Maaskofu walikuwa wapi wakati J. K. Nyerere mara kadhaa baada ya kustaafu alikuwa akishauri serikali ya Mwinyi? Warioba (mstaafu)je?

Mizoga yote sasa ikpo jukwaani; kwa hiyo uvundo unakuwa ni mkali kabisa: huku yupo Tlaatlaah,; pale mzoga Kavulata na Stuxnet; na wewe hapa kwa nafasi yako ya uongozi wa timu ya mizoga inayonufaika kutokana na Genge?

Kikwete ni mhujumu mkubwa wa nchi hii, na wewe hili unalijuwa vyema tokea kwenye nafasi zote alizowahi kuzishika kiuongozi. Sasa ni kama anajiona kuwa kachelewa kuliangamiza taifa hili moja kwa moja, kwa hiyo anahaha amalize kazi kabla uhai wake haujafikia kikomo.
Nenda kamshauri, kwa vile unajiona unaye ukaribu naye; kwamba hata hiyo heshima ndogo aliyojiwekea kwa baadhi ya mizoga ya aina yako (kwa sababu zijulikanazo), nayo itayeyuka. Atapoteza kila kitu.
Punguza chuki zinautesa moyo wako. Weka ushahidi wa moja kwa moja wenye kuweza kukusaidia ukaeleweka mbele ya watu wenye uelewa na wastaarabu, unaomuunganisha JK na hizo tuhuma kuliko haya maneno ya kitoto kwamba ni mhujumu.

Chuki inapokaa moyoni mwa mtu kwa miaka mingi hata siku moja haiwezi kumfundisha wema, itampeleka kule kule katika kuwaza ubaya usio na sababu. Njoo na ushahidi kamili sio kutegemea hizi hisia.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Hivi unafuatilia kweli jinsi mambo yanavyoenda au upo kishabiki zaidi? Angalia Rasilimali zetu jinsi zinavyobufaisha Watu wachache hasa wageni, sehemu muhimu kama Bandali unawapaje wageni ili waendeshe?

Leo hii sekta ya Madini wanufaika wakubwa ni wageni ukiacha huyu Rostam Aziz ambaye naye huwezi kusema kwa asilimia zote kuwa ni Mtanzania.

Wananchi wa hali ya chini wanatozwa Tozo za kila aina ikiwemo kwenye Miamala na LUKU, lakini Matajili wakubwa kama GSM wanapewa msamaha wa Kodi.

Demokrasia imeminywa, Mtu akikosoa tu Serikali anawekewa vikwazo vya kila aina ikiwemo kufunguliwa kesi, kufungiwa Biashara na hata kutekwa na kuuawa.

Hayo ni machache tu, labda useme hayo mafanikio yapo kwenye sekta ipi? Tofauti na hapo labda wewe pia ni mnufaika wa haya yanayoendelea.

Binafsi huwa sibagui Mtu kutokana na jinsia yake au dini yake, suala la jinsia ya Mtu au dini linahusiana vipi na uwezo wa Mtu kuongoza?
Wakati JPM alipokuwa rais mlikuja na vilio vingi vya aina hii. Samia anahitaji kuheshimiwa kaifungua nchi kiuchumi kwa kuangalia ni kwa namna gani rasilimali zinavyoweza kuiongezea Tanzania mapato makubwa kuliko yaliyokuwa yakipatikana katika awamu zilizopita.

Suala la bandari tafuta mtu mwenye uelewa mpana akupe shule ya kueleweka ili uondokane na kuishi na dhana nyingi potofu na za kimtaani. Bandari chini ya DPW pato lake limeongezeka zaidi ya mara mbili kulinganisha na hali ilivyokuwa kabla ya kuja kwa huo uwekezaji.

Tukumbuke zile kebehi za Paul Kagame kwamba anaweza kuifanya Tanzania ikaishi kwa kujitegemea kwa kuituma bandari peke yake, Samia kazifanyia kazi kejeli zile na hivi sasa hakuna tena upigaji wa kipuuzi kutoka kwa watanzania wenzetu walioneemeka huku maslahi yetu halisi yakitelekezwa.

