni hongo.

Ikumbukwe wiki Viongozi hao wa Kanisa la RC La Kenya walimshitumu Rais Ruto na kuwataka waumini wao Wasimchague tena Kwa kipindi Cha pili Cha Uongozi.

View: https://www.instagram.com/p/DCi-XZ8o3lh/?igsh=c3JxNDd2ZzNsNXll

My Take
Sio sawa Kwa Watu wa dini kutumia majukwaa ya dini kutoa maelekezo ya Kisiasa Kwa waumini kama ilivyo sio sawa Kwa Wanasiasa.
 
Kwa Tanzania hakuna wa kukata pesa ila Kanisa la Papa Huwa linatumika kukandamiza Viongozi (Rais ) ambae hajatokea kwenye Kanisa lao.
 
Kanisa Katoliki la Kenya limeamua kurudisha mchango wa pesa uliotolewa na Rais Ruto kwa kanisa hilo uliolenga kujenga nyumba ya padre.

Askofu mkuu wa Nairobi, Phillip Anyolo amesema mchango huo wa dola 40,000, sawa na zaidi ya TZS 108,000,000, wataurudisha kwa Rais Ruto, na kwamba hawahitaji mchango mwingine wowote kutoka kwa Rais Ruto kwa sababu michango hiyo ina harufu ya kutafuta manufaa ya kisiasa.

Askofu Mkuu, Anyolo amesema kuwa pia mchango wa shilingi za Kenya 200,000, nao utarudishwa.

Swali la kujiuliza, kwa hapa Tanzania, kwa mara ya kwanza, Rais amegawa pesa nyingi kwa makanisa, kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya Tanzania, viongozi wetu wa dini hawana macho ya kuona kama hao wenzao wa Kenya? Au wanaamini kuwa michango hiyo inatolewa kwa roho tu ya huruma? Kwa nini itolewe sana kipindi hiki?

Habari hii hapa:

Catholic Church rejects $40,000 from Kenya's president.​

president
Kenya’s Catholic Church has rejected a donation of about $40,000 (£32,000) made by President William Ruto.
He offered the money towards the building of a priest’s house and as a gift to the choir during Mass on Sunday at the Soweto Catholic Church in the capital, Nairobi.

The Catholic Archbishop of Nairobi, Philip Anyolo, said the cash would be returned over "ethical concerns and the need to safeguard the Church from being used for political purposes".

He also declined his other pledges and said a donation of 200,000 Kenyan shillings made by the Governor of Nairobi, Johnson Sakaja - who attended the same service, was also being handed back.

Source: BBC
 
Habari imfikie Bi.Mkubwa na Askafu Shoo na wengineo wenye tabio za Askofu Shoo hata kama ni wa dhehebu au dini tofauti.
 
Hatahivyo wamechelewa sana,walijiingiza wenyewe kumpigia debe ruto nchi nzima kwa kumwita chaguo la Mungu,sasa wanauliuzwa huyo mliyesema ni chaguo la Mungu kawa muongo tena?
Hali ngumu wamejua kuna namna haikuwa vile walivyodhania.
 
Kanisa Katoliki nchini Kenya limekataa mchango wa takriban $40,000 (£32,000) uliotolewa na Rais William Ruto.

Alitoa pesa hizo kwa ujenzi wa nyumba ya kasisi na zawadi kwa kwaya wakati wa Misa ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la Soweto katika mji mkuu, Nairobi.

Msaada huo ulifuatia kauli ya hivi majuzi ya maaskofu wa Kanisa Katoliki, walioisuta serikali kwa kushindwa kutekeleza ahadi zao za uchaguzi.

Makanisa yamekuwa chini ya shinikizo mwaka huu kutoka kwa vijana wanaopinga nyongeza ya ushuru ambao wamewashutumu kwa kuwa karibu sana na wanasiasa.

Kufuatia mchango wa Ruto uliotangazwa sana Jumapili, Wakenya wengi walihimiza Kanisa Katoliki kukataa pesa hizo.

Rais alikuwa ametoa takriban shilingi milioni 2.6 za Kenya ($20,000, £16,000) taslimu, aliahidi pesa zilizosalia baadaye na pia aliahidi kuipa parokia hiyo basi.

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki la Nairobi, Philip Anyolo, alisema pesa hizo zitarejeshwa kwa sababu ya "masuala ya kimaadili na hitaji la kulinda Kanisa dhidi ya kutumiwa kwa madhumuni ya kisiasa".

Pia alikataa ahadi zake nyingine na kusema mchango wa shilingi 200,000 za Kenya uliotolewa na Gavana wa Nairobi, Johnson Sakaja - ambaye alihudhuria ibada hiyo hiyo, pia ulikuwa unarudishwa.

"Kanisa Katoliki linakataza vikali matumizi ya hafla za kanisa kama vile kuchangisha pesa na mikusanyiko kama majukwaa ya kujitangaza kisiasa," Askofu Mkuu Anyolo alisema.

Michango kama hiyo ilikiuka maagizo ya kanisa pamoja na sheria ya Kenya, aliongeza.

Uhusiano wa muda mrefu kati ya makanisa na taasisi za kisiasa - katika nchi ambayo zaidi ya 80% ya wakazi ni Wakristo - inaonekana kuyumba.

Miaka mitatu iliyopita, makanisa yaliyoanzishwa yalipiga marufuku wanasiasa kutumia mimbari wakati wa ibada kwa malipo ya michango.

Lakini uhusiano huo bado ulionekana kuwa wa karibu - huku waandamanaji vijana wakishutumu makanisa kwa kuegemea upande wa serikali ilipoamua kutoza ushuru mpya mapema mwaka huu.

Chini ya alama ya reli ya mtandao wa kijamii #OccupyChurch, wengi walikashifu makanisa kwa kukosa kuwa upande wao wakati wa maandamano mabaya yaliyozuka kujibu nyongeza ya kodi iliyopangwa.

Ghasia hizo ziliilazimu serikali ya Rais Ruto kuondoa mswada wa fedha uliokumbwa na utata mwezi Julai.
 
"....na ukitoa sadaka kwa mkono wa kulia, basi mkono wako wa kushoto usijue mkono wa kulia umetoa sadaka gani..."

Hapo sijuhi kwenye biblia Mungu alikuwa ana maana gani?

Willy angemuuliza Rugemalila WA Tanzania alifanyaje kuwapa mamilioni ya pesa akina Askofu Kilaini!
 
Kanisa katoliki kenya lakataa milion 5 ya Rais Ruto
IMG-20241119-WA0011.jpg
 
Viongozi wa Kikristu nchini Kenya wamerudisha Ksh. Million 5 kwa madai kuwa hawataki kutumiwa na Wana siasa. Na wamesema hata wakiitwa Ikulu hawahitaji chai wala maji bali wanahitaji kuheshimiwa km viongozi wa dini.

Je kwa maamuzi haya ya viongozi wa kidini nchini Kenya, wale wa upande wa Tanzania wanajufunza nini. Je viongozi wa kidini nchini Tz wanaweza kufanya maamuzi km haya.

Kenya is next level ktk kujitambua.
 
Mbona mnasahau nyaraka zenye nondo kali za TEC na KKKT/CCT? Hao wa kenya huenda wameiga misimamo ya viongozi wa dini wa Tanzania
 
Sawa n wakati wa Chadema kuitumia kupata credits
 
Kanisa ni moja tu katoriki lenye mizizi zaidi ya serikali
 
Hao watakuwa wameiga misimamo ya maaskofu wa RC Tanzamia/TEC na nyaraka zao kwa serikali
 
Back
Top Bottom