Hakuna namna nchi inaweza kusogea mbele bila ya kuwepo kwa tozo za aina mbalimbali. Dunia nzima inategemea kodi za aina tofauti kwa uchumi kuweza kusogea mbele. Nenda kaulize TRA kwa mwezi hivi sasa wanakusanya shilingi ngapi.

Kutekwa na kunyanyaswa kumekuwepo tangu awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere tofauti ni kwamba hivi sasa teknolojia ya habari imekua sana, hakuna siri tena kama miaka ile ya nyuma. Wakati wa Mkapa aliuliwa boss wa TISS Amrani Kombe na wasiojulikana hakuna cha ajabu kuona unyama ukiendelea kufanyika. Kwa taarifa yako sehemu ya Novena iliyosaliwa na kanisa katoliki kwa wiki nzima mpaka jumapili ya juzi inahusiana na suala zima la utekwaji wa watu.

Sekta nyingi sana zinapiga hatua kwa sasa. Viwanja vya ndege vinaendelea kukarabatiwa kwa kasi kubwa. SGR inakaribia kumaliziwa kule Kigoma, daraja la Busisi limekwisha kumalizika kujengwa, yapo mengi sana yanafanyika kwa kasi kubwa.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Punguza chuki zinautesa moyo wako. Weka ushahidi wa moja kwa moja wenye kuweza kukusaidia ukaeleweka mbele ya watu wenye uelewa na wastaarabu, unaomuunganisha JK na hizo tuhuma kuliko haya maneno ya kitoto kwamba ni mhujumu.

Chuki inapokaa moyoni mwa mtu kwa miaka mingi hata siku moja haiwezi kumfundisha wema, itampeleka kule kule katika kuwaza ubaya usio na sababu. Njoo na ushahidi kamili sio kutegemea hizi hisia.
Unapenda sana kulitumia hilo neno "chuki", na nilishakwambia karibu mara saba juu ya hiyo unayoiita wewe chuki.

Kiukweli wenye chuki ni watu kama nyinyi, mnapoamua kujiona ni kundi maalum juu ya waTanzania wenzenu wote na kufanya matakwa yenu ndiyo yawe kipaumbele cha matendo yenu.

Ukiniona mimi kuwa na chuki na nyinyi, elewa ni kwa misingi hiyo ya nyinyi kujifanya kuwa juu ya taifa hili. Kwangu mimiyeyote anayesigina maslahi ya nchi hii nitamchukia. Ndiyo ninayo chuki na Samia Suluhu Hassan, kwa sababu halitakii taifa hili mema. Sasa unataka nimpendee kitu gani, imani yake au makombo anayoweza kunitupia ninyamaze? Hilo haliwezekani.
 
Weka ushahidi wa moja kwa moja kuhusiana na usiginaji wa mali za taifa. Vinginevyo huna tofauti na Mange Kimambi anayepewa umbea na yeye moja kwa moja anakwenda hewani bila ya ushahidi wa hicho anachokwenda kukisema mbele ya watu.

Samia anafanya mengi ya maana, anamalizia viwanja vya ndege vyote alivyoachiwa na JPM vikiwa vimejengwa nusu.

Anaendeleza manunuzi ya ndege na shirika linaendelea kusimama kiuchumi. Huko TPA mapato yameongezeka na urasimu umepungua.

Haya yote ni ya dhahiri sio sawa na hizo ngonjera za maneno ya roho mbaya unayoyajaza humu JF.
 
Yoote haya tulisha yajadili tokea nilipokuwa nadhani najadili na mtu mwenye akili timamu, lakini bado unarudiarudia na kutaka nikupe ushahidi. Kama tabia ya namna hii siyo ya kimzoga itakuwa ni kitu gani sasa? Huoni kuwa umenilazimisha nifikie hatua ya kukuweka kwenye kundi hilo la mizoga?

Wewe huna kumbukumbu yoyote ya tuliyokwisha jadili humu, kiasi kila mara unataka nirudie kujibu yale yale kila tunapokutana?
Ndiyo maana niliwahi kukueleza kwamba hii ni njia mbovu tu ya kijinga ya kuepuka ukweli unaoujuwa. Sijui mnafundishwa shule gani hizo 'tactics' za kipuuzi namna hii
 
Hakuna mtu ambaye alikutana na hoja za mstaafu kama Ali Hassan Mwinyi, au kwa sababu aliyetoa ushauri alikuwa wa Vatican?

Warioba mpaka juzi alikuwa anatoa ushauri, haisemwi na maaskofu kwa kuwa ana reference ya ukristo?

Ni udini ?
Suala si kushauri, bali unashauri nini..!!!
 
Wewe mwenye kumbukumbu unarudi kule kule kwenye chuki. Siwezi kusema wewe una chuki ikiwa siioni kwenye hisia zako.

Samia yupo njema sana kiuongozi, usiishie kumtazama kwa fikra za humu Dar nenda huko mikoani katembee uone alivyoweza kutimiza ahadi nyingi za kwenye ilani ya uchaguzi.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
eti ee ila rohoni unajua kuwa viongozi wailslamu ndoo wanaleta neema. waulize wafanyakazi wa selikali watakupa jibu
Sasa anaye toa neema kwa kundi dogo la watu wakati wakati kundi kubwa linapata shida ndio maana wapigaji wote huwa wanapiga awamubya waislam maana ndio hawajielewi kabisa
 
Hakuna mtu ambaye alikutana na hoja za mstaafu kama Ali Hassan Mwinyi, au kwa sababu aliyetoa ushauri alikuwa wa Vatican?

Warioba mpaka juzi alikuwa anatoa ushauri, haisemwi na maaskofu kwa kuwa ana reference ya ukristo?

Ni udini ?
Pumbav kbs!! Usilete uchawa wako kweny mambo ya mustakabali wa nchi!! Mzalendo mwl JK alikua anashauri mamb ya msingi na kuonya kwaajil ya Taifa!! Kipereto wewe!!
 
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa MUNGU, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. ILA AOMBE KWA IMANI, PASIPO SHAKA YEYOTE; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa BWANA. Mtu wa nia mbili husita-sita katika njia zake zote.”
Kwenye maombi Kuna Imani ya kuomba na kuna Imani ya kupokea.
 
Wewe mwenye kumbukumbu unarudi kule kule kwenye chuki. Siwezi kusema wewe una chuki ikiwa siioni kwenye hisia zako.

Samia yupo njema sana kiuongozi, usiishie kumtazama kwa fikra za humu Dar nenda huko mikoani katembee uone alivyoweza kutimiza ahadi nyingi za kwenye ilani ya uchaguzi.
Hivi ni kipi usicho kielewa, unataka kunilazimisha niseme kuwa sina chuki na Samia Suluhu Hassan kwa sababu ya uongozi wake mbovu dhidi ya nchi yetu? Unataka niseme mara ngapi kuwa ninayachukia sana anayofanya kuhusu nchi hii kiuongozi?

Kama hutaki niwe na chuki naye, basi mwambie HAKI ya waTanzania kuwachagua viongozi wao iheshimiwe. Wakimchagua yeye kwa sababu kama unavyo sema wewe kawajengea barabara nyingi na mareli na matakataka chungu nzima, hutanisikia tena. Niache nife huko kimya kimya, nitaheshimu maamuzi ya waTanzania wenzangu.

Sasa unataka nikwambie kitu gani zaidi ya hapo.
Maana ya mimi kukuweka kwenye kundi la mizoga ni hii hii tabia ya kipumbavu sana, ambayo nyote mizoga mnayo.

Unarudia rudia takataka zilezile; over and over, kama li-robot hivi! Hivi huoni kuwa unajionyesha kuwa mtu duni sana kwa tabia za namna hii?
Sitakukumbusha tena juu ya hili; na badala yake nitakutafutia njia sahihi ya kujibu takataka hizo.
 
Si alikua mkatoliki mwenzao, yule gaidi wa kikatoliki Magufuli alivyokua madarakani kateka na kuua kapiga risasi kina Lissu ila hatujaskia wakifunga Novena tukaona wanampa vikapu achangishe sadaka kanisani
Unaweza kuja hapa kuthibitisha kuandamwa kwa aliyekuwa katibu wa TEC Pd.Raymond Saba na utawala wa Magufuli?
 
Hakuna mtu ambaye alikutana na hoja za mstaafu kama Ali Hassan Mwinyi, au kwa sababu aliyetoa ushauri alikuwa wa Vatican?

Warioba mpaka juzi alikuwa anatoa ushauri, haisemwi na maaskofu kwa kuwa ana reference ya ukristo?

Ni udini ?
Usitoe mifano isiyoendana kabsa na Tabia za kikwete kuwa karibu na Rostam Aziz mwizi wa Rasilimali za Nchi, wasitaafu wengine wana busara nyingi hawana Tabia kama za kikwete kumpitisha mama kienyeji kuwa mgombea pekee wa Urais kwa Tiketi ya ccm bila kupitia mchujo halali
 
Wakati JPM alipokuwa rais mlikuja na vilio vingi vya aina hii. Samia anahitaji kuheshimiwa kaifungua nchi kiuchumi kwa kuangalia ni kwa namna gani rasilimali zinavyoweza kuiongezea Tanzania mapato makubwa kuliko yaliyokuwa yakipatikana katika awamu zilizopita.

Suala la bandari tafuta mtu mwenye uelewa mpana akupe shule ya kueleweka ili uondokane na kuishi na dhana nyingi potofu na za kimtaani. Bandari chini ya DPW pato lake limeongezeka zaidi ya mara mbili kulinganisha na hali ilivyokuwa kabla ya kuja kwa huo uwekezaji.

Tukumbuke zile kebehi za Paul Kagame kwamba anaweza kuifanya Tanzania ikaishi kwa kujitegemea kwa kuituma bandari peke yake, Samia kazifanyia kazi kejeli zile na hivi sasa hakuna tena upigaji wa kipuuzi kutoka kwa watanzania wenzetu walioneemeka huku maslahi yetu halisi yakitelekezwa.

Hakuna namna nchi inaweza kusogea mbele bila ya kuwepo kwa tozo za aina mbalimbali. Dunia nzima inategemea kodi za aina tofauti kwa uchumi kuweza kusogea mbele. Nenda kaulize TRA kwa mwezi hivi sasa wanakusanya shilingi ngapi.

Kutekwa na kunyanyaswa kumekuwepo tangu awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere tofauti ni kwamba hivi sasa teknolojia ya habari imekua sana, hakuna siri tena kama miaka ile ya nyuma. Wakati wa Mkapa aliuliwa boss wa TISS Amrani Kombe na wasiojulikana hakuna cha ajabu kuona unyama ukiendelea kufanyika. Kwa taarifa yako sehemu ya Novena iliyosaliwa na kanisa katoliki kwa wiki nzima mpaka jumapili ya juzi inahusiana na suala zima la utekwaji wa watu.

Sekta nyingi sana zinapiga hatua kwa sasa. Viwanja vya ndege vinaendelea kukarabatiwa kwa kasi kubwa. SGR inakaribia kumaliziwa kule Kigoma, daraja la Busisi limekwisha kumalizika kujengwa, yapo mengi sana yanafanyika kwa kasi kubwa.
Bandari ni sehemu muhimu kwa usalama wa Nchi, unapowapa Wageni kusimamia sehemu nyeti kama hiyo ni hatari kwa usalama wa nchi, kusema kwamba mapato ya Bandari yameongezeka sioni uhalisia na wala Uchumi wetu haujafunguka kama unavyodai, ndiyo maana Deni la Taifa limeongezeka karibu mara mbili ya awamu zote za nyuma katika awamu hii.

Si sahihi kwa Wananchi wa hali ya chini kutozwa Tozo za kila aina huku Matajiri wakubwa wakipewa Misamaha ya Kodi.

Hata kama suala la utekaji lilikuwepo haitoi uhalali wa Watu kutokemea na kuonesha kuwa udhaifu wa Serikali iliyopo Madarakani.

Hakuna Ajira kwa Vijana, hakuna Dawa katika Zahanati na Hospitali, huduma za Elimu ni mbovu, mishahara midogo kwa Watumishi, ufisadi wa kila aina(rejea taarifa ya CAG) michango ya kila aina mashuleni, wameondoa ada lakini michango ni zaidi ya ada.

Ndiyo maana nilikwambia awali kuwa kama huoni udhaifu wa Serikali hii huenda wewe ni mnufaika au kuna wanufaika ambao una ubia nao, tofauti na hapo utakuwa ni mtoto mdogo ambaye bado hujaanza maisha.
 
Hivi ni kipi usicho kielewa, unataka kunilazimisha niseme kuwa sina chuki na Samia Suluhu Hassan kwa sababu ya uongozi wake mbovu dhidi ya nchi yetu? Unataka niseme mara ngapi kuwa ninayachukia sana anayofanya kuhusu nchi hii kiuongozi?

Kama hutaki niwe na chuki naye, basi mwambie HAKI ya waTanzania kuwachagua viongozi wao iheshimiwe. Wakimchagua yeye kwa sababu kama unavyo sema wewe kawajengea barabara nyingi na mareli na matakataka chungu nzima, hutanisikia tena. Niache nife huko kimya kimya, nitaheshimu maamuzi ya waTanzania wenzangu.

Sasa unataka nikwambie kitu gani zaidi ya hapo.
Maana ya mimi kukuweka kwenye kundi la mizoga ni hii hii tabia ya kipumbavu sana, ambayo nyote mizoga mnayo.

Unarudia rudia takataka zilezile; over and over, kama li-robot hivi! Hivi huoni kuwa unajionyesha kuwa mtu duni sana kwa tabia za namna hii?
Sitakukumbusha tena juu ya hili; na badala yake nitakutafutia njia sahihi ya kujibu takataka hizo.
Huu ni wakati wa Samia, Mungu alipanga awe rais wa JMT mwaka 2021, punguza kuishi na vinyongo vinaweza kukupa stroke na matatizo mengine ya kiafya.
 
Hakuna Mungu anayemzidi anaye simamia maslahi ya taifa hili kama yupo huyo unayemzungumzia kuweka vibaka kwenye taifa hili na kulinajisi, huyo siyo mungu ni shetani; na ninakuomba sana usirudie kutumia jina la kufuru kwa Mungu.
Ni yale yale ya mizoga. Mwenzio Tlaatlaah nilimkanya aache kukimbilia kuzungumzia maswala ya Mungu wakati akihusisha umwagaji wa damu za waTanzania na kuwateka. Sasa nawe unakuja hivyo hivyo na huyo mungu wa kishetani; hivi mmerogwa?
Mnajiambatanisha kwa Mungu huku matendo yenu yote ni ya kishetani, kwa nini?
 
Hakuna umwagaji wa damu ndani ya JMT na hautakuja utokee siku za karibuni, ondokaneni na dhana za kubuni hizo.
 
Nyerere alikua akishauri mambo ya msingi...

Kikwete ameshauri jambo gani la msingi zaidi ya wizi...

Tazama deni la taifa, rudi hapa ufafanue hiyo pesa imefanya kazi gani?
Mbona mnatumia silaha nzito sana kwenye vita za kirafiki😀
 
Back
Top Bottom